Wengine hatuwezi ku-date na Mwanamke asiyeweza kujilipia nauli na kujinunulia vocha


Hizo ni kauli za jamii Maskini.
Kulea familia ni jukumu la Baba na Mama.
Wote lazima mfanye kazi, mtunze Familia yenu Kwa kushirikiana.
Kujigeuza msukule Kwa wanaume wengi ndio kunawafanya wawaone Wanawake ni wabaya kumbe wao ndio wapumbavu.
Kasome;

Mithali 31:
10Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?
Maana thamani yake yapita thamani ya marijani.
11Moyo wa mumewe humwamini,
Wala hatakosa kupata mapato.
12Humtendea mema wala si mabaya,
Siku zote za maisha yake.
13Hutafuta sufu na kitani;
Hufanya kazi yake kwa moyo wote.
14Afanana na merikebu za biashara;
Huleta chakula chake kutoka mbali.
15 Tena huamka, kabla usiku haujaisha;
Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula;
Na wajakazi wake sehemu zao.
16Huangalia shamba, akalinunua;
Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
17Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi;
Hutia mikono yake nguvu.
18Huona kama bidhaa yake ina faida;
Taa yake haizimiki usiku.
19Hutia mikono yake katika kusokota;
Na mikono yake huishika pia.
20Huwakunjulia maskini mikono yake;
Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
21Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake;
Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
22Hujifanyia mazulia ya urembo;
Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
23 Mume wake hujulikana malangoni;
Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
24Hufanya nguo za kitani na kuziuza;
Huwapa wafanya biashara mishipi.
25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake;
Anaucheka wakati ujao.
26Hufumbua kinywa chake kwa hekima,
Na sheria ya wema iko katika ulimi wake.
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake;
Wala hali chakula cha uvivu.
28 Wanawe huondoka na kumwita heri;
Mumewe naye humsifu, na kusema,
29Binti za watu wengi wamefanya mema,
Lakini wewe umewapita wote.

Huyo ndio MKE sasa. Unaoa MKE na sio mdoli
 
Mke ni msaidizi sio main performer ...
 
Mke ni msaidizi sio main performer ...

Na hicho ndicho nilichoandika.
Kama Mwanamke anakosa nauli na vocha huyo tafsiri yake Hana Sifa za hiyo mithali 31. Yaani sio MKE mwema na Bora.
Kwamba anashindwa kujishughulisha Kwa vitu vidogo vidogo ajihudumie mahitaji yake.
Hivi huyo ukimuoa si atakugeuza msukule wake.
 


"ushasema mwanamke Mbinafsi" - Ulichaguliwa?
 
Wanakuja PM
 
Umepiga kwenye mshono masta yani mi dem wa namna hiyo hata wiki haipiti yani una kaa na dem ana waza kukupiga mzinga tu .... mbezi Beach na mwenge ni karibu lakini anakuomba pesa ya nauli pumbavu kabisa ...... kwanza wana niksi
 
Imategemea unadate na mtu wa aina gani.

Mabinti wengi na actually vijana wengi ni jobless, hawana vipato. Ukimpata binti wa hivi huna budi kumsaidia, tena msaidie sana kila unapoweza kwa sababu ukweli ni kuwa wengi sana wana elimu zao lakini bahati mbaya sana wapo tu home hawana shughuli za kufanya.

Kama unadate mfanyakazi au mjasiriamali, kweli nauli ya uber, boda au daladala ni jukumu lake. Kama hata nauli anaona ubahili kujilipia, basi tena.

Ukiwa na mke ni hadithi nyingine kabisa...
 
hela haziokotwi nyie sio wastaarabu kila saa mizinga

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kuna mteja wa kiume kaingia dukani hapa kasuka yebo yebo za rasta, nimechekaaaaaa ananiuliza unacheka nini?kanitolea macho ikabidi nimjibu kuna mtu kwenye simu ananichekesha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tatizo wao hawatupendi wanatutumia.
 
"ushasema mwanamke Mbinafsi" - Ulichaguliwa?

Kimsingi sijawahi date na Mwanamke mbinafsi.

Unajua wanaume wengi wanakufa mapema Kwa sababu gani?
Unajua wanaume wengi hasa Vijana wanateswa na Wanawake,
Ndio maana ninawasanua Vijana wadogo ambao hawajaingia kwenye Ndoa ili wale Maisha kama Mimi Kaka yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…