Waziri ya Afya, Kwa Sasa mama mjamzito kadi ya clinic anauziwa 10,000. Akijifungua mtoto wa kike 15,000 wakiume 30,000

Wapi
 
Ni sawa na yale yanayotokea ukienda kulipia leseni ya biashara wilaya ya Temeke. Utaambiwa ukajazie taarifa zako kwenye stationary moja iko nje hapo, sijui wanahusiana vipi
 
Kwanini usigome kuweka hiyo vocha?
 
.
Kadi imeandikwa Bure halafu uuziwe si waandike kadi hii inauzwa Tsh10,000.
Tumia akiri kidogo, kadi zinachapishwa nyingi tu kwa wakati mmoja na yawezekana zikachapishwa za kutumia miaka 2 au 3 mbele inapotokea mabadiriko hawawezi kuzichoma moto zilizopo bali anafuta sehemu isiyohusika na kukuandikia 10,000 au anaacha hivyohivyo.
 
Kati yangu nawewe nani hajatumia akiri kabisa?

Bajeti iliyopangwa Kwa ajiri ya mama na mtoto apatiwe huduma Bure hata kama ni miaka 10 kama walichapisha Kwa muda hu ni lazima muda huo ufike ndo mabadiriko yatokee.

Ikitokea badiriko lazima waweke matangazo na kuondoa ya zamani kuwa huduma za mama mjamzito na mtoto Kwa Sasa ni kulipia.

Kwa Sasa Kila kitu Kiko vilevile mabango yte Yana sema huduma ni Bure.
 
Sawa mkuu Wacha nitumie hiyo kidogo.
 
Mzilankende alisema wafyatue tu na hakuna katazo jipya unawalaumu nini 😂😂
 
Ni kwa sheria ipi inayowalazimisha kuweka matangazo, nitajie kifungu na mwaka.
 
NHIF Imekufa Ummy akiwa waziri.
Bima ya watoto wadogo imeyeyuka Ummy akiwa waziri.
Jukwaani anasema Samia amepunguza vifo vya kinamama wakati wa kujifungua kumbe hata kile kijikaratasi Cha taarifa za mama na mtoto Ni sh 10,000. Huyu Ummy ambaye sio daktari si ampishe @dkt.gwajima D kwenye wizara?
Kushika mimba kwa Sasa Ummy akiwa waziri Ni Kama jinsi Fulani hivi.
Private hospital kujifungua Ni kwa operation kwa gharama ndoogo ya milioni moja. Ukienda serikalini wamama ward ya labour utawakuta wanalala mzungu wa nne, treatment wanayo pata kutoka kwa MANESI inatia wasiwasi.
 
Sahihi kabisa mr
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…