Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
- Thread starter
- #21
Jukumu la kulea familia ni la mwanaume tangu mwanzo , labda kulea demu sjui mpenzi sjui mchumba Hilo ndo tatizo , Ila kulea familia ni jukumu la mwanaume na ndo aliyepewa akili na uwezo wa kuyakabili mazingira magumu kuwa fursa...ukitaka mke afanye hyo kazi Mzee ataishia kugawa mbunye tuu , hawanaga huo uwezo hata kidog
Hizo ni kauli za jamii Maskini.
Kulea familia ni jukumu la Baba na Mama.
Wote lazima mfanye kazi, mtunze Familia yenu Kwa kushirikiana.
Kujigeuza msukule Kwa wanaume wengi ndio kunawafanya wawaone Wanawake ni wabaya kumbe wao ndio wapumbavu.
Kasome;
Mithali 31:
10Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?
Maana thamani yake yapita thamani ya marijani.
11Moyo wa mumewe humwamini,
Wala hatakosa kupata mapato.
12Humtendea mema wala si mabaya,
Siku zote za maisha yake.
13Hutafuta sufu na kitani;
Hufanya kazi yake kwa moyo wote.
14Afanana na merikebu za biashara;
Huleta chakula chake kutoka mbali.
15 Tena huamka, kabla usiku haujaisha;
Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula;
Na wajakazi wake sehemu zao.
16Huangalia shamba, akalinunua;
Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
17Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi;
Hutia mikono yake nguvu.
18Huona kama bidhaa yake ina faida;
Taa yake haizimiki usiku.
19Hutia mikono yake katika kusokota;
Na mikono yake huishika pia.
20Huwakunjulia maskini mikono yake;
Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
21Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake;
Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
22Hujifanyia mazulia ya urembo;
Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
23 Mume wake hujulikana malangoni;
Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
24Hufanya nguo za kitani na kuziuza;
Huwapa wafanya biashara mishipi.
25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake;
Anaucheka wakati ujao.
26Hufumbua kinywa chake kwa hekima,
Na sheria ya wema iko katika ulimi wake.
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake;
Wala hali chakula cha uvivu.
28 Wanawe huondoka na kumwita heri;
Mumewe naye humsifu, na kusema,
29Binti za watu wengi wamefanya mema,
Lakini wewe umewapita wote.
Huyo ndio MKE sasa. Unaoa MKE na sio mdoli