Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Mbarawa azungumza kuhusu uwekezaji wa Bandari

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Mbarawa azungumza kuhusu uwekezaji wa Bandari

sio usiri ni Hira, wangehusisha wanasheria wao ingesaidia, nina mashaka na ujuzi wa mwanashetia mkuu wa serikali kama kweli alihusika
Inawezekana na yeye ni mpendwa mtazamaji, mbona kwenye ufafanuzi hajaitwa kuelezea?
 
Inawezekana na yeye ni mpendwa mtazamaji, mbona kwenye ufafanuzi hajaitwa kuelezea?
Ni kuficha aibu, mana mkataba ule hautakiwi uwe hata na typing error. Kuna mmoja alitetetea hivyo ila sio kwa uzito wa mkataba huu.
 
Mpaka sasa nilichokipata ni kwamba Kujitoa kwenye mkataba ni ngumu. They are bitting about the Bush ...... Njia pekee ni ya Kutaifisha ambayo ni very costly.
 
Advocate Murshid Abdallah Mohammed wa Mvita, Kenya, Wafanyabiashara, makuli wapinga uwekezaji wa DP World nchini Kenya kwa sababu zifuatazo...
Ukiwaambia wanakimbilia kwenye manufaa tu hizo setbacks hawazisemi
 
Mpaka sasa nilichokipata ni kwamba Kujitoa kwenye mkataba ni ngumu. They are bitting about the Bush ...... Njia pekee ni ya Kutaifisha ambayo ni very costly.
Wewe umeona mbali sana. Kwenye hayo makubaliano kuna provision inayosema kwamba ukishasaini umesaini na haivunjiki na hakuna mazungumzo tena kinachofuta ni utekelezaji wa makubaliano na mikataba , walifanya hivyo UK wakafukuzwa, wakafanya hivyo Djibouti Jeshi likaingilia kati na kuwafurusha, wamejaribu Kenya wakamshiwa dude wakanyimwa mkataba ! Afadhali ya Kenya walitangaza tena, sisi tumeenda kuwaomba ndio mana wameona kondoo amekuja machinjioni Wacha tumchinje!

Uliona wapi kondoo aliyepelekwa machinjioni kuchinjwa akachomoka kirahisi! Ndio mana nguvu kubwa inatumkka kutetea faida badala ya kujibu vifungu vyenye ukakasi!

Weamua kubadilisha Sheria ili isuit matakwa ya DP world! Hatari sana mtu anakuja kwako anakulazimisha ubadili taratibu zako za kuishi ili kukidhi matakwa Yake halafu wabunge wanakenua meno tu!
 
Balile is a SELL OUT.

Amejioshesha dhahili kwenye hili kongamano ..... ameonyesha upande wake na amekuwa mpiga debe throughout kwenye hilo kongamano.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Muktasari:

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa amezitaja sababu za Serikali kuamua kuichagua Kampuni ya DP World katika kufanya shughuli za uboreshaji wa bandari hapa nchini.

Dar es Salaam; Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof Makame Mbarawa amezitaja sababu za Serikali kuamua kuichagua Kampuni ya DP World katika kufanya shughuli za uboreshaji wa bandari hapa nchini.


Akizungumza katika mkutano na Wahariri leo jijini hapa, Prof Mbarawa amesema DP World ina uwezo mkubwa katika uendeshaji wa shughuli za bandari barani Afrika, Asia, ulaya, Amerika ya Kaskazini na Kusini, na Australia.

“DP World ina uwezo na utaalamu wa kuchagiza katika mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka maeneo ambayo bidhaa zinatoka mpaka kwa walaji wa bidhaa hizo,” amesema Prof. mbarawa.
mbarawa-pic.jpg
 
Azungumzie mapungufu ya mkataba yanatatuliwaje hizo habari za ufanisi bandarini kila binadamu anazifahamu
Hotuba kama hizi ndizo zinathibitisha nia ovu ya hawa amijei.
Tuko kwenye mkataba wenyewe.
 


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anazungumza na Waandishi wa Habari, Jijini Dar es Salaam muda huu kuhusu uwekezaji wa Bandari.

Mbarawa:
Pamoja na Serikali kuendeleza juhudi za maboresho ya Bandari zetu, bado ufanisi katika utoaji huduma wa Bandari haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.

Hali ya ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam na nyingine nyingi zinazoendeshwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania upo chini sana, udhaifu huo unaonekana katika utendaji wa kila siku wa Bandari zetu pamoja na ukusanyaji wa mapato

Bandari ya Dar imeendelea kuwa nyuma dhidi ya Bandari shindani katika Kanda, mfano wastani wa meli kusubiri nangani ni siku 5 sawa na Saa 120 ikilinganishwa na siku 1 na saa 6 kwa bandari ya Mombasa.

Meli kutumia muda mrefu kupakia shehena kantini kwa wastani wa siku tano wakati kimataifa ni siku moja inayokubalika kimataifa.

Ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar es Salaam umetokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana mifumo ya kisasia ya TEHAMA, kutokuwepo kwa maeneo ya kutosha ndani na nje ya Bandari ya kuhifadhia shehena za mizigo pamoja na maegesho ya kutosha ya kuegeshea meli.

Changamoto nyingine ni kukosekana kwa mitambo ya kutosha na ya kisasa inayobadilika mara kwa mara kutokana na teknolojia na hivyo kuwa na gharama kubwa.

Athari za kutokuwa na ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam ni meli kusubiri muda mrefu nangani, mfano gharama ya meli kusubiri nangani kwa siku moja ni takribani Dola 25,000 (Tsh. Milioni 58).

Meli kutumia wastani wa siku tano kupakia na kupakua shehena ukilinganisha na siku 1 inayokubalika kimataifa.

Meli kubwa kutokuja katika Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kuchukua muda mrefu kuhudumiwa, hivyo kusababisha bandari yetu kuwa inayolishwa na Bandari nyingine.

Uwezo mdogo wa Bandari ya Dar unaikosesha Nchi mapato makubwa ambayo yangeweza kusaidia katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa Nchini.

Ili kutoendelea na hali hiyo, Serikali iliingia makubaliano 2000 Serikali ya Awamu ya Tatu iliingia mkataba wa upangaji na uendeshaji na Kampuni ya TICTS, mkataba ambao ulidumu kwa miaka 22 na kuipa haki za kipekee TICTS kuendesha shughuli za gati namba 8 hadi 11 za Bandari ya Dar es Salaam huku maeneo mengine yakihudumiwa na TPA.

Desemba 2022, Serikali ya Awamu ya 6 baada ya kuona mkataba hauendani na maslahi mapana ya Nchi yetu iliamua kusitisha mkataba huo.

Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania ilipokea mapendekezo ya wawekezaji mbalimbali Duniani, lengo kuu likiwa ni kufungua masoko ya kimkakati katika kufungua eneo la bidhaa na usafirishaji ndani ya Nchi na maeneo yanayotuzunguka.

Baada ya uchambuzi wa kina Serikali ilianzisha majadiliano na Kampuni ya DP World kwa sababu zifuatazo:

Uwezo mkubwa wa uendeshaji wa shughuli za Bandari Afrika, Asia, Ulaya, Marekani ya Kaskazini na Kusini na Australia.

DP World ina uwezo na kuchagiza mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka maeneo ambapo bidhaa zinatoka hadi kwa walaji wa bidhaa.

DP World inamiliki zaidi ya meli 400 za mizigo, ina uzoefu wa uendeshaji wa Bandari 6 Afrika na zaidi ya Bandari 30 Duniani kote.

Wawekezaji wengine waliowasilisha mapendekezo yao hayakukidhi sifa kwa mwekezaji ambaye alihitajika.

Mkurugenzi TCCA: Hakuna ardhi ya Tanzania ambayo itauzwa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini, Hamza Johari amewatoa hofu Watanzania kuhusu tarifa za kuwa nchi imeuzwa kutokana na mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai akisema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.

Kauli hiyo ameitoa leo Julai 14, 2023 alipokuwa akizungumza katika mkutano na wahariri jijini Dar es Salaam huku akiwataka watu kutoingiza siasa kwenye masuala yahusuyo uchumi wa nchi na kusisitiza kuwa mkataba huo ni mzuri.

Ni kampuni kubwa sana hii ya DP World, ndio walioinunua P & O Nedlloyd pamoja na Maersk. Wengi wetu ni ujuaji mwingi tu ni tatizo lile lile la kukosa ufahamu wa muda husika wanaita exposure.
 
Huyu ni kanjanja hajajibu hoja za Mwabukusi, Dr. Slaa, Lisu, Dr. Nshala na wengine
Hao uliowataja wameongelea vipande vya mkataba, kwa malengo maalum ya kukupotosha wewe Retired na wasomaji wengine humu.

Hawana uwezo wa kuuongelea mkataba mzima kwa ujumla wake.
 
Binafsi kwenye Hili Hamza kajitahidi sana kueleza kitaalamu kwa asilikia kubwa sijasema asilimia 100

Ila yuko vizuri ukimsikiliza Hamza mtu kama mimi Mkristo nasali kwa Mwamposya sipendi uongo wala unafiki nikipewa taarifa sahihi binafsi naona kabisa Hamza alifanya kazi yake vizuri mno akiwa na dhamiri njema mno kwa maslahi ya nchi kwa asilimia kubwa

Mimi.nimemuelewa hiyo nafasi ya kiofisi aliyonayo kama mkurugenzi wa Anga ni ndogo mno ukilinganisha na uwezo wa akili yake anastahili kuwa na na nafasi kubwa zaidi
Kama hukusomea sheria nikupe siri.
Unaweza kufafanuliwa jambo kiufasaha lakini nje ya uhalisia wenyewe. (Out of content and context)
Uliwai kujiuliza mawakili huwa wanabishania nini mahakaman wakati sheria rejea zinakuwa zile zile!
Mfano mzuri ni huu.
Leo zimejengwa hoja nzuri kuhusu mapungufu ya bandar kwa sasa na faida za uwekezaji.
Je, hilo ndo tatizo la wanaokataa?
 
Ukiwaambia wanakimbilia kwenye manufaa tu hizo setbacks hawazisemi



Na manufaa yenyewe interms of nini Kwa mfano?

Je kiasi cha pesa kitachopatikana ni kiasi gani?

Kuanzia muda gani tangu kazi kuanza?
 
Hivi Hamza Johari ni nani katika mkataba huu? Anaupambania sana
Amesema yeye ndio alieuandaa huu mkataba na anajua tofauti ya BIT na IGA na HGA mimi najua BIT tu hizo nyingine sizijui kwa hiyo hakutufafanulia tofauti ya BIT na IGA na HGA alisema IGA na HGA ni Viena convection ya 1969 sawa lakini mikataba yote hutumia Viena convection kwa hiyo kutakuwa na confusions nyingi sana kwenye hii kitu ila time will tell
 
Hajajibu maswali ambayo mm na familia yangu pamoja na ukoo wangu tunataka kujua uyo DP - WD. Makubaliano/mkataba ni w miaka mingapi?

Yani wandishi w Habari wa Tanzania hawajui kuhoji wao ni Ndioooooooooo kama wabunge tu.
Hawakuwa waandishi walikuwa wapambe sijawahi ona mwandishi aliekwenda shule anauliza maswali namna ile??Wengine walikuwa wanauliza maswali na kujijibu wenyewe kweli Tanzania ni nchi ya miujiza
 
Kiukweli Waziri Mbarawa na timu yake wamejitahidi kujibu maswali ya wahariri na wametoa ufafanuzi mzuri.

Mimi binafsi nimefurahi kupata maelezo ya maswali mengi tuliyokuwa tunajadili hapa jamvini.

Mfano ukomo wa mkataba na namna ya kuuvunja mkataba
Kikubwa ni kwamba kumbe bado Kuna vitu vingi vinakuja kujadliwa sisi tumewahi sana kuhukumu.

Kwa maelezo ya leo naamini serikali Ina nia njema kwa nchi yetu . Tuwe na subira.
KAZI INDELEE
 
Kiukweli Waziri Mbalawa na timu yake wamejitahidi kujibu maswali ya wahariri na wametoa ufafanuzi mzuri. Mimi binafsi nimefurahi kupata maelezo ya maswali mengi tuliyokuwa tunajadili hapa jamvini. Mfano ukomo wa mkataba na namna ya kuuvunja mkataba
Kikubwa ni kwamba kumbe bado Kuna vitu vingi vinakuja kujadliwa sisi tumewahi sana kuhukumu. Kwa maelezo ya leo naamini serikali Ina nia njema kwa nchi yetu . Tuwe na subira.
KAZI INDELEE
Ulipomalizia KAZI UENDELEE!
Umetia mashaka juu ya andiko lako!

Wakati mwingine unapojaribu kutoa Elimu kwa watanzania, usiweke mazingira yakufanya watu wakuhisi unaongea kwa maslahi ya CCM na Mwenyekiti wake!
 
Back
Top Bottom