kitali
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 5,204
- 8,315
Nilikuwa najaribu kuuliza hii vita ni kwaajili ya kutambua Nan ni taifa kati ya Israel na Palestine au ni vita Kati ya Jews na waarabuMbona ulichoandika hakieleweki brother?
Au ni typing error?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilikuwa najaribu kuuliza hii vita ni kwaajili ya kutambua Nan ni taifa kati ya Israel na Palestine au ni vita Kati ya Jews na waarabuMbona ulichoandika hakieleweki brother?
Au ni typing error?
Hoja yenu ya Hamas kushambulia ni mufrisi kwa sababu Israel haijaanza kuuwa wapalestina baada ya shambulizi hilo bali imekuwa ikiuwa wapalestina kwa zaidi ya miaka 75 .Kaka vita sio kitu kizuri, je ulilaani pia Hamas waliporusha makombora mia ngapi sijui kuipiga Israel?!
Nimekuelewa brother. Hii ni vita kati ya mtawala na mtawaliwa. Mtawala anatumia mabavu, vitisho na nguvu ya dola kumkandamiza mtawaliwa.Nilikuwa najaribu kuuliza hii vita ni kwaajili ya kutambua Nan ni taifa kati ya Israel na Palestine au ni vita Kati ya Jews na waarabu
Umemwambia ukweli.Hoja yenu ya Hamas kushambulia ni mufrisi kwa sababu Israel haijaanza kuuwa wapalestina baada ya shambulizi hilo bali imekuwa ikiuwa wapalestina kwa zaidi ya miaka 75 .
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
1. Fikiria hii mbuzi meme yenye huu uzi:
Video: Mateka 250 waokolewa, HAMAS 60 wauawa na 26 kukamatwa
2. Kuwa eti inaujua ukristo kuliko Tutu.
Bure kabisa!
Ni mpumbavu pekee anaye weza kushabikia kinacho fanywa na Israel dhidi ya wapalestina.
Majitu humu yakikatiwa umeme kwa masaa 6 tu yanashinda humu yamekaza shingo na kutoa matusi kwa CCM ila wakati huo yana shangilia dhruma dhidi ya binadamu wengine.
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Lakin kuna wapalestina wengi waisraeli na kabla hawa wakimbizi wa kiyahudi kurudi hapo walikuwepo wayahud wengi tu wanaishi na waarabu bila shida. Mi nadhan tatizo ni nani atambulike ndie Taifa. Maana siamin kwamba hata wapalestina leo hii wakichukua nchi kwa mfano watawatimua wayahud.Nimekuelewa brother. Hii ni vita kati ya mtawala na mtawaliwa. Mtawala anatumia mabavu, vitisho na nguvu ya dola kumkandamiza mtawaliwa.
Na mtawaliwa nae ameshachoka kutawaliwa, kukandamizwa, kutishwa, kupigwa, kufungwa na kuuwawa.
Mtawaliwa sasa anaamua kufanya jambo ambalo linamuweka hata yeye mwenyewe hatarini kwa kuvamia ngome za mtawala na yeye kuuwa kama wanavyouliwa ndugu zake ili dunia ijue mateso na machungu wanayopitia ndio yamesababisha wafanye walichofanya.
Mtawala kwa vile ana jeshi kubwa, silaha na budget ya vita anaamua kuingia vitani rasmi kupambana na watawaliwa ambao wao hawana silaha wala jeshi la kutosha la kupambana na mtawala.
Hamas ni vijana wasiozidi elf 20, lakini wanapambana na nchi 3 ambazo ni Israel yenye wanajeshi zaidi ya laki 2, na hapo waliongeza na askari wengine wa akiba, Marekani ambayo imeongeza msaada wa kijeshi kwa Israel na manuari ya kijeshi ili tu kupambana na vijana wasiozidi elf 20 tena hawana ndege wala kifaru. Hapo bado sijaziweka nchi za Ulaya zikiongozwa na Uingereza.Ahaaa makombora ya tarehe 7/10 si ulifurahia hamasi walibeep sasa wanapigiwa na tena ndani ya miezi mitatu hamas itafutika kabisa hizibora atafutika kabisa
Umeandika ujinga, kama ubaguzi hata Israel imewafukuza waafrika kibao Rwanda ikawapokea na kuwahifadhi.Maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge,hao wapalestina c ndio walianzisha vita kwa kurusha mabomu,Sasa wapambane na hali yao maana waliyataka wenyewe,halafu hao SA ni mbwa Koko tu hawana impact yoyote kwa Israeli,wakitaka na wao wajiunge na palestina wapigane na Israel,hapahapa Africa tu wanawabagua waafrica wenzao kisa wivu wa kijinga halafu wajidai wanauchungu na palestina,uwanja upo wazi na wao wanakaribishwa kwenye mapambano
Hahaha..Good.. just check another one right there
Ulichoandika ni kweli kuwa wayahudi walikuwa wanaishi vizuri tu miaka na miaka. Mziki ulikuja kubadilika baada ya waingereza na wamarekani kukusanya wazungu wenzao na kuja kuwamwaga hapo kwa kisingizio cha kuwa ni wayahudi wa Ulaya.Lakin kuna wapalestina wengi waisraeli na kabla hawa wakimbizi wa kiyahudi kurudi hapo walikuwepo wayahud wengi tu wanaishi na waarabu bila shida. Mi nadhan tatizo ni nani atambulike ndie Taifa. Maana siamin kwamba hata wapalestina leo hii wakichukua nchi kwa mfano watawatimua wayahud.
Wewe ndio mjinga,halafu hakuna mahali nilipokwambia mm n myahudi,Sasa kama hujuwi uhusiano wa Israeli na marekani endelea kusema Israel anamtegemea mmarekani,hao south Africa hawamuwezi Israeli kwa chochote kile,na hao wapalestina waendelee kuwakumbatia Hamas ili wagawane maumivuUmeandika ujinga, kama ubaguzi hata Israel imewafukuza waafrika kibao Rwanda ikawapokea na kuwahifadhi.
Unaposema kuwa Afrika kusini haina impact yoyote na kwamba kama inataka ijiunge na Hamas kupambana na Israel pia naona wewe hautumii kichwa kufikiri, bali unatumia...
Hivi unaojua Africa kusini vizuri kijeshi au unaongea tu kwa vile umejaaliwa kuwa myahudi uchwara wa gezaulole? Kama Israel imeomba msaada wa kijeshi na fedha kutoka Marekani ili ipambane na kikundi cha vijana wasiozidi elf ishirini wasiokuwa na kifaru au ndege ya jeshi, sasa watapoingia vitani na Afrika Kusini si ndo wataiomba na Ulaya nzima ije iwasaidie?
Vijana wanaoshindwa population hata na wakazi wa kata ya kwenu wanasababisha nchi lote liingie vitani, liongezewe msaada wa kijeshi na Marekani, litumie mivifaru na midege ya kivita kupambana na vijana wanaotumia silaha duni tena wanazotengeneza wenyewe na bado Israel hawajafanikiwa kwa lolote, alafu ndo uje useme iingia vitani na nchi yenye full jeshi, silaha bora na uwezo mkubwa wa kijeshi. Labda uniambie kama na Israel italihita jeshi la Marekani lije liwasaidie kupambana kama walivyoomba kusaidia misaada ya kijeshi, fedha na ile manuari ya kijeshi ya Marekani ili kupambana na vijana wachache.
Ila kwa Israel yenyewe haiwezi maana imeonesha udhaifu wa kutumia jeshi zima hadi askari wa akiba, midege, mivifaru nk kupambana na vijana wachache tu wenye silaha duni. Ni sawa sawa na kiongozi utumie jwtz kupambana na panya road wenye kutumia visu na mapanga alafu uje useme una jeshi bora.
Kwa vile Hamas hawazidi elfu 20 basi Israel kama ni jeshi bora na lenye weledi ilitakiwa itumie makomando kadhaa hata sawa na idadi ya hao Hamas ili kuwadhibiti, silaha zinazoendana na uwezo wa Hamas nk. Ila hapakuwa na haja ya kutumia jeshi la nchi nzima zaidi ya laki mbili, kuita askari wa akiba, mivifaru, midege nk kupambana na vijana wachache tu. Inachekesha na kufikirisha sana kwa nchi inayoojiita super power mashariki ya kati.
Myahudi wapo kila rangi wewe sema una bifu na wazungu. Wapo wayahud weusi wako wayahud waarabu wapo wayahud wa Iran nk. Kuwa na rangi sawa na mzungu haiondoi ukweli kuwa ni wayahud. Ishu ni kwamba hawa jamaa hiyo style wanayoingia nayo ndio style waliyoondolewa nayo huko miaka ya nyuma.Ulichoandika ni kweli kuwa wayahudi walikuwa wanaishi vizuri tu miaka na miaka. Mziki ulikuja kubadilika baada ya waingereza na wamarekani kukusanya wazungu wenzao na kuja kuwamwaga hapo kwa kisingizio cha kuwa ni wayahudi wa Ulaya.
Ukitizama hao wayahudi wenyewe walioletwa kutoka Ulaya hawana tofauti hata kidogo na waingereza au wamarekani ambao ni wazungu. Ni kama vile wazungu waliwaleta wazungu wenzao hapo kwa lengo la kuja kusaka fursa zilizopo pale Mashariki ya kati, haswa haswa hapo Palestina ambapo kuna rasilimali kama vile petrol, gesi, maeneo ya kihistoria nk. Leo hii rasilimali hizo zipo chini ya waisrael wazungu, na ukute Marekani na Waingereza wanakuja tu kujichukulia na kupeleka kwao kutokana na mission waliotengeneza kwa hao wayahudi wa kizungu.
Wapalestina nao hawataki kufanywa wajinga kwa kupandikiziwa wazungu katika ardhi yao kwa kutumia kimvuli cha kiyahudi. Wapalestina wanawajua wayahudi wa kweli na wameishi nao miaka mingi bila shida yoyote.
Hamas kama ALLAH vile!!Ni aje waungwana,
Ndugu waungwana hapa jakwaani kwetu kuna vijana wengi ambao wamekuwa waki comment ujinga katika thread za watu wenye akili, na elimu kubwa kushinda wao, lengo ni kutaka waonekane kuwa na wao ni miongoni mwa wale wanaowatetea, hata kama hao wanaowatetewa hakuna anaewajua hata mmoja.
Ndugu waungwana hapa jukwaani kuna watu wanashangaza sana, kwa kukimbilia kuishambulia SA kutokana na kitendo chao cha kufungulia Israel kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya raia wasiokuwa na hatia, kina mama, watoto wachanga wenye umri wa chini ya miaka mitano, vilema, vizee nk.
Washambuliaji hawa wa mitandaoni haswa hapa JF ambao wengi wao wanaongozwa na kundi la wayahudi wa huko chato na nachingwea, wameshindwa kujua sababu haswa zilizopelekea nchi hiyo ya ki afrika kujiingiza katika swala hilo na ukizingatia nchi hiyo ina asilimia ndogo sana ya wavaa kobaz ambao hata hao kidogo wenyewe hawapo serikalini na wala hawana maamuzi yoyote ndani ya serikali, chama tawala wala vile vya upinzani.
Swala hili limewaunganisha wa afrika kusini wote akiwemo mwanasiasa machachari Julius Malema, tena bila kujali utofauti wa vyama vyao.
Na sababu kuu za kuichukia na kuichukulia hatua za kuishtaki kwa ukatili Inayofanya Gaza ni hizi:
1. Afrika kusini ni moja kati ya nchi ambazo zilipitia changamoto kubwa ya kutawaliwa kimabavu, kufungwa bila hatia, kuadhibiwa bila kosa, na wengine kuuwawa kwa sababu ya kudai uhuru wao, ardhi yao na haki zao. Hili walilopitia waafrika kusini ndio wanalilopitia wapalestina kwa zaidi ya miaka 70. Hivyo waafrika kusini wanajua na kufahamu machungu wanayopitia wapalestina kule kwao.
Hili swala la watu wanaojaribu kutumia nguvu kudai haki zao walizonyimwa kwa zaidi ya miaka 70 kuitwa magaidi na nchi za magharibi (Hamas) hata wao wa afrika kusini walikumbana nalo hadi kupelekea baadhi ya vijana na wanachama wa anc kukimbilia Tanzania, Zambia, Zimbabwe na kwengineko ili kukwepa mkono wa sheria wa wazungu ambao waliwaona na kuwaita wapigania uhuru na haki zao, tena katika nchi yao wenyewe kuwa ni magaidi.
2. Pili wakati wa ubaguzi wa rangi, Israel ilikuwa ni moja ya nchi ambazo zilisupport utawala wa kibaguzi wa rangi, lakini pia makaburu wengi walienda Israel kusomea mbinu za kijeshi za kuja kupambana na vijana weusi wa afrika kusini bure bila malipo yoyote kwa wayahudi.
Yaani kwa kiswahili chepesi tunaweza kusema kuwa Israel ndio ilikuwa unadhamini askari hao kwenda kujifunza ukatili katika nchi yao ili waje wauwe wenzao kwa sababu tu ya utofauti wa kirangi nk.
Unaweza ukajiuliza inakuaje nchi nyingi zifanye ukatili na Afrika kusini isiguswe wala kufuatilia ukatili huo, lakini huu wa Israel umewagusa. Na hiyo ni kwa sababu ya historia ya kile walichowanyia kupitia makaburu na kilichowatokea.
Afrika kusini ni nchi kubwa hivyo haiwezi kukurupuka tu kuanza kuichukia nchi nyingine tena ya mbali na mipaka yake bila sababu na ukizingatia nchi wanayoitetea ni ya kiarabu wakati wao sio waarabu, ni ya kiislamu wakati wao 95% sio waislamu.
Yani kwao ni bora hata baadhi ya nchi za kizungu zilionesha kuwasaidia na kuguswa na mateso waliyokuwa wanapitie enzi zile moja ya nchi hiyo ni Denmark kuliko Israel ambayo ilikuwa upande wa wazungu ili wawaangamize na kuwauwa wazawa.
Nina imani kama kungekuwa na ukaribu fulan wa kimipaka, basi wazee wa kazi wangepenyeza silaha kadhaa kwa Hamas ili kulipiza kisasi ya kile walichofanyiwa na wayahudi enzi hizo 😄😄😄
Wale wenye akili zilizojaa kichwa karibuni mjadili ki akili ili wale wasiofahamu sababu ya ufunguaji wa kesi waweze kufahamu na kujifunza. Lakini pia na wale watakaokuja kucheuwa povu lao kama mdomo wa kinda la ndege mnaruhusiwa kwa sharti la kutotukana watu hovyo.