Wewe ndio chanzo cha umasikini katika familia yenu

Nmecheka ila sijui nimecheka nini😅😅
 
Hichi ulichoandika mkuu siku zote kitazidi kuturudisha nyuma ama kutudumaza. Acha ukweli usemwe. Tukianza kubembelezana na kutafutiana lugha laini, kamwe hatutasonga na kuuaga umasikini. Siku zote ukweli mchungu na unauma vibaya mno, lakini hatuna namna lazima tuunywe. Unapowaona Israel wameendelea kiuchumi, kijeshi na kijamii ujue hawakuchekeana. Waliambiana ukweli, jasho liliwatoka na hatimae leo wamekuwa miongoni mwa mataifa super power. Vijana tuache kudeka. Ajira Kama hazipo kafyatue hata tofari uuze, nenda shambani kalime, kachime mkaa wa kupikia uuze, jifunze ufugaji ama nenda migodini kachimbe madini. Tanzania ni nchi iliyobarikiwa fursa lukuki. Tuache kutumia mda mwingi kwenye mambo yasiyo na tija, hakika ipo siku Tanzania tutakuwa wazalishaji wakubwa duniani wa mazao ya mifugo na shambani. Vijana watoke magetoni!!
 
Nitajie matajiri watano kutoka kwenye 'top list' ya dunia (1-100) wenye watoto wengi
 
Hivi unajua elfu 10 miaka thelathini iliyopita ulikuwa unanunua kiwanja kabisa, hesabu zako hazijakaa vzur
Tafuta maana ya time value of money na maana ya inflation. 30,000 ya sasa ni sawa na 500 ya mwaka fulani. Ukiwa unapiga hesabu kwa sasa unataja thamani ya sasa hivi na ukipiga hesabu ya zamani unataja kiasi kile kisha subject ya thamani ya sasa.
 
Muhimu ni kukubali ukweli, na kuchukua hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…