Wenye familia na watoto mnawezaje kutazama Runinga nyumbani?

Wenye familia na watoto mnawezaje kutazama Runinga nyumbani?

Nikishakubali matokeo kuwa kwangu Tv ya sebuleni sio mali yangu.

Nashukuru Mungu niliweka TV chumbani. Ninachotaka kuangalia nakiangalia chumbani kwangu. Huko sebuleni ni Nickelodeon na Cartoon Network.

Ningeweza kutumia ubabe wa ubaba lakini sioni faida yake. Ikiwa nipo hai acha wanangu wa enjoy nyumbani kwa baba yao.

Kwenye cartoon unawafundisha maarifa gani ya maisha?
 
Mimi kwangu watoto nimewapa amri ya kuangalia taarifa ya habari tu halafu ikiisha tv lazima izimwe,halafu huwa baadae nawauliza wanisimulie walichokiona kwenye taarifa ya habari
 
Hawa ni wababa wa enzi za ukoloni. Ni washamba na wanavaa MAYENU.

Kwanini usiwaache watoto wakaangalia katuni zao wewe uende chumbani ukasali hata rozari?

Watoto hawana raha, libaba linabadilisha tu chaneli! Khaaa!!!

Hili nalo mkalitazame!

cc Lamomy cocastic fundi bishoo Extrovert
Mimi TV sina mpango nayo ila simu yangu 24/7 haikai mbali nami
 
Eti?

Unarudi nyumbani unakuta watoto wanatazama katuni zao kwa raha zao, au tamthilia pendwa za kike..... unawezaje kubadili chaneli bila kuonekana katili?

Tuseme muda wa Taarifa ya Habari, au hata mechi pendwa za soka..... ukibadili channeli watoto hao wanakukimbia sebuleni unabaki mwenyewe.

Hujisikii vibaya?

Hapa ndo umuhimu wa kupitia maeneo fulani kabla ya kurudi nyumbani, wenzetu mnawezaje?
ungana nao ndio furaha ya familia, kama ni game cheza na mwanao, angalia hiyo tamthilia na mkeo akusimulie hiyo ndio furaha ya baba kuwepo nyumbani wape kipaombele wao, ndio furaha yao. Na ni jukumu la baba kuwapa furaha wale wa nyumbani mwake
 
""Then watoto wajengee library room TV wawe wanaangalia kila jumapili tu"""
Dr mbona utakua kauzu sana 😂😂😂

Watoto lazima waandaliwe kuwa thinker na sio follower.

And in this universe the beautiful things is invisible

Affection
Compassion
Sympathy
Empathy
Kindness
Humbleness
Goodness
Wisdom

So it is just hardest to my kids to be smarter and productive kwa kutazama TV lazima wasome Sana vitabu ili wapate insight.
 
Ukiwa dingi wa kiafrika unatakiwa uweke chanel ambayo nyumba nzima hawapendi alafu we mwenyewe huangalii unasinzia ila wakibadilisha tu chanel unashtuka usingizi unaisha halafu unawaambia rudisha haraka.
Dah we jamaa nimecheka balaa. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Eti?

Unarudi nyumbani unakuta watoto wanatazama katuni zao kwa raha zao, au tamthilia pendwa za kike..... unawezaje kubadili chaneli bila kuonekana katili?

Tuseme muda wa Taarifa ya Habari, au hata mechi pendwa za soka..... ukibadili channeli watoto hao wanakukimbia sebuleni unabaki mwenyewe.

Hujisikii vibaya?

Hapa ndo umuhimu wa kupitia maeneo fulani kabla ya kurudi nyumbani, wenzetu mnawezaje?
Wanapaswa kujua muda wa baba na muda wao.

Nimepanga kuja kuwa na setup room yangu.
Hii haitaingiliana na mambo ya sebuleni ni full gaming, movie and music. Inakuwa na sound proof kabisa.
 
Back
Top Bottom