Miss Natafuta
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 28,122
- 52,886
Unaendeleaje KwanzaSijakuelewa unaposema shetani hayupo! Kama hayupo tunamkemea nani na tunaomba ili iweje? Shetani yupo na ni adui, nadhani unajua matendo yake maovu ata bila kufundishwa, matendo mema tunayojifunza kutoka kwa neno la Mungu yanakukwaza wapi?
Na pia ni kweli maandiko yanaonya kuhusu manabii wa uongo na watumishi wa kujifanya Mathayo 7:15-23 inasema wazi kuhusu hilo. Lakini pia tunakumbushwa tusihukumu kwa haraka bali "tuipime roho" (1 Yohana 4:1) na kumwachia Mungu haki ya mwisho! Utajikuta unaingia vita na Mungu bure Kwa kuwashuku au kuwatusi watumishi wake, nina uhakika hiyo sio kazi yako muachie Mungu mwenyewe! Amini unachokiamini na uishi humo! Unaongea kwa uchungu sana sijajua kimekutokea nini, ila nina imani ukiamua kuamini tu sina hakika kama tunapata hasara yoyote katika kuamini tu!ni heri uamini Mungu yupo usimkute, kuliko kuamini hayupo ukamkuta!! Utamwambia nini? Ni kasheshe, binafsi tangu niokoke sijapoteza kitu! Kwahiyo sioni hasara! Na kama manabii wa uongo wapo basi na wa kweli wapo!! Kwanini usifocus na wakweli? Kama humwamini mwamposa au sjui nani ni lazima uwafatilie hao?
Hawajabeba hatma ya wakristo ulimwenguni kote, mtafute unaye mwamini ishi hapo! Naona wengi sana mnapinga watumishi bila wa kuwafatilia hata kidogo bila kusoma maandiko! Huenda mmesikia tu au umesoma sehemu ukakuta wakiwapinga nawe ukaliunga… nakushauri;
Avoid Hast generalizations!!
Kuhusu lugha ya kejeli na matusi, haileti majibu ya kweli wala haioneshi hekima. Yakobo 3:10 inatufundisha kwamba kinywa kimoja hakiwezi kutoa baraka na laana kwa wakati mmoja. Tujibu kwa upole na hekima ili tupambane na uongo bila kuingia kwenye dhambi ya chuki au dharau.
Achana na watu judgemental