Wengi wanaotaka wake zao wasifanye kazi wana upeo mdogo wa kufikiri halafu ni wabinafsi

Hakuna sehemu yotote kwenye biblia wala kwenye qu'ran mwanamke analisha Familia.

Matajiri woote hadi leo hakuna Mke wake anafanya biashara za Upatu.

Ni umaskini wetu tu.

Mwanamke ni Mfalme wa familia na watoto.

Waarabu na wahindi wametuzidi hapa.
 
Kwani akifanya kazi hawezi kuwa pambo au kumburudisha mumewe?

Kuna wanawake wanaofanya kazi na bado ni warembo kuliko wanaokalizwa nyumbani.
Hoja yako haina mashiko
We naona hujui hata kazi zenyewe......awe polisi kila siku lindoz akirudi kachoka balaa.

Bado unataka awe pambo? We utakuwa ni mnyanyasaji wa wanawake sio bure.
 
Mdogo wangu Robert,, umeowa? Kweli,,, oa kwaza utatuletea mlejesho..
 
Mkuu mimi mke wangu nilimruhusu afanye kazi ila saa kumi na mbili jioni awe home kunipikia (maana anajua kabisa chakula cha jioni anatakiwa apike yeye na sio dada wa kazi)

Siku akaniletea pigo zake kuniambia Boss alimsubirisha

Nikamuuliza, "Huyo Boss wako anakulipa sh ngapi kwa mwezi?"
Aliponijibu nikamwambia haya kuanzia sasa hakuna kwenda kazini maana pesa ninayompa mimi kwa ajili ya kutumia kazini ni nyingi mara mbili ya mshahara wake

Yaani alipwe mshahara wa miezi miwili ndo afike pesa ninayompa kwa ajili ya matumizi yake

Sasa nikamwambia akae Nyumbani huo mshahara anaolipwa huko nitakuwa namlipa mimi
 
Wanawake wa sasa bila kuwa na mfumo dume hutoboi

Wapo wa kuishi nao hivyo unavyotaka wewe ila sio hawa wa Haki Sawa
 
Ni mtihani sana.
 
Sasa kwamsimamo wako huo sio vibaya. Ila elewa hakuna mwenye maagano na Muumba. Ikitokea mume akaumaliza mwendo akaacha watoto unadhani ninani ayawalea ikiwa mama hana a,b,c juu ya kujishuhulisha?
Watu wafanye kazi. Tasiige mabilionea kupumzisha wake zao nyumbani wakati maskini hata mkewe ameshindwa kumuwekea house girl
 
Mleta mada ameandika kwahasira inaonekana jambo hilo limemgusa mojakwamoja ndani mwake. Anazohoja nzuri lakini uwasilishaji wake umekosa utulivu
 
Hapa mkuu naona umetaka tu kujifurahisha na kujipa matumaini kwa uongo.
matumaini yapi mfungie mkeo aliwe kwa kuona hana kazi ya kufanya na anataka pesa... ataliwa hadi na waokota makopo....
 
Tafuta pesa, imeandikwa mwanaume atakula kwa jasho, mwanamke atazaa kwa uchungu
 
Mwanamke akifanya kazi pesa yake itakuwa inafanya nini ?
 
Mwanamke asaidiane na mumewe au sio ?😀

Yaani wanawake hawa wasaidiane na mume zao au wanawake wengine una wazungumzia ?😀
 
Umegenerize sana, wanawake wapo wa type nyingi ni kama kuku, wapo kuku mzinga kwajil ya pambo wapo kuku wa nyama na wapo kuku wa mayai.

Ukitaka mwanamke wa kukaa ndani wapo wengi tu kwa wadigo ukitaka mpambanaji wasio bagua kazi nenda kwa waha uko, ukitaka wenye kazi nenda migodini mara uko. Na wote unaweza kuishi nao kwa raha inategemea na wewe unataka nini. Kupanga nikuchagua hayana muongozo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…