Wenye familia na watoto mnawezaje kutazama Runinga nyumbani?

Wenye familia na watoto mnawezaje kutazama Runinga nyumbani?

Watoto TV mwisho saa Tano asubuhi,unafugaje mitoto inalelewa na TV kutwa?
Nahisi tofauti yetu mimi na wewe ni kuwa wewe una mitoto kama ulivyoandika. Mimi nina watoto.

Sijui umetumia kigezo gani kuamini wanangu wanalelewa na TV kupitia comment yangu moja tu. Sitohoji hilo maana ni bundle lako, simu yako na fikra zako umetumia kuandika ulichoandika.

Hakuna formula ya kulea mtoto
Iliyoainisha kuwa Tv mwisho saa 5 asubuhi. Inawezekana ni sheria yako, hai apply kwa kila mtu.

Comment ilijibiwa kwa ujumla, ukitaka mmeng'enyo wa muda hasa wa saa ngapi mpaka saa ngapi wanaangalia tv, basi nitafurahi kukuelezea.

Maisha yanatofautiana chief, usiishi kwa kukariri.
 
Eti?

Unarudi nyumbani unakuta watoto wanatazama katuni zao kwa raha zao, au tamthilia pendwa za kike..... unawezaje kubadili chaneli bila kuonekana katili?

Tuseme muda wa Taarifa ya Habari, au hata mechi pendwa za soka..... ukibadili channeli watoto hao wanakukimbia sebuleni unabaki mwenyewe.

Hujisikii vibaya?

Hapa ndo umuhimu wa kupitia maeneo fulani kabla ya kurudi nyumbani, wenzetu mnawezaje?
Nyumba standard inatakiwa si tu kuwa na TV zaidi ya moja, bali hata sebule zinatakiwa kuwa zaidi ya moja. Kuruhusu watoto wakae sebule yao wakaangalia vitu vyao, na wakubwa wakakaa sebule yao wanaangalia vitu vyao.

Halafu hizo TV inatakiwa kila chumba kiweze kuwa na TV yake.

Yani ikibidi mpaka jikoni mtu akitaka kupika huku anaangalia vipindi vya mapishi aweze kuwa na ki TV cha kiushkaji cha jikoni.
 
Hii tabia naiona sana hapa kwa shemeji mume wa dada. Yaani ananikuta naangalia tv yeye anasema tutoe aangalie mahabari.

nanyanyasika sana hapa. Nataka nimuombe dada simu nimwambie mama
"""nanyanyasika sana hapa. Nataka nimuombe dada simu nimwambie mama"""
Nusu nipaliwe na uji 😂😂😂😂😂
 
Mkuu umemaliza kila kitu. Demokrasia ndio inafanya mpaka tupate mashoga na wasagaji.

Acheni ukiritimba na ubeberu ☹️ lazima uwe fair kwa watoto wako ukiwa fear nao watafurahia na watakubaliana na wewe kuangalia unachotaka muhimu ni kutumia kauli nzuri kwa watoto wako watawale kisaikolojia sio kwa ubabe
 
Eti?

Unarudi nyumbani unakuta watoto wanatazama katuni zao kwa raha zao, au tamthilia pendwa za kike..... unawezaje kubadili chaneli bila kuonekana katili?

Tuseme muda wa Taarifa ya Habari, au hata mechi pendwa za soka..... ukibadili channeli watoto hao wanakukimbia sebuleni unabaki mwenyewe.

Hujisikii vibaya?

Hapa ndo umuhimu wa kupitia maeneo fulani kabla ya kurudi nyumbani, wenzetu mnawezaje?
Saiv watu wanajenga nyumba wanaweka sebule mbili moja ya watoto na watu wazima ila kama uchumi wako thwaifu unajenga chumba kimoja kikubwa unaeka mlango mpan iyo itaitwa multipurpose room
 
Saiv watu wanajenga nyumba wanaweka sebule mbili moja ya watoto na watu wazima ila kama uchumi wako thwaifu unajenga chumba kimoja kikubwa unaeka mlango mpan iyo itaitwa multipurpose room
TV siyo ya kuwaachia watoto,nakumbuka miaka ya 90 mwanzoni tukitizama wazungu videoni wakinyonyana ndimi tuliona uchafu,lakini Leo kila mtu analilia denda,mavazi ya mabinti leo tv Zina ushawishi mkubwa,namna tunavyojamiiana Leo ni matokeo ya tv,tv ni shule ovu isiyo rasmi,usiiache iwe mwalimu wa wanao
 
Kama mimi ndo mtoto huwa najiskia vibaya sana..
Mfano father yeye akija tuu
""Weka TV iman hapo mnaangalia angalia miziki ndo mnajifunza nini ""

Mda huo mtakaa ndani kimya
Hawa ni wababa wa enzi za ukoloni. Ni washamba na wanavaa MAYENU.

Kwanini usiwaache watoto wakaangalia katuni zao wewe uende chumbani ukasali hata rozari?

Watoto hawana raha, libaba linabadilisha tu chaneli! Khaaa!!!

Hili nalo mkalitazame!

cc Lamomy cocastic fundi bishoo Extrovert
 
Mimi ilikuwa ikifika saambili usiku namwachia Mama rimoti ili apitie ITV

Personally nyumabani taarifa ya habari ilikuwa lazima itazamwe doesn't matter mama yupo au hayupo.

Then watoto wajengee library room TV wawe wanaangalia kila jumapili tu
 
Nyumba standard inatakiwa si tu kuwa na TV zaidi ya moja, bali hata sebule zinatakiwa kuwa zaidi ya moja. Kuruhusu watoto wakae sebule yao wakaangalia vitu vyao, na wakubwa wakakaa sebule yao wanaangalia vitu vyao.

Halafu hizo TV inatakiwa kila chumba kiweze kuwa na TV yake.

Yani ikibidi mpaka jikoni mtu akitaka kupika huku anaangalia vipindi vya mapishi aweze kuwa na ki TV cha kiushkaji cha jikoni.
Hii ni kwa maisha ya dunia ya kwanza, kiujumla hatujafika huko.
 
Back
Top Bottom