TANZIA Waziri wa TAMISEMI Mohammedi Mchengerwa Amefiwa na Baba Yake Mzazi Akiwa Ibadani Makka Na Atazikwa hukohuko Makka

Akikujibu vema ni tag
 
Pole Sana Ila nasikia kwenda huko unabidi utumie HELA ambazo hazina makando kando.
Ni kweli kabisa ibada ya HIJA au umra inatakiwa ifanyike kwa kutumia mali zilizopatilana kwa njia ya halali!
Na sisi tunamhukumu mtu kutokana na yale tunayoyaona pasi na kidhaniana dhana mbaya au kupelelezana.
Mtu ambaye hujamkamata akiiba ukimuita mwizi wapata dhambi na kimpeleleza pia ili ujue kama ni mwizi pia ni dhambi!
Allaah amekataza kupelelezana na kudhaniana dhana mbaya katika Suurat Alhujuraat Aya ya 12 pale aliposema:
"{ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱجۡتَنِبُواْ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلظَّنِّ إِنَّ بَعۡضَ ٱلظَّنِّ إِثۡمٞۖ وَلَا تَجَسَّسُواْ وَلَا يَغۡتَب بَّعۡضُكُم بَعۡضًاۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمۡ أَن يَأۡكُلَ لَحۡمَ أَخِيهِ مَيۡتٗا فَكَرِهۡتُمُوهُۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ تَوَّابٞ رَّحِيمٞ }
Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu."
 
"Allahumma ighfir lahu warhamhu wa ‘afihi wa’fu ‘anhu wa akrim nuzulahu wa wassi’ madkhalahu waghsilhu bil-ma’i wath-thalji wal-barad, wa naqqihi mina adh-dhunubi wal-khataya kama yunaqqa ath-thawbu al-abyadu mina ad-danas, wa abdilhu daran khayran min darihi, wa ahlan khayran min ahlihi, wa adkhilhu al-jannata wa a’idhhu min ‘adhabil-qabri wa min ‘adhabin-nar."

Maana yake:
“Ewe Mwenyezi Mungu! Msamehe na umrehemu, mpe afya na umuachilie. Mheshimishe kwa mapokezi mema na mpatie nafasi pana. Muoshe kwa maji, theluji na barafu. Mtakase na madhambi kama vazi jeupe linavyotakaswa na uchafu. Mbadilishie nyumba bora kuliko aliyokuwa nayo, familia bora kuliko aliyokuwa nayo, na muingize Peponi. Muepushe na adhabu ya kaburi na moto wa Jahannam.”

Dua hii inafundishwa katika Hadithi ya Mtume Muhammad (SAW) na ni nzuri sana kwa kumuombea msamaha marehemu wa kiume. Inaweza kusomwa baada ya Swala ya Janaza au wakati wowote wa kumuombea marehemu.
 
Unaleta habari nusunusu huku tunakujua unaandika sana thread ndefu. Umeshindwa nini kuleta habari iliyokamilika na timilifu? Haya sasa, jibu maswali ya GENTAMYCINE
 
Hii Dua ni Kwa wale wanaofia Makkah au marhum Wote?
 
Sina tatizo lolote. Nimeona Wote mmetupia taarifa hiyohiyo, maudhui yaleyale, muda huohuo. Inatokea sana kwa wenye multiple ID.
Ungesoma heading usingepata shida iliyokukuta

Mimi nilimnukuu Maulid Kitenge kisha mods wakaongezea nyama na kuunganisha Uzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…