WAZO: kwanini serikali isipunguze muda wa kustaafu kwa watumishi wa umma

Dah Kwahiyo unadhani hao ndo wamesababisha uwe jobless?
Hata tukiacha wote kazi nafasi zilizopo kwenye sekta ya umma haifiki 1M...Labda ungelalamika hao waliopo makazini wanafanya Nini katika kuongeza ajira?
 
Yaan tuanzie kijana anaitaka nafasi ya mtu mwingine.badala ya serikali kuwezesha kuleta kwenye uchumi uwekezaji zije ajira mpya ,yaan chakula hakitoshi kwenye harusi suruhisho ninkila mtu ale nusu sio chakula kiongezwe??? Huu ni ushauri wa kukata tamaa kabisa .
Ifahamike hata hao ukiwastaafisha miaka 50 nao sio kuwa watajiajiri wataanza tafuta kazi tatizo hapa ni
1.sekta binafsi haijawezeshwa kuzalisha ajira ili kuondoa nakisi
2.serikali haijaweka mikakati ya vijana kupata mtaji wakuweza kujiajiri
3.vijana hawana uwezo sio kuwa wajinga bali elimu wqnayopewa haijawaandaa kujiajiri bali kuwa mabank teller na mameneja .

Aidha nikuongezee muajiriwa huwa anakuwa mzuri kadili anavotumikia muda mrefu kuanzia kuwa na uzoefu ,kuwa wanamjua in and out kuwa anakuwa more commited .ofisini kwangu baada ya interview ya wahasibu 1000 tuliajiri watatu mwaka huu .yaan ukikaa nao stori zao ni kununua subaru kula bata kutafuta mtaji kujiajiri.wakati hawa wenye 50 wao huzungumzia malezi ya watoto wao ,kupandishwa cheo na mshahara .unazani muajiri atampenda nani?
Hawa tulionao tulikuwa na wahasibu 10 wa4 walisharesgn kwa kuiba mara kupata ajira ingine etc ila hawa wakongwe 6 yaan they are here to stay na unaona kabisa wanaipenda kampuni mpaka baa wanava tshet za kampuni
 
Hii inaweza saidia kupunguza tatizo la ajira nchini ikibidi kutoka

Naunga mkono hoja. Uchumi ukue ili ajira ziwe nyingi. Tuzalishe bidhaa zenye viwangi vya kimataifa ili tuuze hadi nje ya nchi. Kwa kufanya hivyo wote wataajiliwa na hatutatosha. Mfano kilimo kikiboleshwa then tuuze unga Africa mzima mbona watu tutaona mijin hakuna maana
 
Alale usingizi wa pono huko aliko!
 
Nakuunga mkono wazo zuri sana lakini siyo kwa swala la ajira,
Hii ni kwa mfanyakazi mwenyewe apate muda wa kuzifaidi na kutumia nguvu zake

Kuhusu ajira watu wangewekewa option ya kusaini mikataba mfano miaka 15 ikiisha either usaini upya mkataba mwingine au ustaafu upishe wengine
 
TUMIA AKILI
 
Ajira serikali inatakiwa kuwa miaka 18 tu isipokuwa kwa wachache walio chaguliwa kwa ufanisi wao na ubora wao na ndani ya hiyo miaka 18 mkataba uwe ni miaka 6 una sahini tena miaka 6 na baada ya hapo una sahini tena 6 ya mwisho
 
Kwa Kada ya afya sawa, ila majority ya graduates wamesoma kozi ambazo ni Managerial. Watu wa afya bado ni wachache compared na wengi ambao hawajasoma afya.
 
Lengo la kufanya hivyo ni kuongeza wigo mpana wa watu kujiajiri. Mna encourage watu kujiajiri ila mtu atajiajiri vipi bila kuwa na mtaji?

Aliyetoka kazini mfano mzuri wale watu waliokuwa kwenye ma NGO's ambao wamerudi mtaani wengi waliofanya kazi kwa miaka 10 tu hawakosi 50M au zaidi kwenye savings zao.

Sasa mtu kama huyo utamfananisha na graduate ambaye hana hata shillingi mia kwenye account na ana madeni ya HESLB kisha unamfosi ajiajiri wakati hela za mtaji hana.
 
Hii inaweza saidia kupunguza tatizo la ajira nchini ikibidi kutoka miaka 60 mpka 45 au 50 ili vijana nao wapate nafasi kwani hii itatoa nafasi nyingi katika kada mbalimbali .
Ni wazo zuri ila lingetazamwa suala la kupunguza kwanza matumizi holela ya serikali ili fedha ielekezwe kwenye kupanua wigo wa ajira kwa vijana, kwa mfano hivi sasa bunge ni kubwa mno na fedha inayotumika huko ni nyingi mno, hakuna sababu ya kuongeza wabunge na madiwani wakati huu. Pili ununuzi wa magari ya kifahari nao unachangia sana katika kuzorotesha uchumi, kwa mfano tukibana matumizi ya serikali fedha hiyo ikakopeshwa kwa vijana wakafungua miradi ya kilimo, ufundi na ufugaji tatizo la ajira litapungua pia
 
Hiko halimalizi tatizo, sema litatengenezwa tatizo la watu wazima wengi kuwa jobless pia.Hao wote watakaostaafu automatically wanaenda kuwa jobless.
Pili serikali ni watu sio hewa, thus hawawezi wao wakajihujumu, kujipunguzia miaka ya ulaji - NEVER
 
Mifuko ya hfadhi ya jamii inazidi kufirisika duniani kote..... Tegemea muda WA kustaafu unaongezwa kuanzia 2040 huko Hadi 65 kwa lazima.

Wenye maamuzi umri wao ni 50+
 
wabunge wakitumia kruger harrier sio mbaya
 
Sasa Hata makato ya HELSB yatakuwa yameisha Kweli 🤣
Au atayamalizia Akiwa Mtaani baada ya Kustaafu..?

HAmuoni kuwa mtatengeneza mazingira ya Rushwa makubwa na Mtu kuharibu kazi kwa makusudi akijua muda wake umekaribia kuisha?
 
Hii inaweza saidia kupunguza tatizo la ajira nchini ikibidi kutoka miaka 60 mpka 45 au 50 ili vijana nao wapate nafasi kwani hii itatoa nafasi nyingi katika kada mbalimbali .
Ungekuwa muajiriwa serikalini usingeleta hili wazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…