Waziri wa Kilimo Hussein Bashe zuieni uuzwaji wa chakula nje ya nchi, mfumuko wa bei unatisha!

Kwenye mfano wako hapo hapo.
Je, kufunga mipaka kunamsaidiaje huyo mkulima ambaye tayari ameuza mahindi au korosho kwa bei ndogo (bei ya shambani) ?
 
Kajilimie chakula chako jiwekee akiba siyo wanaume wenzio wakuwekee akiba
 
ili mkulima afaidike, ili watu waende kulima na wawekeze kwenye kilimo inatakiwa zoezi la kuacha mipaka wazi liwe endelevu siku zote, maisha yote.
 
Kwenye mfano wako hapo hapo.
Je, kufunga mipaka kunamsaidiaje huyo mkulima ambaye tayari ameuza mahindi au korosho kwa bei ndogo (bei ya shambani) ?
Hakumsaidii yeye binafsi kama mkulima,bali kunasaidia Watanzania wote kwani bei ya mazao ya chakula haitakuwa juu kutokana na kupatikana kwa urahisi.
 
Wanaopata faida sasa hivi hata siyo Wakulima bali wafanya Biashara!!!


Mkulima kashauza mazao yake kitambo sana kwa bei ya kutupwa!!!
 
mazao ni mali ya waliolima , uzuie mtu kuuza mali yake kwa sababu ya wanunuzi masikini wasio na hela wa kitanzania ! yaani uache vibopa wa nje ? bila shaka utakuwa umelogwa tu
 
Ni kweli mnanufaika kwa bei hiyo ila mngepambana muwezeshwe muuze unga badala ya mahindi yan hapo ndio mngepiga pesa kinyama tena ingewezekana hata mkiuzia hapa hapa TZ
Hayo tuachie wenyewe wakulima hatuhitaji ushauri wa mtu aliyekaa mezani baadaye utakuja na ushauri ohh uzeni ugali badala ya unga pikeni ugali muuze nje ukiwa umeshaiva tayari mtapata pesa zaidi kuliko mkiuza unga.

Tuachie wenyewe wakulima
 
Mfumuko wa bei ni dunia nzima kutokana na vita ya Ukraine. Siyo bongo peke yake.
 
Kifunga mipaka na kutokuuza chakula nchi jirani sio suluhisho la mfumuko wa bei za vyakula.

Unataka kuua njaa jirani zako? Wao wanapata wapi pesa za kununulia huo unga wewe ukose?

Naamini hiyo ndio bei halisi, zidisha juhudi.
 
Hakumsaidii yeye binafsi kama mkulima,bali kunasaidia Watanzania wote kwani bei ya mazao ya chakula haitakuwa juu kutokana na kupatikana kwa urahisi.
Kwahiyo kusema kwamba mipaka ifungwe kwa hoja ya kumsaidia mkulima, sio sahihi. Si ndio ?
 
Kwani wakulima hawana haki ya kupata faida? Kipindi cha Magufuli tulipata hasara kubwa sana kwa hiyo wacha na sisi tuinjoi. Hakuna mpaka kufungwa, Bashe shikilia hapo hapo
 
In the long run wafanyabiashara watashindana wao kwa wao kulingana na demnd hivyo Bei itarise na wakulima kunufaika. Jifunze uchumi vizuri
Msimu ujao mvua zikiwa nzuri wakulima watalima supply itakua kubwa zaid ya demands Bei itashuka, Bei inapanda sahivi kwa sababu supply ni ndogo iliyoshababishwa na mavuno hafifu kwenye msimu wa mahindi uliopita kwa hiyo demand kubwa ndo maana bei inapaa
We ndo hujui theory za uchumi zinavyofanya kazi
 
Kwani wakulima hawana haki ya kupata faida? Kipindi cha Magufuli tulipata hasara kubwa sana kwa hiyo wacha na sisi tuinjoi. Hakuna mpaka kufungwa, Bashe shikilia hapo hapo
Ni wakulima wachache sana wenye mazao wengi walishawauzia wafanyabiashara na wengine waliuza mazao yao tokea yakiwa shambani wanufaikaji wakubwa ni wafanyabiashara wa kupanda huku kwa bei
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…