TANZIA Waziri wa TAMISEMI Mohammedi Mchengerwa Amefiwa na Baba Yake Mzazi Akiwa Ibadani Makka Na Atazikwa hukohuko Makka

Ni ule wakati ambao Papa Francis anabariki wewe kuolewa na mwanaume mwenzako huko motoni ndo wakati huo huo tunaenjoy mabikra

Ha ha ha! Sasa kwani mabikira si maandiko matakatifu ndugu yangu
 
Ela za dhulma, utawala wa dhulma ila Mungu yupo.
 
Baadhi ya maswali haya Lucas hawezi kukupa majibu sahihi kwa sababu yanahusiana na imani ya dini ya kiislamu na yeye Lucas Bado hajasilimu ( japo tunamkaribisha yeye na wewe na watu wote katika dini tukufu ya uislamu ) Licha ya kwamba kujibu maswali hayo hata kama angekuwa muislamu alitakiwa awe msomi wa dini ya kiislamu ndiyo ajibu maswali hayo.
Mimi nitajibu baadhi ya maswali ambayo ni muhimu.
SWALI la 2️⃣ Ni utaratibu uliopo kwamba kabla mtu yeyote kwenda kutekeleza ibada ya HIJA au umra lazima apimwe afya kwahiyo bila shaka hilo lilifanyiwa kazi na taasisi iliyohusika na safari yake ya kwenda huko.
SWALI la 3️⃣ ( A ) ni kwamba kwa kauli sahihi ni kwamba muislamu huzikwa katika nchi na mji aliofia endapo katika mji huo kuna waislamu wa kumfanyia haki za msingi anazostahiki kufanyiwa maiti ya kiislamu.
Yaani kuoshwa, kuvikwa sanda, kuswaliwa na kuzikwa.
Kwa mtazamo huu mchaga muislamu aliofia Kigoma au Morogoro hatosafirishwa kupelekwa Moshi bali atazikwa hapohapo katika mji ambao mauti yamemkuta.
Pamoja na hili Kuna masheikh wengine wanaoona kwamba inafaa kumsafirisha maiti kumtoa katika mji aliofia na kwenda kumzika kwao au katika mji bora zaidi kuliko mji aliofia.
(B) Mji wa makka kwetu sisi waislamu ni mji mtukufu na bora kuliko miji yote iliyopo hapa duniani.
Kwahiyo kufa na kuzikwa katika mji huo ni jambo ambalo kila muislamu analitamani na kulipenda na kwa ajili hiyo hata wale masheikh wanaoona kwamba inafaa kusafirisha maiti toka mji mmoja kwenda mji mwingine wanaona kwamba muislamu akifia mji wa makka ni bora azikwe huko huko Makka badala ya kumsafirisha kumletea Tanzania na kwa msingi huo Mimi Nina umri wa miaka 48 na nimeanza kufuatilia dini nikiwa mtoto wa miaka 11 na sijawahi kuona wala kusikia muislamu yeyote aliyefia Makka aloyesafirishwa kurudisha Tanzania.
Katika kipindi ambacho watu walikufa sana huko Makka ni tukio la mwaka 2016 ambapo waislamu walikufa sana na kwa kukanyagana kutokana na makosa yaliyofanywa na mashia wa kutoka Irani na naijeria kupita katika njia zisizoruhusiwa hatimaye wakasababisha msongamano na watu kuanguka na kukanyagana.
Pamoja na hayo najua familia za waislamu wa hapa Tanzania waliopoteza ndugu zao katika tukio hilo lakini hakuna maiti hata moja iliyoletwa hapa Tanzania toka Saudi Arabia.
SWALI lako la 4️⃣ Japo si muhimu sana ni kwamba taarifa zilizopo ni kwamba mh Rais jana kaanza ziara ya kikazi mkoani Tanga sasa aliamua kukatiza ziara kwa ajili ya msiba huu wa kifamilia au akiamua kumalizia ziara hasa kwa kuzingatia kuwa marehemu kazikwa nje ya nchi hili ni swala binafsi kwa mh Rais na familia yake.
Sawali la 5️⃣ (A) Kuhusu mazingira kwa sasa Makka hakuna msongamano wowote wa kuhatarisha maisha ya yeyote anayekwenda kufanya Ibada ya umra au kuitembelea misikiti mitukufu ya Makka na Madina kwa kuwa kipindi hiki hakuna watu wengi tofauti na msimu wa hijja ambao ndio huwa na watu wengi.
( B ) Ibada ya hijja na Umra ni lazima kwa kila muislamu mwenye uwezo wa nguvu ( afya njema )na mali ya kumpeleka na kumrudisha.
Swala la afya halina uhusiano sana na umri wa mtu ( ndio maana huwa nawaambia watu wanaomuandama Mzee Wasira kuwa umri ni namba tu kwakuwa kila mtu ana umri wake wa kuzeeka)
Tukimuangalia mh waziri Mchengerwa Bado ni kijana jambo linaloonyesha kuwa baba yake (Allaah amrehemu ) hakuwa Mzee sana kiasi kwamba hana uwezo wa kufanya mambo yake mwenyewe.
Na swala la afya na uwezo wa mwili na mali mtu hujiona yeye mwenyewe kuwa anaweza au hawezi! Pia kama afya yake hairidhishi taasisi ya HIJA na Umra inayomsafirisha inaweza kumshauri aakhirishe safari hadi afya yake ikae vizuri.
SWALI la 6️⃣ Kuhusu kwanini kazikwa huko nimeishaeleza kwenye jibu la swali namba 3️⃣ ama kwanini kazikwa haraka sana ni kwamba sheria ya kiislamu inatutaka tunapohakikisha kuwa mtu kaishafariki dunia yatakiwa tumzike haraka sana ili akaanze kulipwa ujira wa matendo yake aliyoyatenda hapa duniani.
Kwahiyo sisi hatuweki maiti mortuary wiki hadi mwezi kwakuwa tunajua hata tukimuacha mwaka mzima hawezi fufuka tena lazima tutamzuka tu.
Kwa huku Tanzania baadhi ya waislamu wanaweza kumuacha maiti hadi kesho lakini kwa nchi za kiislamu kama Saudi Arabia na nchi nyingine za kiarabu lazima wazike siku hiyohiyo.
SWALI la 7️⃣ kiasi fulani linafanana na SWALI la 2️⃣ na niseme kwamba familia ya mh Mchengerwa sio watu wanaoweza kufanya safari za kihuni bila kufuata masharti.
Ili uingie Saudi Arabia lazima uwe na visa ambayo utaipata toka ubalozi wa Saudi Arabia na ili upate visa lazima ueleze malengo ya safari yako ni nini na hapo ndipo litakuja swala la kueleza safari yako kama ni ya hijja au umra unasimamiwa na taasisi gani ? Sasa hapo ndipo litakuja swala la kuhakikisha kwamba umepimwa na kuthibitishwa kwamba hauna magonjwa ya kuambukiza na kama afya yako inaruhusu kuingia katika michakato na kanuni za ibada ya hijja na Umra!
Ahsanteni sana.
 
Afadhali umesadia kuuliza maswali niliyokuwa najiuliza maana haiwezekani mtu azikwe ugenini wakati ana mji wake, watoto, majukuu na jamaa zake.
Hizi ni akilia na fikra za kitumwa

Labda akizikwa Tanzania, pepo itakuwa mbali. Uarabuni ni jirani zaidi na ahera!!
 
Huku hakunaga Waislamu wako hawa Bakwata ambao Wana muandamo wao wa mwezi wa Ramadan

Lakini kwenye kuzika, huku unaweza kuzikwa hata kama umezimia. Fasta fasta. Wenzetu wanasubiria kwanza wajihakikishie umekufa.

Hii ya huku sio far kabisa. Inaleta mashaka sana
 
Labda akizikwa Tanzania, pepo itakuwa mbali. Uarabuni ni jirani zaidi na ahera!!
Acha umbumbumbu.Embu soma majibu ya Chifu Mkuu upate Elimu na kuondoa upofu wako wa akili. Ni post #87
 
Kweli kabisa! Hadithi inapatikana katika kitabu maarufu Cha hadithi Cha swahihi Muslim swahaba aliyemsikia Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم akisoma Dua hiyo anaitwa Aufu bin Maaliki Al Ash-jai'y anasema alipomsikia mtume akimsomea maiti Dua hiyo aliona wivu hadi akasema: Natamani Mimi ndye ningekuwa yule maiti kwa Dua hiyo ambayo maiti yule kaombewa na mtume
صلى الله عليه وآله وسلم.
 
na hakuna hela isiyo na makandokando,labda uchapishe zako!
Hii kuwa ukienda Hijja na hela za Makando kando huwezi kurudi Sio Kweli. Kuna watu chungu nzima tunawajua kuwa ni mafisadi papa wamekwenda Hijja na wamerudi!
 
Mwashambwa uwe na adabu kwa Rais.

Kauli ya 'kifo ni kifo', ni kauli ya Rais Samia. Kumwambia aliyeirudia kauli ya Rais ni mjinga maana yake unamwambia mmiliki wa kauli hiyo ni mjinga!! Ndicho ulichokusudia?
Usichukue kauli kutoka kwenye sentensi ndefu na kauli ndefu na kuisimamisha yenyewe bila miguu.
 
Pole yake...
 
Alipangiwa atakufa huko makkah. Waislam wanaamini mtu huwa anafuata kaburi lake. Na mimi natamani kulifuata kwenye taifa teule Israel nitafurahi balaa nikifa Israel.

Ritz Jagina Malaria 2 gTurn Adiosamigo 100 others and 100 others

Nyau de adriz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…