Wazungu wakiendelea kukaza hivi hivi hadi mwisho inaweza kutuchukua muda gani kuingia katika total economic crisis?

Hata wakaze Hadi wazeeke wataambulia zero gain
Screenshot_20260804-141920.jpg
 
Economists,
Planners,
Financial analysts,
Insiders,
Strategists,
JFers,

Karibuni.
Tukimuita Kitila Mkumbo atakana yote na kutuambia mbona tulianza kujitegemea zamani!Sioni uimara wa kiuchumi kama nchi kuweza kujisimamia kwa miaka miwili.
NB;Timu itumwe Iran ikajifunze ujuzi wa kuishi kwa vikwazo na mkwamo wa kiuchumi.
 
... sanasana watatuharakisha kubobea upande wa pili ambako tunasubiriwa kwa hamu!
NB: Dunia ni 'MULTIPOLAR' sasa hivi na si muda mrefu vita vya kugombania wafuasi itakolea!
Ninawaonea huruma wanaofikiria vikwazo vitaleta mageuzi ya kisiasa, maana mimi ninachoona ni nchi kuzama zaidi China na Urussi ambapo hizo mambo sio 'issue'!
 
Hatuwezi kuingia kwenye "economic crisis" tutakuwa tuu na nakisi kubwa ya kibajeti "Budget deficit", bajeti yetu inategemea % wahisani, mikopo na ruzuku kutoka kwa nchi wahisani, EU,Bretton Woods (IMF & WB) na wengine.

Kuwa na nakisi ya bajeti, maana yake ni kwamba tutashindwa gharamia matumizi mengi ya kimaendeleo kutokana na "cut" ya sehemu ya bajeti inayotegemea mikopo, ruzuku na hisani.
Ndio maana unaoana miradi mingi hasa ya kimakakati inasua sua, bodi ya barabara hakuna fedha, deni la taifa linaongezeka sababu ya kuongezeka kwa kasi ya kukopa ili ku "finance" miradi.

Kauli ya waziri; Kitila Mkumbo kusema kwamba hatutateteleka kwa wahisani kuminya misaada na mikopo; ni kauli ya kisiasa ya kujilisha upepo. Katika bajeti "every single coin counts". Kama ulikuwa unapata $400M kila mwaka kutoka Umoja wa Ulaya kufanya matumizi ya kibajeti kama ruzuku/grant,ukizikosa hizo maana yake utafute namna nyingine ya kuzipata au uachane na miradi hiyo. Au ubaini vyanzo vipya vya kodi, au ukope au utafute hisani.

Ni kauli ya kujipa moyo. Angalia bei ya kuingiza magari imepaa, gari iliyokuwa inanunuliwa Japan kwa 17M sasa hivi ni 19, 20M. CIF ndogo, clearance costs kubwa.

Ushauri: Huyu mama akubali masharti ya wahisani. Mbona Mwinyi na Mkapa walikubali "Structural Adjustment Program- SAP's). Tutakubaki ubanafsishaji, uchumi wa soko, na demokrasia, tukavimba kwenye "Shillings devaluation". Nchi kama ya kwetu huwezi wavimbia watu wanaokusaidia karibia 40% ya budget's expenditures, ni sawa na mtoto akimbie viboko nyumbani, akachezee, arudi usiku viboko vipo pale pale, atachapwa tuu. 😊
 
Kauli ya waziri; Kitala Mkumbo kusema kwamba hatutateteleka kwa wahisani kuminya misaada na mikopo; ni kauli ya kisiasa ya kujilisha upepo. Katika bajeti "every single coin counts". Kama ulikuwa unapata $400 kila mwaka kutoka Umoja wa Ulaya kufanya matumizi ya kibajeti, ukizikosa hizo maana yake utafute namna nyingine ya kuzipata. Au ubaini vyanzo vipya vya kodi, au ukope au utafute hisani.

Ni kauli ya kujipa moyo. Angalia bei ya kuingiza magari imepaa, gari iliyokuwa inanunuliwa Japan kwa 17M sasa hivi ni 19, 20M. CIF ndogo, clearance costs kubwa.

Ushauri: Huyu mama akubali masharti ya wahisani. Mbona Mwinyi na Mkapa walikubali "Structural Adjustment Program- SAP's). Tutakubaki ubanafsishaji, uchumi wa soko, na demokrasia, tukavimba kwenye "Shillings devaluation". Nchi kama ya kwetu huwezi wavimbia watu wanaokusaidia karibia 40% ya budget's expenditures, ni sawa na mtoto akimbie viboko nyumbani, akachezee, arudi usiku viboko vipo pale pale, atachapwa tuu. 😊
Asante sana CPA...
 
Wazungu lini waliachia?

Au hujui unachouliza?

Mbona unaota ndoto za mchana? Ni lini wazungu walikaza dhidi ya Tanzania?

Nchi pekee za Afrika ambazo zimewahi kupata kibano cha kiuchumi kutokana na ukiukaji wa haki na demokrasia ni Liberia, Sierra Leone na Zimbabwe.
Kibano kwenye nchi hizo kilihusisha kuzuia nchi zote kununua madini kutoka kwente mataifa hayo.

Fikiria leo hii, Tanzania iwe kwenye vikwazo vya kiuchumi, tusiruhusiwe kuuza madini nje, wala watalii kuingia nchini. Ufahamu kuwa sekta ya utalii na madini ndizo chanzo pekee kikuu cha pesa ya kigeni.
Zimbabwe ambayo ilikuwa na uchumi na maendeleo mazuri kuliko Tanzania kabla ya vikwazo, leo ni duni kwa kiwango ambacho ni vigumu kuelezea.

Tuombee tusifikie huko. Tukifika huko, waliotusababishia wataondoka nchini, na kuiacha laana kwa wahanga wanaokushdiwa kusaidiwa na hivyo vikwazo.
 
Hata Cuba wana viwanda vikubwa sana vya sukari toka walipo anza kuwekewa vikwazo.
Uchumi wao upoje? Vipuri na chemicals zingine zinazo takiws kwenye viwanda tutatoa wapi?
Tukifanikiwa uzalishaji mkubwa tutauza nje ya nchi wakati wa vikwazo?
Uchumi wao uko vizuri kwani una shida gani?
 
Inategemea na shock absorbers zetu, lakini miezi 8 hadi 12 ni mingi sana.

Maana sisi ni nchi inayotegemea kuagiza bidhaa nyingi kutoka nje kuanzia teknolojia hadi mafuta. Thamani ya shilingi ikishuka kwa sababu yao maana yake bei ya kila kitu itapanda mara mbili au tatu. Hapo ndio utaona mshahara wa mtu mzima unatosha kununua mahitaji ya ndani tu.
 
Hatuwezi kuingia kwenye "economic crisis" tutakuwa tuu na nakisi kubwa ya kibajeti "Budget deficit", bajeti yetu inategemea % wahisani, mikopo na ruzuku kutoka kwa nchi wahisani, EU,Bretton Woods (IMF & WB) na wengine.

Kuwa na nakisi ya bajeti, maana yake ni kwamba tutashindwa gharamia matumizi mengi ya kimaendeleo kutokana na "cut" ya sehemu ya bajeti inayotegemea mikopo, ruzuku na hisani.
Ndio maana unaoana miradi mingi hasa ya kimakakati inasua sua, bodi ya barabara hakuna fedha, deni la taifa linaongezeka sababu ya kuongezeka kwa kasi ya kukopa ili ku "finance" miradi.

Kauli ya waziri; Kitila Mkumbo kusema kwamba hatutateteleka kwa wahisani kuminya misaada na mikopo; ni kauli ya kisiasa ya kujilisha upepo. Katika bajeti "every single coin counts". Kama ulikuwa unapata $400M kila mwaka kutoka Umoja wa Ulaya kufanya matumizi ya kibajeti kama ruzuku/grant,ukizikosa hizo maana yake utafute namna nyingine ya kuzipata au uachane na miradi hiyo. Au ubaini vyanzo vipya vya kodi, au ukope au utafute hisani.

Ni kauli ya kujipa moyo. Angalia bei ya kuingiza magari imepaa, gari iliyokuwa inanunuliwa Japan kwa 17M sasa hivi ni 19, 20M. CIF ndogo, clearance costs kubwa.

Ushauri: Huyu mama akubali masharti ya wahisani. Mbona Mwinyi na Mkapa walikubali "Structural Adjustment Program- SAP's). Tutakubaki ubanafsishaji, uchumi wa soko, na demokrasia, tukavimba kwenye "Shillings devaluation". Nchi kama ya kwetu huwezi wavimbia watu wanaokusaidia karibia 40% ya budget's expenditures, ni sawa na mtoto akimbie viboko nyumbani, akachezee, arudi usiku viboko vipo pale pale, atachapwa tuu. 😊
🔥🔥🔥
 
Hata Cuba wana viwanda vikubwa sana vya sukari toka walipo anza kuwekewa vikwazo.
Uchumi wao upoje? Vipuri na chemicals zingine zinazo takiws kwenye viwanda tutatoa wapi?
Tukifanikiwa uzalishaji mkubwa tutauza nje ya nchi wakati wa vikwazo?
😁😁🔥🔥
 
Mbona unaota ndoto za mchana? Ni lini wazungu walikaza dhidi ya Tanzania?

Nchi pekee za Afrika ambazo zimewahi kupata kibano cha kiuchumi kutokana na ukiukaji wa haki na demokrasia ni Liberia, Sierra Leone na Zimbabwe.
Kibano kwenye nchi hizo kilihusisha kuzuia nchi zote kununua madini kutoka kwente mataifa hayo.

Fikiria leo hii, Tanzania iwe kwenye vikwazo vya kiuchumi, tusiruhusiwe kuuza madini nje, wala watalii kuingia nchini. Ufahamu kuwa sekta ya utalii na madini ndizo chanzo pekee kikuu cha pesa ya kigeni.
Zimbabwe ambayo ilikuwa na uchumi na maendeleo mazuri kuliko Tanzania kabla ya vikwazo, leo ni duni kwa kiwango ambacho ni vigumu kuelezea.

Tuombee tusifikie huko. Tukifika huko, waliotusababishia wataondoka nchini, na kuiacha laana kwa wahanga wanaokushdiwa kusaidiwa na hivyo vikwazo.
😁😁🔥🔥🔥
 
Back
Top Bottom