Well done Jakaya Kikwete

Well done Jakaya Kikwete

Jakaya Kikwete sasa hivi tunaweza kusema is a seasoned politician.

Amepitia mengi, mazuri na mabaya.

Ingawaje urais wake watu walidiriki kumwita ati dhaifu, ndani ya hii miaka mitano wananchi wameona maana ya uvumilivu wa Kikwete.

Nampongeza sana Kikwete vile vile kwa kumpigia tafu Mama Samia, dhidi ya makundi hasi, mengine yakiwa na sura ya kikabila.

Sisi wana CCM long time tunashukuru kuwa sasa chama kinarudi kwa wenye chama ambao wengine ni waasisi.

Mimi kadi yangu ni ya 1977.

Waliingizwa watu ambao wengine wametoka vyama vya upinzani na kuwaacha makada halisi.

Hongera Jakaya Mrisho Kikwete.

Nenda kapumzike kwenu Kyela ukale mbasa, umeanza mapambio ya Vasco Dagama unafikiri atakurudisha kwenye ulaji? Ulile kako!
 
Mama akiwa katikati ya JK na Magu ana nafasi ya kufanya vizuri just amuige Mwinyi Zanzibar
 
Mafisadi mnafurahisha kweli kweli
Mlikuwa mnachekelea kama hamna akili nzuri....

Watu wakitekwa na wasiojulikana......
Watu wakiibiwa fedha zao na TRA...
Watu wakibambikwa kesi za uhujumu uchumi...
Watu wakibambikwa kesi za madawa ya kulevya.......
Watu wakiuwawa halafu polisi inasema wamejinyonga.....
Watu wakinyang’anywa kampuni zao.......
Vyombo vya habari kupokwa kutoa habari (not to this extent).......
Ukabila wa vyeo..
Ukabila wa maendeleo....

Halafu bado unakenua kujiita mnyonge.
Akili kumkia wewe!
 
Nenda kapumzike kwenu Kyela ukale mbasa, umeanza mapambio ya Vasco Dagama unafikiri atakurudisha kwenye ulaji? Ulile kako!
Mkuu mimi adui wangu maonezi ya TRA, najitegemea.
Mi sio nyie mnao sukuma makalio kwenye fomu mwezi mzima ili kukinga mkono posho msizostahili.
 
Hata Magu alikuwa akikwama kwenye mambo ya uongozi alikuwa anarudi kwa JK ,Mwinyi ni mzee ,mkapa cha pombe sasa mtu pekee ni JK
 
Mlikuwa mnachekelea kama hamna akili nzuri....

Watu wakitekwa na wasiojulikana......
Watu wakiibiwa fedha zao na TRA...
Watu wakinambikwa kesi za uhujumu uchumi...
Watu wakibambikwa kesi za madawa ya kulevya.......
Watu wakiuwawa halafu polisi inasema wamejinyonga.....
Watu wakinyang’anywa kampuni zao.......
Vyombo vya habari kupokwa kutoa habaro (not to this extent.......
Ukabila wa vyeo..
Ukabila wa maendeleo....

Halafu bado unakenua kujiita mnyonge.
Akili kumkia wewe!
Ukiwa JIZI na MUUZA NGADA lazima ushughulikiwe!

Kwahiyo ulitaka wakuache?
 
  • Thanks
Reactions: ora
Mwendazake kakopa hela nyingi kuliko watangulizi wake wote waliopita unalijuwa hilo?
Hata kama alikopa kazi imeonekana ,wengine walikopa pesa ikaishia kuwanufaisha wao na familia zao, pia aliweza kukomesha yale mambo ya unanijua mimi nani au Rizi kapiga simu.
 
Jakaya Kikwete sasa hivi tunaweza kusema is a seasoned politician.

Amepitia mengi, mazuri na mabaya.

Ingawaje urais wake watu walidiriki kumwita ati dhaifu, ndani ya hii miaka mitano wananchi wameona maana ya uvumilivu wa Kikwete.

Nampongeza sana Kikwete vile vile kwa kumpigia tafu Mama Samia, dhidi ya makundi hasi, mengine yakiwa na sura ya kikabila.

Sisi wana CCM long time tunashukuru kuwa sasa chama kinarudi kwa wenye chama ambao wengine ni waasisi.

Mimi kadi yangu ni ya 1977.

Waliingizwa watu ambao wengine wametoka vyama vya upinzani na kuwaacha makada halisi.

Hongera Jakaya Mrisho Kikwete.
Vita vya panzi; sherehe ya mwewe.
 
Kikwete huyu mtu bhana , daah Mungu ampe maisha marefu Sana Sana ... Nilimchukia Sana by 2015 Ila Kwa sasa nimeona thamani yake kabisa kabisa.. sometimes huwa tunajifunza Kwa Gharama kubwa Sana
Nilikuwa kama wewe!

Mungu anisamehe kwa kosa hilo la kumchukia Kikwete kwa kutojitambua na kukosa uzoefu wa utawala mbovu!

Mungu mbariki sana Mh Kikwete. Kiongozi muungwana.
 
Ngoma droo!!

Tupo tunaoamini mpaka Leo, kikwete hawezi kabisa kuifanya nchi ikaheshimika hata kidogo, afanyeafanyavyo,amebarikiwa tu kuwa na moyo wa kupuuza mambo, lakini kuiongozi ni zero kabisa

Siwezi kusahau kipindi chake, ilikuwa ni hovyo tu, hakuna la maana, la maana ni Kwa hao waliofaidika na safari zake
Vipi wasiojulikana walikuwepo?

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom