Wengine hatuwezi ku-date na Mwanamke asiyeweza kujilipia nauli na kujinunulia vocha

Wengine hatuwezi ku-date na Mwanamke asiyeweza kujilipia nauli na kujinunulia vocha

Mwanamke AKUPENDE? Seriously?

Wakosai 3:18-19
Enyi wake,watiini waume zenu,kwani ndivyo APENDAVYO Bwana.Nanyi waume wapendeni wake zenu msiwe wakali kwao

Waefeso 5:25
Ninyi waume WAPENDENI wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa akajitoa nafasi yake Kwa ajili yake.

Hayo mambo ya sisi kupenda wanaume hatujaagizwa,,,tumeagizwa kuwatii waume zetu.na tutakutii ikiwa Utawajibika.

Paul hawezi kuwa reference nzuri kwenye mambo ya sheria. Tena sheria za mahusiano.
Paulo ni kama Yesu, ishu za mahusiano ya kindoa hatuwezi kumtumia MTU ambaye hana uzoefu wa mahusiano. Na ambaye hajawahi kuingia kwenye ndoa.

Hapo labda uwataje kina Ibrahim, Yakobo, Daudi, Suleiman na wote waliokuwa na familia.

Lakini kina Daniel, Isaya, Yesu, Paulo na wa mfano huo hawawezi kuwa role model wa mambo hayo.
 
Mwanamke hakuombi hata hela ya kununua Peruvian Hair, sembuse ya kwenda kusafisha Kucha Saluni.

Unadate na Mwanamke ambaye hakuombi Vocha si atafanya akili yako ilale, Mwanamke lazima akuombe vi elfu 50, 50 ili akufanye utie bidii kutafuta hela
🤣🤣🤣
 
Unachotaka kuongea hapa ni tofauti na ulichoongea mwanzo.
Imebidi nitumie lugha hii rahisi kuweza kueleweka.

Mwanamke anapokuomba hizo elfu 50, 50 ndiyo chachu yenyewe kufanikiwa.

Wanasema kadri unavyotoa ndivyo zinavyozidi kupata 🤗
 
Upendo una gharama both side! Kama one side haigharamikii basi hamna upendo. Kama unashindwa vidogo vidogo kama Vocha au Nauli nini utagharamia kwenye relationship. Huyo kupe hafai.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Paul hawezi kuwa reference nzuri kwenye mambo ya sheria. Tena sheria za mahusiano.
Paulo ni kama Yesu, ishu za mahusiano ya kindoa hatuwezi kumtumia MTU ambaye hana uzoefu wa mahusiano. Na ambaye hajawahi kuingia kwenye ndoa.

Hapo labda uwataje kina Ibrahim, Yakobo, Daudi, Suleiman na wote waliokuwa na familia.

Lakini kina Daniel, Isaya, Yesu, Paulo na wa mfano huo hawawezi kuwa role model wa mambo hayo.
Hicho kibali Cha kuanza kupingana na Biblia umekitoa wapi??

Anyways,hata tukiwaangalia hao uliowataja kama reference
Suleiman,Kuna Muongaji kama huyu tangu kuumbwa Kwa ulimwengu?fuatilia chanzo Cha "The hanging garden ya Babylon ndio utajua hujui

Daudi,huyo kama hujui ndio kiboko mwingine,kama unabisha muulize mke wa Uria akupe Stori

Ibrahim,Hakuna mwanamke alikuwa anadekezwa kama Sarah kama hujui huyu hata vyombo alikuwa haoshi,kila kitu analetewa na Ibu,kazi anafanya Hajir,

Tena hao uliowatoa mfano wanahonga Vito vya thamani,dhahabu,rubi,lulu sio nyie wa siku hizi hata vocha mnashindwa nunua Pete ya silver mtaweza?
 
Hivi haya mambo si yanatokana na mgawanyo wa majukumu jamani au, labda siku kazi za nyumbani (kupika, vyombo, kufua, usafi, kulea mume na watoto) zikiacha kuonekana ni za kike tu na mtu yeyote kuweza kuzifanya wakati wowote ule, basi nahisi hata jukumu la kutafuta pesa litaacha kuonekana ni la mwanaume tu

Halafu ninyi si ndio mnakataa haki sawa sasa mbona mnapigania majukumu sawa, tena mnataka ikibidi mwanamke afanye mengi zaidi, ila likija kwenye suala la haki sawa mnaruka futi elfu

Yani lazima tukubaliane kama tunapinga haki sawa kwamba mwanaume ndio ana haki zaidi kuliko mwanamke, basi tupinge na majukumu sawa kwamba mwanaume ndio awe na majukumu zaidi kuliko mwanamke, lazima mkubali kwamba with great power comes great responsibility sasa wanaume wa kiafrika wanaitaka hiyo power tu ila responsibility hawataki
 
Mkuu unaonaje ukigombea nafasi ya mwenyekiti wa UWABATA( Umoja wa Wanaume Bahili Tanzania)?
 
Hicho kibali Cha kuanza kupingana na Biblia umekitoa wapi??

Anyways,hata tukiwaangalia hao uliowataja kama reference
Suleiman,Kuna Muongaji kama huyu tangu kuumbwa Kwa ulimwengu?fuatilia chanzo Cha "The hanging garden ya Babylon ndio utajua hujui

Daudi,huyo kama hujui ndio kiboko mwingine,kama unabisha muulize mke wa Uria akuoe Stori

Ibrahim,Hakuna mwanamke alikuwa anadekezwa kama Sarah kama hujui huyu hata vyombo alikuwa haoshi,kila kitu analetewa na Ibu,kazi anafanya Hajir,
Tena hao uliowatoa mfano wanahonga Vito vya thamani,dhahabu,rubi,lulu sio nyie wa siku hizi hata vocha mnashindwa nunua Pete ya silver mtaweza?

Sijapingana na Biblia Ila naeleza habari za Biblia kama zilivyo.
Huwezi muuliza Yesu habari za vita au mahusiano ya mapenzi Wakati Hana ujuzi wala uzoefu nayo.

Huyo Paulo Hana ajualo kwenye ishu za mahusiano ndio maana nikasema hao hawawezi kutoa ushauri wa maana kwenye masuala ya Mahusiano ya mapenzi.

Hao Wanawake waliodekezwa na kupewa mapenzi nao walionyesha ushirikiano wa kutosha Kwa Waume zao.
Kuanzia Sarah Kwa Ibrahim,
Abigael Kwa Daudi,

Wanawake wote wenye majina makubwa kwenye Biblia hawakuwa Materialist au wanyonyaji au makupe.
 
Back
Top Bottom