Wengi mnatokwa povu tu ila huu ndio ukweli wa kwanini SA imeamua kutetea haki za wapalestina kwa kufungua kesi ya mauaji ya kimbari dhidi Israel

Afrika Kusini wako sahihi kuwashitaki Israel
 
Maumivu ni kwa watoto wachanga, wanawake na waandishi wa habari ambao wote hao hawana silaha na wala hawapambani na Israel.

Wale vijana elf 20 tu wameshindwa kupatikana, na wale mateka wameshindwa kuokolewa na jeshi zima la Israel likishirikiana na Marekani πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Ndiomaana nakuona haujui unachoandika. Kwanza Afrika Kusini imeshafungua kesi pindi ambapo nchi nyingine zimeshindwa kufanya hivyo (huu ni ubabe wa kwanza wa SA imeuonesha kwa Israel)

Pili imemtimua balozi wa Israel kinoma noma (hii wameionesha Israel yako dharau)

Sasa iambie Israel yako ithubutu kufanya inachoweza kufanya kwa SA kama haijapokea kipigo ambacho haikuwahi kukumbana nacho katika maisha yao. Midege na mivifaro imeshindwa kurudisha mateka waliotekwa na vijana wachache, ndo wataweza kuingia mzigoni na jeshi kubwa lenye uwezo wa hali ya juu.
 
Hilo igizo tu on a the Hague
Mivifaru, madege ya kijeshi, jeshi zima la Israel na askari wa akiba vyote kwa pamoja vimeshindwa kuwakomboa mateka walio katika mikono ya vijana wachache wanaotumia silaha duni πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Hii ni aibu. Ni sawa na jwtz, polisi na askar magereza washindwe kuwakomboa watu wanaoshikiliwa na panya road pale manzese. Hilo litakuwa jeshi tena au ni kikundi cha mgambo chenye silaha.
 
Kwani uyahudi ni race, dini au taifa?

Naomba unijibu kwanza alaf tuendelee.
 
Yale waliyoyafanya Hamas kuua watoto wazee na wamama 1400 na kuteka watu yalikua sahihi? SA acha waendelee na wanachokifanya kwa sababu ni haki yao lkn hakina madhara yeyote katika mipango ya Israel kujilinda
Wewe unahesabu yale yaliofanywa na Hamas 7 October, lakini hauhesabu zile operation zilizokuwa zinafanywa na jeshi la Israel kabla ya hiyo 7 October huko West Bank.

Walipokuwa wanaingia katika nyumba za wapalestina usiku kuwatoa watu na kuwapeleka kusikojulikana , kuwanyang'anya nyumba zao na kuzikabidhi kwa wayahudi, kuvamia kambi usiku na kuuwa vijana kwa kisingizio kuwa ni magaidi. Kwamba mtu akidai haki yake kwa mapambano hata ya kurusha mawe dhidi ya askari wanaotumia bunduki huyo raia lazima aitwe gaidi. Hii mbinu ilitumiwa sana na makaburu kuwaita vijana waliokuwa wanapigania haki zao kuwa ni magaidi. So hilo ni jambo linalojulikana.

Israel alipokuwa anaingia majumbani kuuwa watu wasiokuwa na hatia hovyo, alipokuwa anavamia kambini kuuwa watu hovyo, kutumia nguvu zilizopitiliza kwa kuruhusiwa kutumia bunduki dhidi ya raia wanaotumia jiwe na manati hilo lilikuwa sawa na ilitafsiriwa kuwa wanajilinda. Lakini hawa ambao wameuwawa, wamenyang'anywa nyumba zao, wamefungwa bila sababu walipoamua kusema sasa unyonge basi acha na sisi tujitutumie kufanya kile ambacho na wao kitawatia uchungu kama tunavyotiwa uchungu sisi kila siku, tayari kikaonekana kuwa ni kitu cha ajabu na kikatili huku ule ukatili uliokuwa unafanywa na Israel kabla ya hiyo 7 October ukiwa umefunikwa kupitia mgongo wa huu mpya wa Hamas.

Cha kushangaza jeshi zima lenye askari zaidi ya laki 2 na wengine wa akiba juu wameingia na midege yao, mivifaru na mimeli ya kivita kupambana na vijana wasiozidi elf 20 tena wenye silaha duni, na mpaka leo wameishia kutumia midege na mivifaru hiyo kuuwa raia tu bila kuokoa mateka wanaoshikiliwa.
 
Detail ya kiwango cha elimu inaonekana kupitia comments ya mtu.
Sidhani kuwa kuna mtu mwenye elimu anaweza kuandika ujinga, kwa sababu ujinga mara zote huandikikwa na wajinga.
 
Detail ya kiwango cha elimu inaonekana kupitia comments ya mtu.
Sidhani kuwa mtu mwenye elimu anaweza kuandika ujinga, kwa sababu ujinga mara zote huandikikwa na wajinga.
Mimi tena Mkuu?
Myahudi wa Mbagala huyo, ashavurugwa na vita alafu mateka hajawapa πŸ˜„πŸ˜„
 
Kwani uyahudi ni race, dini au taifa?

Naomba unijibu kwanza alaf tuendelee.
Jews ni jamii iliyochanganyika na race zote. Dini ya yao wanaita Judaism na Taifa ni Israel. Sasa hawa Jews wapo ambao sio waisraeli kuna raia wa Morocco Yemen Iran Iraq Jordan jews na Ethiopia. Hawa walioko Israel wengi ni wale waliorud baada ya mateso huko walipokuwa hasa ulaya kwa miaka mingi ya utawanyiko wao. Japo wapo wale waliokuwepo hapo muda wote mpaka Wakat wa anguko la ottoman empire.
 
Wewe ndio hujuwi unachoongea,hao Hamas wanapigana kwa kujificha kwa raia, Israeli ingetaka kupiga mtu yeyote bila kuangalia raia wapalestina wangeisha,halafu hiyo SA haimuwezi Israeli kuanzia uchumi mpaka technology,hao waarabu wanaomzunguka Israeli kwa pamoja walichezea kichapo ndani ya siku sita,SA anatafuta kiki,hamuwezi Israel kwa chochote kile,na kadiri muda unavyozidi kwenda utathibitisha mwenyewe nan anaumia pakubwa kati ya hao wapalestina na Israel
 
SA ina wanasheria bora sana hiyo kesi watawakimbiza mno Israel wapo Ma Prof wawili ni wazuri sana kwa hizi kesi ngoja tusubiri muda utaongea zaidi..
 
Jews ni jamii iliyochanganyika na race zote.
Hapa nakubaliana na wewe mkuu
Dini ya yao wanaita Judaism na Taifa ni Israel.
Kwa vile Jews ni mchanganyiko wa race kutoka mataifa yote, basi ulitakiwa useme kuwa dini au imani hiyo ya Jews ilianzishwa nchini Israel na sio kwamba wote taifa ni Israel, maana hiyo ni dini kama ilivyo Ukristo na Uislam. Mfano Tanzania kuna wakristo wa dhehebu la Roma, lakini utaifa wao ni watanzania na sio waroma au waisrael ambapo inasemekana imani hiyo ya Kikristo ndipo ilipoanzia.

Vilevile hauwezi kuwapa waislam wa Tanzania au Kenya kuna utaifa wa Saudi Arabia kisa dini wanayoamini imeanzishwa nchini huko.

Hivyo unavyosema kuwa Jews au wayahudi taifa la ni Israel unakosea maana ushakiri mwenyewe kuwa kuna ambao sio waisrael, umesema kuna waithiopia, wamisri nk.
Sasa hawa Jews wapo ambao sio waisraeli kuna raia wa Morocco Yemen Iran Iraq Jordan jews na Ethiopia.
Hii ndo nimejibu hapo juu
Hawa walioko Israel wengi ni wale waliorud baada ya mateso huko walipokuwa hasa ulaya kwa miaka mingi ya utawanyiko wao.
Kwa vile umejibu vizuri swali langu kuwa wayahudi wapo wa race tofauti basi haina haja ya kubisha kuwa kina Netanyahu wanaweza kuwa wayahudi wenye asili ya kizungu. Kama wazungu haswa waingereza waliweza kwenda Marekani kusaka rasilimali za huko America kwa njia walizozijua wao, wakatawala na baadae kupigana wenyewe kwa wenyewe na kupelekea baadhi yao kuanzisha taifa la Marekani, kama wazungu waingereza waliweza kwenda kusaka rasilimali Canada, New Zealand, Australia, South Africa, Zimbabwe, Kenya, Ghana, Nigeria wakaingia katika hizo nchi kwa njia wanazozijua wao, wakatawala na wengine kubaki na kutengeneza mataifa kama New Zealand, Canada nk, je wanaweza kushindwa kuingia Israel kupitia mgongo wa wayahudi na kufanya nchi yao?

Kwa vile ni vigumu kupima DNA ni nani anaeweza kuthibitisha kuwa mtu aina ya Netanyahu ni myahudi wa asili ya Israel? Dunia ya leo haswa kwa wenzetu wazungu ambao wako tayari kufanya lolote au chochote kwa masilahi ya nchi zao usishangae kina Netanyahu wakatengenezwa toka wakiwa shuleni ili waje wajifanye wayahudi kwa malengo maalumu ya wanaomtuma.
Japo wapo wale waliokuwepo hapo muda wote mpaka Wakat wa anguko la ottoman empire.
Katika msafara wa mamba kenge nao wapo. Ukute ile mission iliyoongozwa na UK kuwarudisha waisrael nchini hapo ndio imetumiwa njia ya kupenyeza watu wao kwa sababu ya masilahi yao.
 
Hadithi hadithi hadithi njoo utam kolea πŸ˜‚πŸ˜‚ unajua SA inashinda nchi ngapi za Ulaya uchumi. Alafu SA ndio inategemewa rasilimali zake na Ulaya ndiomaana wazungu walikataa kuondoka.

Israel mpaka leo bado inategemea msaada wa kijeshi na fedha za kujikimu kutoka Marekani, UK na Ujerumani, wao binafsi hawana uwezo wa kujiendesha, kujilinda wala kujisimamia hili hata wewe mwenyewe rohoni kwako unalijua, sema ndo vile umeamua na wewe ujitutumue ili uonekane haushindwi.

Hayo unayosema wewe ni maelezo tu ya kusimuliwa ambayo hakuna mtu aliyashuhudia. Lakini haya yanayoendelea leo ni ya dhahiri kila mtu anaona, anasikia au kusoma kupitia simu yake. Kwa vile media na utandawazi wa mitandao haukuwepo wajinga wakawa wamejaribu kutulisha matango pori sijui operation Entebbe huko Uganda. Wajinga wengi walimezeshwa uongo ule. Sasa leo watu wanataka kuona hao makomandoo walioenda kuokoa watu Uganda wawaokoe hao ndugu zao ambao wapo hapo hapo karibu yao, lakini wapi tunakwenda mwezi wa NNE huu hakuna hata dalili ya makomandoo na jeshi lao lenye askari mpaka wa akiba, mivifaru, midege, mimeli ya kijeshi vyote vinauwa watoto wachanga tu wasiokuwa na uwezo wa kurusha hata jiwe.

Tunashukuru Mungu media na mitandao ya miaka hii imetusaidia kuuona ukweli na uongo wa makomandoo uchwara. Kusadiki kwa toma ni kujionea, sio zile porojo za kuadisiwa ambazo nyingi hazina ukweli.

Vijana elf 20 tu wanalichachafya taifa zima na vibaraka wao.
 
SA ina wanasheria bora sana hiyo kesi watawakimbiza mno Israel wapo Ma Prof wawili ni wazuri sana kwa hizi kesi ngoja tusubiri muda utaongea zaidi..
SA inajiamini katika hili, na wanajua wanachokifanya. Lazima Israel waombe poo
 
Endelea kujifariji,hivi aliyeomba vita isimamishwe kwa muda apewe msaada wa vyakula na huduma nyingine za kijamii ni nani? Ni raia wa upande upi wamekufa zaidi? Ni nani ambae amepoteza eneo lake?
 
Endelea kujifariji,hivi aliyeomba vita isimamishwe kwa muda apewe msaada wa vyakula na huduma nyingine za kijamii ni nani? Ni raia wa upande upi wamekufa zaidi? Ni nani ambae amepoteza eneo lake?
Kwahiyo wewe ubora wa vita unaupima kwa kuuwa raia. Yani wanaouwa raia wengi kwa midege, mivifaru na mimeli ndio mabingwa wako hata kama wameshindwa kuwaokoa mateka wao waliotekwa na vijana elf 20 tu πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„

Nina wasi wasi na umri wako, huenda najadiliana na mtu alieiba simu ya shemej yake au baba yake ili aje aitetee Israel.

Acha nikuache ulale kabla shemej yako hajarudi akakukuta unachezea simu yake. Siku ukikua ukinunua simu yako na kuanza kufuatilia haya mambo kwa kutulia nina imani utajifunza mengi.
 
Kwahiyo wewe ubora wa vita unaupima kwa kuuwa raia. Yani wanaouwa raia wengi kwa midege, mivifaru na mimeli ndio mabingwa wako hata kama wameshindwa kuwaokoa mateka wao waliotekwa na vijana elf 20

Endelea kuwa na huo wasiwasi,unafaham maana ya vita? Unafaham kwanini Hamas wanavizia yani wanajificha kwa raia na hawawaface Idf direct? Usianze kukwepa mada mara oh sijuwi umri wako,mara unakaa kwa shemeji yako,mkuu acha ramri na tabia za kike,tubishane kwa hoja,hunifaham Wala sikufaham ila tuheshimiane
 
Upuuzi mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…