Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Hivi leo hii ukisikia mtu kaokota shilingi milioni kumi [10,000,000] halafu kaipeleka polisi au karudisha kwa mwenyewe,je utamwonaje? Bilashaka wengi wetu tutamwona ni mpumbavu
Ukweli ni kwamba mtu huyu ni mkubwa kuliko hiyo hela ambayo wengi wetu tunababaika nayo,yupo imara kiroho,kihisia na ana uwezo mkubwa wa kudhibiti tamaa yake,akisema hapana ni hapana na akisema ndio ni ndio,hakuna tena migongano au mvutano wa fikra zake
Hata sisi ni wakubwa pia ni vile tu bado hatuja tumia uwezo wetu wa ndani kabisa,sisi ni wakubwa kuliko dharau tunazo fanyiwa na watu mbali mbali katika maisha yetu ya kila siku,ukiwa mkubwa kuliko dharau unazofanyiwa,utazipuuza na hazita kuumiza kichwa na kushindwa kufanya mambo yako binafsi
Ukiwa mkubwa hautashindwa kusamehe makosa uliyofanyiwa na binadamu wenzako,kwakuwa unajua wewe ni mkubwa kuliko hayo makosa uliyofanyiwa hivyo unaweza kuwasamehe wale wote walio kukosea,lau ukiamini wewe ni mdogo kuliko hayo makosa hakika hautaweza kuwasamehe watu na utaishi kwa vinyongo kila siku
Tambua kwamba wewe ni mkubwa kuliko hayo mapenzi ambayo kila siku yanakuumiza kichwa na hisia zako pia,unaweza kuyaweka pembeni na kusonga mbele,kwakuwa unajua wewe ni mkubwa kuweza kupata mwenza mzuri zaidi atakayeendana na vigezo vyako
Kwa jambo lolote na hali yoyote utakayo kutana nayo maishani tambua wewe ni mkubwa kiroho,kihisia,kimtazamo na una uwezo wa kuhimili hali hiyo kwakuwa uwezo huo unao
Ni hayo tu!