Wazungu/West wako mbali sana, wamefikia hadi kwenye supu ya box/kopo!

Wazungu/West wako mbali sana, wamefikia hadi kwenye supu ya box/kopo!

Inategemeana mkuu kwa Amerika wananiambia ukitaka kula kitu fresh kama nyama ya ngombe au ya kuku unatakiwa uwe na pesa asilimia kubwa vya kula vingi ni vya supar market xa makopo lakini uhalisia unachokula sio
Wamekudanganya, vyakula vyote huko vinauzwa supermarket. Junk foods vyakula vya mtaani ndio vinapigiwa kelele na vinaliwa karibia na kila mtu.
 
Vyakula vya Makopo vina sumu na huko wanakula maskini, vyakula vya asili wanakula wenye uwezo....

Hahaha wabongo kwa ujuaji bana dah nawakubali, unaweza kukuta huyu ni msomi kbs ati! Yani watu kutunza chakula kipatikane muda wowote kinakua sumu? Nyie msokula sumu mna afya gani ya maana? Mnahara na kuishia miaka 50 tu hao unaosema wanakula sumu wanapiga miaka 100+
 
Unashangaa Supu ya kopo ni ubunifu tu ila sisi unauza karanga peke yake na korosho peke yake wakati nyie ndio walimaji
Zikija kwa wazungu wanachanganya kila aina na utamu wake unashangaa
Ila sisi akili nzito aise
Juzi nimeenda supermarket nimenunua juice ya apple iliyochanganywa na maua bisha sasa
Sisi maua ni kunusa tu na ndio tunayo kila kona
Juice za matunda wanachanganya na matango au mchicha kabisa
 
Hivi uanjua US ni taifa dhaifu sana kwa upande wa afya za watu wake, obesity ni janga kubwa kwao.

Unajua ni makampuni mangapi ya vyakula kutokea USA yamepigwa marufuku kufanya biashara katika mataifa mengine?
Watu 300m vs 60m unategemw ratio nzurii , pili nchi iliyowekeza kwenye singeli na udaku Kwa upande wa media VS nchi inayogusia Kila nyanja za maisha ya raia wake , unategemea Tz wakianza fuatilia afya za watu tutabakia Salam , Tz tuna wagonjwa WENGI san wanajulikana baada ya kuleta mahospitalini Kwa magonjwa mengine
 
Watu 300m vs 60m unategemw ratio nzurii , pili nchi iliyowekeza kwenye singeli na udaku Kwa upande wa media VS nchi inayogusia Kila nyanja za maisha ya raia wake , unategemea Tz wakianza fuatilia afya za watu tutabakia Salam , Tz tuna wagonjwa WENGI san wanajulikana baada ya kuleta mahospitalini Kwa magonjwa mengine
Sijakataa kwamba Tz hakuna wagonjwa, na hakuna nchi ambayo hakuna wagonjwa.

Huko USA, sio vyakula tu vyenye sumu, hata maji yanawekwa floride.
 
Mkuu, processed food hiyo. Zimejaa chemicals na preservatives. Ndiyo maana wazungu wanaugua sana cancers.
Karibia kila kitu unachokula duniani leo kina chemicals, hakuna ushahidi wazungu wanaugua sana cancers kwa sababu ya kula processed food. Wazungu wana vinu vingi vya nyuklia, viwanda vya bidhaa karibia zote, pombe kali za kila aina, sigara, plastics kila mahali, wamechimba madini muda mrefu sana n.k hizi zote ni risks factors.
 
We unajua leo ? Mboma 90's vilikuwepo madukani. Samaki wa kufungashwa ktk kopo waliuzwa madukani baadae vikapotea au mzazi alifulia na kuacha kununua, na nyie mnaona vipya. Muwe mnauliza kwanza wahenga.
Ila ladha yake huwezi kula kama hujavizoea. Waachie wazungu wewe nenda buchani au mgahawani upate sup fresh.
Kwa nini kila cha wazungu mnakiona cha maana wakati kuna wazungu wanatamani waje Africa.
 
Back
Top Bottom