Wengi mnatokwa povu tu ila huu ndio ukweli wa kwanini SA imeamua kutetea haki za wapalestina kwa kufungua kesi ya mauaji ya kimbari dhidi Israel

Mbona ulichoandika hakieleweki brother?
Au ni typing error?
Nilikuwa najaribu kuuliza hii vita ni kwaajili ya kutambua Nan ni taifa kati ya Israel na Palestine au ni vita Kati ya Jews na waarabu
 
Kaka vita sio kitu kizuri, je ulilaani pia Hamas waliporusha makombora mia ngapi sijui kuipiga Israel?!
Hoja yenu ya Hamas kushambulia ni mufrisi kwa sababu Israel haijaanza kuuwa wapalestina baada ya shambulizi hilo bali imekuwa ikiuwa wapalestina kwa zaidi ya miaka 75 .

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nilikuwa najaribu kuuliza hii vita ni kwaajili ya kutambua Nan ni taifa kati ya Israel na Palestine au ni vita Kati ya Jews na waarabu
Nimekuelewa brother. Hii ni vita kati ya mtawala na mtawaliwa. Mtawala anatumia mabavu, vitisho na nguvu ya dola kumkandamiza mtawaliwa.

Na mtawaliwa nae ameshachoka kutawaliwa, kukandamizwa, kutishwa, kupigwa, kufungwa na kuuwawa.

Mtawaliwa sasa anaamua kufanya jambo ambalo linamuweka hata yeye mwenyewe hatarini kwa kuvamia ngome za mtawala na yeye kuuwa kama wanavyouliwa ndugu zake ili dunia ijue mateso na machungu wanayopitia ndio yamesababisha wafanye walichofanya.

Mtawala kwa vile ana jeshi kubwa, silaha na budget ya vita anaamua kuingia vitani rasmi kupambana na watawaliwa ambao wao hawana silaha wala jeshi la kutosha la kupambana na mtawala.
 
Hoja yenu ya Hamas kushambulia ni mufrisi kwa sababu Israel haijaanza kuuwa wapalestina baada ya shambulizi hilo bali imekuwa ikiuwa wapalestina kwa zaidi ya miaka 75 .

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Umemwambia ukweli.
 
Kina KMK254 huu uzi watakuwa wanautazama kama wanavyomtazama mwendazake kwenye kutoa heshima za mwisho

Tudhihirishie uwepo wa huyo 'mungu' wenu anayesababisha mzike waafrika wenzenu wakiwa hai na kuchinja wengine.....
 

Ahaaa makombora ya tarehe 7/10 si ulifurahia hamasi walibeep sasa wanapigiwa na tena ndani ya miezi mitatu hamas itafutika kabisa hizibora atafutika kabisa
 
Maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge,hao wapalestina c ndio walianzisha vita kwa kurusha mabomu,Sasa wapambane na hali yao maana waliyataka wenyewe,halafu hao SA ni mbwa Koko tu hawana impact yoyote kwa Israeli,wakitaka na wao wajiunge na palestina wapigane na Israel,hapahapa Africa tu wanawabagua waafrica wenzao kisa wivu wa kijinga halafu wajidai wanauchungu na palestina,uwanja upo wazi na wao wanakaribishwa kwenye mapambano
 
Lakin kuna wapalestina wengi waisraeli na kabla hawa wakimbizi wa kiyahudi kurudi hapo walikuwepo wayahud wengi tu wanaishi na waarabu bila shida. Mi nadhan tatizo ni nani atambulike ndie Taifa. Maana siamin kwamba hata wapalestina leo hii wakichukua nchi kwa mfano watawatimua wayahud.
 
Ahaaa makombora ya tarehe 7/10 si ulifurahia hamasi walibeep sasa wanapigiwa na tena ndani ya miezi mitatu hamas itafutika kabisa hizibora atafutika kabisa
Hamas ni vijana wasiozidi elf 20, lakini wanapambana na nchi 3 ambazo ni Israel yenye wanajeshi zaidi ya laki 2, na hapo waliongeza na askari wengine wa akiba, Marekani ambayo imeongeza msaada wa kijeshi kwa Israel na manuari ya kijeshi ili tu kupambana na vijana wasiozidi elf 20 tena hawana ndege wala kifaru. Hapo bado sijaziweka nchi za Ulaya zikiongozwa na Uingereza.

Yani wewe, kaka zako na wajomba zako mchukue nyundo, nondo na mapanga muende katika uwanja wa mpira mkapambane na watoto wawili tu wenye umri wa miaka kumi kumi kila mmoja tena wao watumie fimbo tu kupambana na wewe. Alafu nyie bila aibu muingie mtaani kujisifu kuwa mna nguvu kwa kuwapiga watoto hao, bila kuangalia idadi yenu, umri wenu, silaha zenu na nguvu zenu.

Kisheria watoto kama hao walitakiwa wathibitiwe na watoto wenzao lakini sio familia nzima mpaka wajomba. Hamas kwa vile ni kikundi cha watu wachache na chenye silaha chache na duni. Tulitegemea jeshi lenye weledi lingekadiria nguvu za kuwadhibiti kutokana na ujuzi wao wa kijeshi. Hapengekuwa na ulazima wa kuiingiza nchi nzima vitani hadi kufikia kuwaita askari wa akiba na kuomba msaada wa kijeshi kupambana na vijana wasiokuwa hata na kifaru. Ndomaana Russia na Iran wanawacheka, kuona nchi inayojiita ina nguvu na silaha za kisasa inatumia jeshi zima na silaha zao za kisasa kudhibiti vijana wachache na bado hawajafanikiwa kuwamaliza. Wanachofanya ni kutumia jeshi na silaha kubwa kubwa kulipua makaburi, kuuwa watoto wachanga, wanawake, waandishi wa habari nk.

Hii ni aibu kwa nchi inayojiita super power. Bora hata Ukraine imeonesha uanaume wa kupambana na dubwasha Russia bila kusababisha madhara makubwa kwa kina mama na watoto wasiokuwa na hatia.
 
Umeandika ujinga, kama ubaguzi hata Israel imewafukuza waafrika kibao Rwanda ikawapokea na kuwahifadhi.

Unaposema kuwa Afrika kusini haina impact yoyote na kwamba kama inataka ijiunge na Hamas kupambana na Israel pia naona wewe hautumii kichwa kufikiri, bali unatumia...

Hivi unaojua Africa kusini vizuri kijeshi au unaongea tu kwa vile umejaaliwa kuwa myahudi uchwara wa gezaulole? Kama Israel imeomba msaada wa kijeshi na fedha kutoka Marekani ili ipambane na kikundi cha vijana wasiozidi elf ishirini wasiokuwa na kifaru au ndege ya jeshi, sasa watapoingia vitani na Afrika Kusini si ndo wataiomba na Ulaya nzima ije iwasaidie?

Vijana wanaoshindwa population hata na wakazi wa kata ya kwenu wanasababisha nchi lote liingie vitani, liongezewe msaada wa kijeshi na Marekani, litumie mivifaru na midege ya kivita kupambana na vijana wanaotumia silaha duni tena wanazotengeneza wenyewe na bado Israel hawajafanikiwa kwa lolote, alafu ndo uje useme iingia vitani na nchi yenye full jeshi, silaha bora na uwezo mkubwa wa kijeshi. Labda uniambie kama na Israel italihita jeshi la Marekani lije liwasaidie kupambana kama walivyoomba kusaidia misaada ya kijeshi, fedha na ile manuari ya kijeshi ya Marekani ili kupambana na vijana wachache.

Ila kwa Israel yenyewe haiwezi maana imeonesha udhaifu wa kutumia jeshi zima hadi askari wa akiba, midege, mivifaru nk kupambana na vijana wachache tu wenye silaha duni. Ni sawa sawa na kiongozi utumie jwtz kupambana na panya road wenye kutumia visu na mapanga alafu uje useme una jeshi bora.

Kwa vile Hamas hawazidi elfu 20 basi Israel kama ni jeshi bora na lenye weledi ilitakiwa itumie makomando kadhaa hata sawa na idadi ya hao Hamas ili kuwadhibiti, silaha zinazoendana na uwezo wa Hamas nk. Ila hapakuwa na haja ya kutumia jeshi la nchi nzima zaidi ya laki mbili, kuita askari wa akiba, mivifaru, midege nk kupambana na vijana wachache tu. Inachekesha na kufikirisha sana kwa nchi inayoojiita super power mashariki ya kati.
 
Ulichoandika ni kweli kuwa wayahudi walikuwa wanaishi vizuri tu miaka na miaka. Mziki ulikuja kubadilika baada ya waingereza na wamarekani kukusanya wazungu wenzao na kuja kuwamwaga hapo kwa kisingizio cha kuwa ni wayahudi wa Ulaya.

Ukitizama hao wayahudi wenyewe walioletwa kutoka Ulaya hawana tofauti hata kidogo na waingereza au wamarekani ambao ni wazungu. Ni kama vile wazungu waliwaleta wazungu wenzao hapo kwa lengo la kuja kusaka fursa zilizopo pale Mashariki ya kati, haswa haswa hapo Palestina ambapo kuna rasilimali kama vile petrol, gesi, maeneo ya kihistoria nk. Leo hii rasilimali hizo zipo chini ya waisrael wazungu, na ukute Marekani na Waingereza wanakuja tu kujichukulia na kupeleka kwao kutokana na mission waliotengeneza kwa hao wayahudi wa kizungu.

Wapalestina nao hawataki kufanywa wajinga kwa kupandikiziwa wazungu katika ardhi yao kwa kutumia kimvuli cha kiyahudi. Wapalestina wanawajua wayahudi wa kweli na wameishi nao miaka mingi bila shida yoyote.
 
Wewe ndio mjinga,halafu hakuna mahali nilipokwambia mm n myahudi,Sasa kama hujuwi uhusiano wa Israeli na marekani endelea kusema Israel anamtegemea mmarekani,hao south Africa hawamuwezi Israeli kwa chochote kile,na hao wapalestina waendelee kuwakumbatia Hamas ili wagawane maumivu
 
Myahudi wapo kila rangi wewe sema una bifu na wazungu. Wapo wayahud weusi wako wayahud waarabu wapo wayahud wa Iran nk. Kuwa na rangi sawa na mzungu haiondoi ukweli kuwa ni wayahud. Ishu ni kwamba hawa jamaa hiyo style wanayoingia nayo ndio style waliyoondolewa nayo huko miaka ya nyuma.
 
Yale waliyoyafanya Hamas kuua watoto wazee na wamama 1400 na kuteka watu yalikua sahihi? SA acha waendelee na wanachokifanya kwa sababu ni haki yao lkn hakina madhara yeyote katika mipango ya Israel kujilinda
 
Hamas kama ALLAH vile!!

View: https://x.com/ImtiazMadmood/status/1746229725654130991?s=20
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…