We mwl. Kuluthum Lema wa S/M Kimandafu uko juu ya waziri wa Elimu? Kwanini uwachape wanafunzi waliofika shuleni kabla ya saa moja asubuhi?

Sasa mkubwa kwa shule zetu za saint kayumba watoto ukisema waanze kufika saa mbili shule , watafagia mazingira ya shule saa ngapi , usafi madarasani , kumwagilia maua kama yapo n.k
Na masomo yataanza saa ngapi ?
Unataka masomo yaanze saa nne ?
unataka kusema kwamba tuna sheria na miongozo ambayo haitekelezeki?
 
ukifatilia sana unakuja tambua kwamba taratibu zetu za kufanya kazi hazipo sawa , yani kwenye taasisi maamuzi yanayoafikiwa yanafanyiw tathmini?
 
Stress na ugonjwa wa akili
 

Naunga mkono hoja.
 
unataka kusema kwamba tuna sheria na miongozo ambayo haitekelezeki?
Ndio , shule vipindi vinaanza saa mbili baadhi ya shule saa mbili na nusu , ukisema wanafunzi waanze kufika saa mbili kuna wengine watafika saa tatu.
Kuna ratba za usafi wa mazingira , kuna assembly wanafunzi wataingia saa ngapi darasani kuanza vipindi ?
 
Reactions: Lax
Unazijua kanuni ni miongozo ya elimu,mwalimu tu wazamu anatakiwa kufika mapema zaidi kuliko mwalimu mwingine,hapo namaanisha saa1:00 kurudi nyuma,

Je mwanafunzi yeye afike saa ngapi pi
 
nakupata na naunga mkono hoja kwamba tunataratibu nyingi sana ambazo hazitekelezeki au nyingine hata hakuna anayeweka taratibu za kutekeleza jambo fulani.

hapa jijini dar es salaam kwa sasa si jambo la ajabu sana kukutana na wanafunzi 3 asubuhi kituo cha daladala wanakwenda shule

ila swali nalotaka kujiuliza mlolongo huu wa vitu vingi ambavyo havitekelezei au vinakosa utaratibu wa kuvitekeleza wahusika wanapata ugumu gani hata wa kutambua jambo hili haliendi kama inavyokusudiwa - - - kusema kwamba hawafahamu si kweli
 
Wakati wewe unawashangaa wanao mshukia mtoa mada kuna wengine tu akushangaa wewe ulicho andika upupu mtupu wahi shuleni ili usichapwe hiyo ndo suluhu
 
Wachapwe tu watoto wa siku hizi wamekuwa legalege sana.
 
Wewe ni mjinga usiyejitambua. Unazungumzia miaka ya gizani na sasa kwamba ipo sawa?

Husikii matukio ya watoto kulawitiwa na kubakwa nyakati za alfajiri na wakati mwingine nyakati za kurejea nyumbani wakiwa wamechelewa?

Unajua watoto wengi wanatoka familia duni hivyo nyumba wanazoishi ni vichochoroni sana hadi aje atokee barabara kuu, hiyo risk hujaiona? Au kwakuwa wewe ni tasa ndiyo maana huna uchungu na watoto?
 
Nachokikumbuka saint kayumba nilizozisoma mara nyingine sikuwa mtu wa kuwahi shule,kuhusu uvaaji ndio nilikuwa nikiamua navaa hata jeans na snekers halafu na report muda wa kuanza vipindi baada ya parade na mwisho wa vipindi ndio ulikuwa mwisho wangu wa kuwepo shule…Na hii hizi desturi zilikuwa na wasomi masela wa zamani….

Saivi mtoto yai baba yai,jambo kidogo anakuja kumdhalilisha mitandaoni mtu anaye shiriki malezi ya mtoto…Mwalimu ni kama mzazi tu,mtoto inabidi wakati mwingine akosee ili kujifunza.

Isitoshe mtoto hajielewi,anachapwaje kabla ya saa moja,na ndio maana nikamuita yai.INASIKITISHA SANA.
 
Tafuta pesa uwe na maisha mazuri uache kuwalaumu walimu ambao wanakusaidia kulea mtoto wako ambaye hana akili kama bichwa lako
 
Wakati wewe unawashangaa wanao mshukia mtoa mada kuna wengine tu akushangaa wewe ulicho andika upupu mtupu wahi shuleni ili usichapwe hiyo ndo suluhu
Kwahiyo unakubaliana kila mtu avunje sheria fresh tu au?

Sheria iko wazi muda wa mtoto kufika shuleni sasa inapotokea amefika ndani ya muda wa kisheria halafu mwalimu kwa ujinga wake akataka mtoto afike mapema kinyume na sheria na kanuni, hapo anakuwa anafuata sheria ama anavunja sheria?

Hili halihitaji mwanasheria kuelewa bali akili hiyo hiyo kiduchu uliyojaaliwa unapaswa kuelewa sheria mtambuka.
 
Tafuta pesa uwe na maisha mazuri uache kuwalaumu walimu ambao wanakusaidia kulea mtoto wako ambaye hana akili kama bichwa lako
Akili kama hii yako ndiyo inayofikisha taifa kwenye kiwango duni cha uelewa.

Kwamba mtoto kuchapwa bila utaratibu ama kinyume na sheria ni sahihi tu kwa upande wako? Uvunjifu wa sheria ni sawa na uhalifu.

Malezi haimaanishi ukiukaji wa sheria bali utembee kwenye mfumo wa sheria unavyotaka.

Kila siku unasikia matukio ya watoto kuuawa kwa vipigo na walimu halafu wewe unasema ndiyo malezi ambayo walimu wanatekeleza? Ujinga unatibika wahi matibabu.
 
Umezunguka kitaalamu sana mkuu. Kuna wakati unajiuliza hivi hawa wanaoshobokea watoto kuadhibiwa vipigo kinyume na sheria wana watoto ama ni amtasa na wagumba?

Likitokea janga la mtoto kupoteza maisha kwa vipigo kutoka kwa walimu utasikia wanavyonyanyua midomo yao juu kukemea na kulaani kitendo hicho wamesahau kama wao ndiyo waungaji mkono wa ukatili dhidi ya mtoto.

Sasa kipi bora kati ya kuzuia madhara ama kutibu madhara? Adhabu yoyote ya viboko ina mwongozo very strict na walimu wanapaswa kuizingatia kikamilifu mwongozo huo.
 
Wewe khuma kweli, huko kulawitiwa kumeanza leo!au kumeanza baada ya kauli ya kisiasa ya mkenda? Tangu nchi hii inapata uhuru hakujawahi kubadilika ratiba ya kwenda shuleni leo ndio ujifanye unatoka povu!
 
Mitoto yenu ikiwa mizembe hata kufua chupi zao na kufagia hivyo vijumba vyenu lawama mnapeleka kwa walimu kuwa wamewadekeza

Acha watoto wawahi shule wakafagie na kudeki madarasa punguani wewe
Nimeona mwenzio huko LOTH HEMA nae kichwa imewaka moto, walimu mmekuaje aisee??

 
Kweli kizazi kimebadilika sana, zamani ukichapwa shuleni unapiga zako kimya maana ukisema home unaweza ukachezea kibano kingine. Ila siku hizi sisi wazazi ndio tunakuwa namba moja kutetea ujinga wa watoto wetu sijui tunalea kizazi cha namna gani.

Yan viboko viwili vitatu tu mnaripoti mpaka kwenye mitandao ya kijamii
 
Haya sasa! Ndio maana mimi sihangaiki hata afike saa 8 mchana au asipokuja kabisa. Mzazi wake si anajua aliko.
 
Huna pesa bado una kelele tena shukuru sana Waalimu wafatiliaji hao. Shule anayosoma mtt wa Waziri siyo sawa na ya mtt wako sasa usiwatipu Walimu wamfatilie mtt endelea kurusha pumb kubishana ususiwe mtt....sie Tumesoma kayumba kuwahi kulitusaidia mengi achana na mwlm kabis
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…