Wewe ni mkubwa kuliko shilingi milioni Kumi

Wewe ni mkubwa kuliko shilingi milioni Kumi

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Screenshot_20241228_090833_Google.jpg

Hivi leo hii ukisikia mtu kaokota shilingi milioni kumi [10,000,000] halafu kaipeleka polisi au karudisha kwa mwenyewe,je utamwonaje? Bilashaka wengi wetu tutamwona ni mpumbavu

Ukweli ni kwamba mtu huyu ni mkubwa kuliko hiyo hela ambayo wengi wetu tunababaika nayo,yupo imara kiroho,kihisia na ana uwezo mkubwa wa kudhibiti tamaa yake,akisema hapana ni hapana na akisema ndio ni ndio,hakuna tena migongano au mvutano wa fikra zake

Hata sisi ni wakubwa pia ni vile tu bado hatuja tumia uwezo wetu wa ndani kabisa,sisi ni wakubwa kuliko dharau tunazo fanyiwa na watu mbali mbali katika maisha yetu ya kila siku,ukiwa mkubwa kuliko dharau unazofanyiwa,utazipuuza na hazita kuumiza kichwa na kushindwa kufanya mambo yako binafsi

Ukiwa mkubwa hautashindwa kusamehe makosa uliyofanyiwa na binadamu wenzako,kwakuwa unajua wewe ni mkubwa kuliko hayo makosa uliyofanyiwa hivyo unaweza kuwasamehe wale wote walio kukosea,lau ukiamini wewe ni mdogo kuliko hayo makosa hakika hautaweza kuwasamehe watu na utaishi kwa vinyongo kila siku

Tambua kwamba wewe ni mkubwa kuliko hayo mapenzi ambayo kila siku yanakuumiza kichwa na hisia zako pia,unaweza kuyaweka pembeni na kusonga mbele,kwakuwa unajua wewe ni mkubwa kuweza kupata mwenza mzuri zaidi atakayeendana na vigezo vyako

Kwa jambo lolote na hali yoyote utakayo kutana nayo maishani tambua wewe ni mkubwa kiroho,kihisia,kimtazamo na una uwezo wa kuhimili hali hiyo kwakuwa uwezo huo unao

Ni hayo tu!
 
Nitarudisha pesa ya kuokota kama tu;

  1. nimemuona alieidondosha.
  2. kumetangazwa kupotea hiyo pesa na muhusika.
Sitokuja kufanya kosa la kuokota pesa na kuipeleka Polisi. Polisi ni wezi na majambazi. Kupitia hiyo pesa wanaweza hata kunidhuru ili wajimilikishe.
 
Yaani niokote pesa nikawapeleke polisi, POLISI hawa hawa ninaowajua mimi, ndugu yangu huwajui polisi wetu vizuri.
Ikiwa imetangazwa basi ninaweza rejesha.

Lakini pia inahitaji imani kubwa haswaa, una dhiki zako, mwanao anahitaji laki 7 hapo muhimbili, nyumba yako inahitaji milioni 2 kupaua upya, mabati ya sasa yanavuja.
Inahitaji imani ya level ya juu sana.
 
Hapo kwenye dhiki na mahitaji yako ndio inahitajika ustahamilivu wa kutosha kupinga tamaa yako binafsi au uwe mkubwa kushinda tamaa yako na kurudisha hela za watu

Wengi wetu hapa ndio kwenye mtihani boss
 
Nitarudisha pesa ya kuokota ya kiasi hicho kama tu;

  1. nimemuona alieidondosha.
  2. kumetangazwa kupotea hiyo pesa na muhusika.
Sitokuja kufanya kosa la kuokota pesa na kuipeleka Polisi. Polisi ni wezi na majambazi. Kupitia hiyo pesa wanaweza hata kunidhuru ili wajimilikishe.
Unafanya masihara na chombo cha dolla wewe, aisee wewe hebu panda kwenye arrest. Kwa lafudhi ya kihaya😂😂😂
 
Nakumbuka Mwaka fulani niliiokota hela kwenye bahasha zaidi ya 1.2 million ilikuwa chini ya uvungu wa gari. Nilipoichukua ile bahasha nikatetemeka sana maana kipindi hicho kulikuwa na habari za watu kutega hela za majini ilikuwa Zanzibar.

Nilipoiokota ile bahasha nikamfuata jamaa mmoja alikuwa na huduma za Tigo/Mpesa huku natetemeka nikamwambia nimeokota hii bahasha Kaka akaniambia tuipige pasu nikampa kama laki 3 hivi nyingine ikabaki nayo.

Baada ya masaa mawili yule jamaa akanifuata na yule mtu aliyepoteza ile hela na huyo jamaa nilikuwa sipigi naye story maana alikuwa anajifanya much know sana. Wakanifuata mpaka ofisini wakaja kuniulizia nikatoka nje yule jamaa aliyepoteza ile Hela alikuwa amelowa jasho natetemeka.

Akawa anasema Mwanangu hiyo hela nilikuwa naenda benki kui deposit nimefika mpaka benki kuangalia bahasha kwenye begi siioni na ilikuwa ni hela ya Kampuni aliyokuwa anafanya kazi. Kampuni ya simu vodacom.

Akaonyesha mpaka form za deposit alizokuwa amejaza na amount ni ile ile 1.2 Million ikabidi nimrudishie kama 900,000 yote. Akanipa laki 1

Tangu siku ile jamaa Akawa mshikaji na akaniomba msamaha kwa ujuaji alizokuwa ananifanyia. Na Akawa ananipa na kazi za kufanya repair ya computer zao pale ofisini kwao.
 
Nitarudisha pesa ya kuokota ya kiasi hicho kama tu;

  1. nimemuona alieidondosha.
  2. kumetangazwa kupotea hiyo pesa na muhusika.
Sitokuja kufanya kosa la kuokota pesa na kuipeleka Polisi. Polisi ni wezi na majambazi. Kupitia hiyo pesa wanaweza hata kunidhuru ili wajimilikishe.
Yaani nipeleke polisi, sio milioni 10, hata laptop ya laki 7 sipeleki unless aliyepoteza katangaza au nimemuona akisahau au kudondosha
 
Siwezi rudisha pesa kama hiyo nikiokota niwe nimemuona aliyedondosha au sijamuona. Hiyo pesa inakuwa halali yangu.
Hapo wewe ni mdogo kuliko hiyo hela hauna ustahamilivu na ujasiri wa kusema hapana

Hii ndio mifano ya viongozi wengi barani Afrika ikiwemo Tanzania,wanaweza kupindisha sheria au kuingia mikataba mibovu kwakuwa wao ni wadogo kuliko hela,lau wangekuwa wakubwa kupita hela wangeangalia maslahi mapana ya taifa
 
Nakumbuka Mwaka fulani niliiokota hela kwenye bahasha zaidi ya 1.2 million ilikuwa chini ya uvungu wa gari. Nilipoichukua ile bahasha nikatetemeka sana maana kipindi hicho kulikuwa na habari za watu kutega hela za majini ilikuwa Zanzibar.

Nilipoiokota ile bahasha nikamfuata jamaa mmoja alikuwa na huduma za Tigo/Mpesa huku natetemeka nikamwambia nimeokota hii bahasha Kaka akaniambia tuipige pasu nikampa kama laki 3 hivi nyingine ikabaki nayo.

Baada ya masaa mawili yule jamaa akanifuata na yule mtu aliyepoteza ile hela na huyo jamaa nilikuwa sipigi naye story maana alikuwa anajifanya much know sana. Wakanifuata mpaka ofisini wakaja kuniulizia nikatoka nje yule jamaa aliyepoteza ile Hela alikuwa amelowa jasho natetemeka.

Akawa anasema Mwanangu hiyo hela nilikuwa naenda benki kui deposit nimefika mpaka benki kuangalia bahasha kwenye begi siioni na ilikuwa ni hela ya Kampuni aliyokuwa anafanya kazi. Kampuni ya simu vodacom.

Akaonyesha mpaka form za deposit alizokuwa amejaza na amount ni ile ile 1.2 Million ikabidi nimrudishie kama 900,000 yote. Akanipa laki 1

Tangu siku ile jamaa Akawa mshikaji na akaniomba msamaha kwa ujuaji alizokuwa ananifanyia. Na Akawa ananipa na kazi za kufanya repair ya computer zao pale ofisini kwao.
Nimeipenda hii

Siku zote ukiwa mkubwa kuliko jambo fulani huwa unapata kingi zaidi,hizo repair ulizokuwa unafanya naamini kabisa zilizidi gharama ya hiyo hela uliyookota

Kuna mifano mingi ya watu waliokota pesa na kuzirudisha kwa wenyewe na kupata dili kubwa zaidi kwakuwa wamedhibitisha kwamba wanathamani na ukubwa unaostahili mambo makubwa zaidi
 
Back
Top Bottom