Nimekuelewa mamake. Langu lilikuwa angalizo la jumla tu kuhusu the law of attraction; and it was necessarily not about you.
Kwa kizazi hiki cha Gen Z nadhani mparaganyiko ndiyo utakuwa mkubwa zaidi maana watoto ni kama wanajilea wenyewe tu. Na thamani ya mwanamke inazidi kushuka maana mbali na kutoa mbususu, mwanamke anaonwa kama vile hana kingine cha maana. Labda hili vuguvugu la wanawake kushika mavyeo makubwa makubwa litasaidia japo nadhani tatizo hasa ni huko chini kwenye malezi.
Na mbaya zaidi juhudi nyingi zimewekezwa kwa mtoto wa kike. Mtoto wa kiume ametelekezwa na kwa hali ya sasa nadhani ni wazi kwamba ni kazi ngumu to raise real men ambao wanajitambua na watakaoweza kusimama kama wakuu wa familia, walezi, walinzi na makuhani wa familia zao huko mbele ya safari. Huku nako mabinti ndiyo kwanza wanafundishwa mambo ya usawa 50/50 full feminism.
Something gotta give!
Umeongea jambo la maana sana. Ni kweli kuna mparaganyiko mkubwa, hasa kwenye suala la malezi. Vijana wa kiume wengi wanapotea kwa sababu hawapati uelekeo wa kiume wa maana, na kwa upande wa mabinti, dunia inawasukuma zaidi kwenye ‘image’ badala ya utu. Tunahitaji kurejesha mizani, kwa neema ya Mungu.😥
Ukiangalia tu dada zetu pia wanajishusha wenyewe thamani kwa mambo ya aibu kabisa! Wengine wakifanikiwa wanajiweka juu pia,(sio kwa ubaya lakini) ukiwa masikini ni mateso makubwa😅kwaio mwanamke amechoka kuonekana kama kiumbe dhaifu! Wengine kutumika kama chombo cha starehe kwa mapenzi au sio mapenzi yao!
Mi huwa najiuliza ni kutokana na enzi za mababu zetu, kuna mambo yalitokea zamani unajua, mwanamke hapelekwi shuleni, haruhusiwi kusimama mbele au kuongoza watu! Waliolewa wadogo sana walinyimwa haki zao kama wanazopata wanaume! Kwaio ili kuyaondoa haya ilibidi women movement ifanyike na wanaume walikuwemo usifikiri wanawake tu😅 ndio feminism ikatokea na kuraise awareness amongst themselves! Kwa hivyo kuna wanaume ni mafeminist pia!
Pia kwa ninavyoelewa Feminism ni harakati au mtazamo wa kijamii unaolenga
kuhakikisha usawa wa kijinsia hasa kupigania haki za wanawake ili wawe na nafasi sawa na wanaume katika jamii, kazi, elimu, siasa, na maisha kwa ujumla.
Na ilitokea ili;
~Kupigania haki za wanawake
~Kupinga ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia
~Kuweka mazingira ya usawa kati ya wanaume na wanawake na siyo kumpa mwanamke nguvu ya juu zaidi, bali nafasi sawa.
Waliosoma elimu ya jamii hapa wananielewa zaidi