Mkuu kwanza Kabisa naomba Nikubaliane na wewe Kwamba Ninaweza Kuwa Mpumbavu kwako kwa Hoja Nilizozitoa!
Pili Nimesikitika Sana kama Serikali inazalisha Wasomi Kaliba yako,Naomba Nikiri kwamba Tuna Safari ndefu sana Ya kujenga Nchi yetu Kuliko Tulivyokuwa tunatarajia..
Kabla ya kukujibu hoja zako (Ambazo nikiri Ni dhaifu sana) hebu tuangalie kwa umakini mambo kadhaa:
Umejikita kwenye Ad Hominem Logical Fallacy yaani Badala ya kushambulia hoja, wewe Umeanza kushambulia mtu binafsi kwanza kwa kuniita "mpumbavu" na kudharau taaluma yangu ya udaktari. Kwanza Kabisa Hoja Haipingwi kwa Kumtukana Mtoa Hoja Hoja Inapngwa kwa kuitukana Hoja Yenyewe
Hapo Juu Nimekueleza Kuhusu Marekani Na Nchi za Ulaya kama Miongozo yetu kama Afrika Kwa kuwa ni Nchi zilizoendelea ila badala ya Kujadili Hoja Hizo umekuja na False Equivalence Fallacy unajaribu kusema huwezi kulinganisha Marekani na Tanzania bila kueleza kwanini. Hata hivyo, hoja zangu hazikuhitaji Marekani na Tanzania ziwe sawa kwa kila kipengele, bali zinazingatia msingi wa uhalisia wa ajira duniani kote, siyo tu kwa nchi moja.
Mwisho kabisa unaleta Strawman kwakuwa Hujajibu hoja yangu yoyote ya msingi kuhusu elimu ya kujitegemea na matumizi mabaya ya rasilimali za serikali, badala yake umeegemea katika kulinganisha kiwango cha maisha cha Tanzania na Marekani, ambacho si kiini cha hoja yangu
Sasa kwakuwa Ulijielekeza Vibaya Naombq nichukue nafasi Hii Kukuelekeza Vizuri
Tatizo la ajira si suala la kuwaondoa waliopo kazini bali ni suala la kuongeza nafasi za ajira kwa njia endelevu.
Yaani Kuzima moto nyumba ya Jirani Hakumaanishi Moto Ule Uuhamishie Kwenye Mapori..
Utakuwa Ni akili za Pwagu na Pwaguzi..
kama Unaona kupunguza umri wa kustaafu ndio suluhisho la upungufu wa ajira, basi tungeona nchi zote duniani zikifanya hivyo. Badala yake, nchi zilizoendelea zinaweka mfumo wa kujiajiri na sera za uwezeshaji wa ajira, siyo kufukuza waliopo kazini.
we Unahisi Kwa nini mtu atumie miaka 30+ kusoma halafu afanye kazi miaka 10 tu? Unajua Mtumishi Anatumia Mwaka mmoja Kuchunguzwa (Kuwekwa On probation) na kwa sasa Anapata Seniority Ndani ya Miaka Mitano So Nchi ambayo Senior Employee wote wanastaff ila Junior Staff wanabaki kazini Si nchi ambayo inaweza ikafanya maendeleo kwenye Jamii yoyote..
na si tu kwamba itaathiri uchumi, bali pia itaathiri mfumo wa kijamii kwa kuleta mzigo mkubwa wa kiuchumi kwa wastaafu wenye umri mdogo sana...
Yaani Tutakuwa na Mzigo Mkubwa Ndani ya Jamii Kuwa na Wastaafu wenye Umri wa Miaka 45 Huku Life Expectancy Ikiwa ni miaka 65 kwa Tanzania..
So Unahisi Huyu Mtumishi Uliyemeachisha Kazi Kw miaka 20 Yote Anafanya nini kwenye Jamii?
Unatengeneza Umaskini Kwenye Nchi Kwa Kiwango kikubwa Tunashuhudia Wastaafu wengi wakiishi Maisha Ya shida sana..
Nikuondoe Wasiwasi kwa Sera ya Afya Ulimwenguni..
Kwa Kazi yangu Nayofanya Umri wa Kustaafu ni Miaka 60 mpaka 65 Dunia nzima so relax ...
Sasa Nakukaribisha Kama Utaweza Kufanya Mjadala Bila Ya Matusi Kuhusu Hili swala Nipo hapa..