Wenye familia na watoto mnawezaje kutazama Runinga nyumbani?

Wenye familia na watoto mnawezaje kutazama Runinga nyumbani?

Nikishakubali matokeo kuwa kwangu Tv ya sebuleni sio mali yangu.

Nashukuru Mungu niliweka TV chumbani. Ninachotaka kuangalia nakiangalia chumbani kwangu. Huko sebuleni ni Nickelodeon na Cartoon Network.

Ningeweza kutumia ubabe wa ubaba lakini sioni faida yake. Ikiwa nipo hai acha wanangu wa enjoy nyumbani kwa baba yao.
Watoto TV mwisho saa Tano asubuhi,unafugaje mitoto inalelewa na TV kutwa?
 
Eti?

Unarudi nyumbani unakuta watoto wanatazama katuni zao kwa raha zao, au tamthilia pendwa za kike..... unawezaje kubadili chaneli bila kuonekana katili?

Tuseme muda wa Taarifa ya Habari, au hata mechi pendwa za soka..... ukibadili channeli watoto hao wanakukimbia sebuleni unabaki mwenyewe.

Hujisikii vibaya?

Hapa ndo umuhimu wa kupitia maeneo fulani kabla ya kurudi nyumbani, wenzetu mnawezaje?
Pongezi ziende kwa mke wangu kwa kulea wstoto kwa nidhamu ya hali ya juu, the moment nikiingia sebuleni na kukaa wanangu wananiletea renote haraka yule mdogo ananiwashia ch 406 au 224 225 dstv na wanaondoka zao kucheza ps.
 
Ukiwa dingi wa kiafrika unatakiwa uweke chanel ambayo nyumba nzima hawapendi alafu we mwenyewe huangalii unasinzia ila wakibadilisha tu chanel unashtuka usingizi unaisha alafu unawaambia rudisha haraka.
Eeeh hizi ndo zile mshua wamemletea kelele job anatafuta pa kuzimalizia mbaya zaidi iwe kipindi kama hiki mmetoka kumaliza mitihani ukitest ukalale ndo unaitwa we leta matokeo.

Kikubwa mtu ajichanganye tu na hizi ilikuwa sana ma faza wa kitambo huko.
 
Kama mimi ndo mtoto huwa najiskia vibaya sana..
Mfano father yeye akija tuu
""Weka TV iman hapo mnaangalia angalia miziki ndo mnajifunza nini ""

Mda huo mtakaa ndani kimya
Hii tabia naiona sana hata hapa kwa shemeji mume wa dada. Yaani ananikuta naangalia tv yeye anasema tutoe aangalie mahabari.

nanyanyasika sana hapa. Nataka nimuombe dada simu nimwambie mama
 
Kama mimi ndo mtoto huwa najiskia vibaya sana..
Mfano father yeye akija tuu
""Weka TV iman hapo mnaangalia angalia miziki ndo mnajifunza nini ""

Mda huo mtakaa ndani kimya
Hii tabia naiona sana hapa kwa shemeji mume wa dada. Yaani ananikuta naangalia tv yeye anasema tutoe aangalie mahabari.

nanyanyasika sana hapa. Nataka nimuombe dada simu nimwambie mama
 
Back
Top Bottom