Nakadori
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 8,778
- 21,010
Wana wa mama tozo hopeful mnapambana ipasavyo...
Basi bwana mwezi uliopita nikiwa benk flan ya kikulima kikulima nikakutana na ndugu yangu kwenye ukoo tulipotezana mda sana. Huyu ndugu alikuwa na mkewe pamoja na rafiki wa mkewe. Hawa wanawake wote walikuwa na vibendi vikubwa tu vya kujifungua Leo kesho.
Kutokana na foleni kwenye benk hii hasa mwisho wa mwezi tukajikuta tumeshazoeana na hawa wanawake wawili as if tunajuana mda mrefu na story zikaanza kunoga.
Heeeeh huku na huku yule rafiki wa mke wa ndugu yangu akachomekea ishu za kumtrak mumewe ajue alipo, akawa anajisemea ngoja nichek kama yuko ofisini au ametoka. Kumbe bwana amefunga sijui ndo gprs au ndo nini (me sikutaka hata kujua kilichofungwa na kwamba kimefungwa kwenye gari au kwenye simu). Akawa anajisemea Leo atanitambua na atasema hapa alikuwa wapi....?
Kweli wanawake ndo tumefikia kuwafanyia wanaume hivi ili kuwalinda wasichepuke? Nilimhurumia bi dada na tumbo lake lililochomoka, nikajisemea huyu anataka kuzaa kabla ya majira yake, mambo gani ya kuchungana kama ng'ombe jamanii? Na wewe mwanaume na ndevu zako unakubali kabisa kutrakiwa?
Mwanaume akiamua kutulia anatulia mwenyewe ila sio kwa kuwa anachungwa, na pia mwanaume akitulia ni kwamba atapunguza list ya wanawake atabaki na mmoja hivi...yani hapo ndo ametulia.
Hivi wanawake wa ndoa mbona mnajipaga stress, mmegeuka mapolisi kwa wanaume zenu yani hawapumui hawana tena ule uhuru kabisa, kifungo kifungo kweli.
Me mambo ya kuchungana kwa style hii asee nanyoosha mikono juu.