Angalau
Seran umekuwa mwamanifu.Nashukuru pia nimepokea uzoefu na ushauri kutoka kwa watu mbalimbali naamini utanisaidia pia.
Binafsi nia yangu pia ni kuishi katika usafi bila kuzini🙏.
Nimejaribu kufatilia njia gani nitumie niweze kuwa mshindi katika hili… vita dhidi ya uzinzi na uasherati ni kali sana…
Kuwa na hisia kali za mapenzi naamini sio ugonjwa ni ishara kuwa afya ni njema na tukiona hisia zinakuwa kali yatupasa kumshukuru Mungu kwa kutupa zawadi hii.
Naamini moja ya njia ya muhimu ya kushinda hisia zinazotuelekeza kwenye uzinzi ni
kumtumaini Mungu kwa moyo wote.
Binafsi nakiri wazi kuwa kushinda dhambi hii si rahisi kwetu lakini kwa Mungu ni rahisi sana. Hakika kushinda dhambi hii ya uzinzi ni neema ya Mungu pekee.”
“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;” tumtumaini Mungu hata wakati akili zetu hazielewi tutashindaje.Tusiwe na mashaka je kesho, mwakani je nitaweza kudumu kuwa mwaminifu bila kuzini..??? Kama leo ametuwezesha kuwa washindi kesho na kesho kutwa tutashinda pia.
Pia nimegundua dhambi zingine tunaweza kuomba tukazikemea na kushinda lakini katika uzinzi Biblia inasema yenyewe tusijadili nayo tuikimbie kabisa …”
Ikimbieni zinaa…. ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.”
Jambo la mwisho
Yesu Kristo ndiye kielelezo pekee katika kushinda dhambi zote…”
“bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.”
Yeye aliwezaje kushinda… kwa ufupi nikitazama maisha ya
Yesu duniani alishinda sana ubinafsi kwa kutamani kuishi tu akimpenda Baba wa mbinguni na kuwahudumia sana wanadamu wengine. Hivyo alikuwa na maombi mengi ili kujua mapenzi ya Mungu na kuyatenda.
Hisia zetu zinapotupelekea kuzini ni kwasababu ya ubinafsi wa kutaka kujiridhisha…
tutamani kuishi kwaajili ya Mungu na kuwatumikia wengine tutashinda ubinafsi hatimaye uzinzi pia.
Kwa kusisitiza mwandishi mmoja anaitwa E.G.White anaandika ..”Our heavenly Father has a thousand ways to provide for us of which we know nothing. “MH 481.2 Naamini Mungu ana njia nyingi kusaidia kukidhi mahitaji yetu hata kukidhi hisia zetu kabla ya kuingia kwenye ndoa.
Angalizo: Hisia za mapenzi zinapokuja tusitafute njia yoyote kushindana nazo labda kwa kushiriki mapenzi kwa namna yoyote ile(kwa ambao hawako kwenye ndoa.) Hisia kamwe si za kudumu kwa utulivu baada ya muda fulani zinapotea tunarudi kuwa kawaida.
Tunayaweza yote( hata kushinda dhambi ya uzinzi) kupitia Mungu anayetutia nguvu. Mungu na atusaidie🙏.