Mungu hakuwa mjinga kuwaacha wasambae dunia nzima kama mateka na wakimbizi .
Wakati wa kuwarejesha kwao umefika .
Ni wapumbavu tu wanaobisha uwepo wa Mungu na historia ya kutokea kwa Taifa hilo ambalo asili yake ni Uajemi. Kwa hiyo hao wa Israel ni waajemi kwa asili ndio maana hata ndani ya Iran wapo . Urusi wapo ,Itali wapo ,Uingereza ,wapo,Ujerumani ,wapo,Marekani wapo ,Ufaransa wa wapo , Na nchi zote karibu zote za Ulaya mashariki wapo ,Afrika ya Kaskazini wapo ,Afrika kusini wapo, mashariki ya kati ndio wamejichanganya kila mahali. Sasa katika hali hiyo watakosaje watu wa kuwapigania kwa kiwango chochote .
Na Marekani mara nyingi wanaingilia hiyo vita ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza kutokea kwa sababu ni wazi kuwa katika teknolojia wanayoibuni kila siku mayahudi hawawezi kukubali taifa lao liangamizwe na mtu yeyote . Katika hali ya kutetea taifa lao watajibu mapigo ya kuangamiza watu wengi na miundombinu na miradi ya Nchi za magharibi ikiwemo visima vya mafuta na pia miradi ya Nyuklia inayofadhiliwa na Urusi . Kwa ni busara tu inayotumika kuionya Israel kuingia kwenye nchi na nchi kama Irani yenye watawala magaidi wanaosaidiwa na Urusi bila kujua kuwa vita haina macho . Iraki ilikua na nguvu kubwa sana lakini ilipoanza kuhangaika na Mombo ya Israel badala ya maendeleo yake ikasambaratishwa .
Libya ilikua na nguvu na uchumi mkubwa sana ilipoanza kuhangaika na mambo ya Israel na kutisha kuifuta kwenye Ramani ya dunia ,ilisambaratishwa. Ujerumani lilikua taifa kubwa lenye nguvu kubwa sana na Hitler akiwa mtawala mtata sana ,kosa la kuwaza kuwafuta wayahudi kwenye uso wa dunia likawa ni anguko lake . Sasa kwa satu wanaofikiri kuwa bibilia ni kijitabu tu wataabika sana Irani itakapoanguka na kupotea kabisa kwenye nchi kubwa duniani .
Mungu aliwaweka pale kwa kazi yake na alijua ni wabishi na wanamsimamo mgumu sana lakini wakati wa kusudi lake ukitimia watarejea na kuwa watiifu kwa Masihi Yeshua au Yesu.
Irani pia inadhaminiwa na Urusi na China na Korea ,Yote hayo ni Mataifa makubwa yenye nguvu za kiuchumi .
Irani kama Irani haina uwezo bila kuwa na marafiki wenye nguvu .
Ukiona marafiki danampambambania rafiki yao basi ujue ana manufaa kwao.
Kwa hiyo Irani ikijidanganya kuwa itaishambulia Israel ijue ndio mwisho wake kwa sababu Israel ina watu wenye uwezo mkubwa wa kisayansi na wamejiwekeza kwenye Mataifa makubwa ya magharibu.
Muda utasema na maandiko yatatimilika kama yalivyoandikwa.