Wenye nyumba wengi hapa Dar es Salaam ni watu maskini sana

Sio wanakimbilia mkuu uwezo ndio unalazimisha mtu afanye hivyo. Unafikiri nani ambaye hataki kuchukua apartment pale Kilimanjaro Kempinski mwaka mzima kama wewe ulivyopanga hotel nzima mkuu.
Mimi sijapanga apartment mkuu. Tupo wote kwenye nyumba za kupanga. Sema wengi tunakosea kwenye kuchagua vyumba pamoja na kusoma mikataba kabla ya kukilipia kodi.
 
Mkataba wa upangishaji unasoma kabla ya kulipa kodi??
Sijakuelewa, hiyo ni sehemu dogo kapanga. Kodi ya jengo imewekwa kwenye luku yake wakati mwenye nyumba anakaa hapohapo na pia hataki kutoa control number ili bili ilipwe moja kwa moja.

Haya huwezi kuyafahamu mpaka ukishaingia kwenye nyumba.
 
Jenga yako🤣🤣🤣
 
Si ujenge kwako ili kuondokana na hizo changamoto?Nyumba yake mwache ajiwekee masharti yake ukiona magumu hamia kwako.Eti wenye Nyumba maskini unamjua maskini wewe?
Ukipanga ni lazima usiwe na nyumba? Watu kibao wanaishi kinondoni, mikocheni na sinza ingawa wana nyumba kigamboni, bunju, mapinga, mbezi nk
 
Uliona mbali kwakweli.
 
Mwenye nyumba wangu hana hizo tabia.
Mzungu wa roho,kwanza hata kuonana physically hatujawahi.

Anakula zake cake ya taifa huko mji wao,,,na nasikia ana mijengo kama yote.

Bill ikitoka anaiforward.
Ukarabati anatuma fundi wake ndio basi hana usumbufu.
 
Hongera sana kwa kupata mmiliki wa nyumba mwenye hela. Hawa wamiliki maskini ni tatizo kubwa.
 
Mimi sijawahi kumwona LIVE mwenye nyumba wangu. Nilipopanga ni sehemu zimejengwa nyumba 12. Tunamjua meneja wake tu. Bill za maji na umeme kila nyumba inajitegemea. Mazingira ya nje kuna mfanya usafi kabisa haituhusu. Sisi usafi mwisho barazani. Hela pekee tunayochangishana ni ya ni ya kusomba taka. WENYE NYUMBA MASKINI NI KERO MJINI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…