WHO wathibitisha pombe ni sumu. Sasa nina ujasiri wa kusema: "kunywa pombe bila kulewa ni dhambi."

Mimi kilevi changu warembo. Wewe ni mrembo ?
Aisee kama warembo ndio kilevi chako basi ujue hiyo ni sumu kali kuliko pombe! Sura za warembo zinaweza kukuletea magonjwa hatari kama gonorrhea, chlamydia, syphilis, UKIMWI, na hata hepatitis B!

Mbaya zaidi ukiondoka duniani utatupwa motoni. Chagua leo: kilevi chako kiwe Neno la Mungu(Biblia). Isome kila siku uyajue mapenzi ya Mungu
 
Yesu hakuwa mlafi, hakuwa mlevi Wala hakutenda dhambi. Ila Yesu alikula, alikunywa mvinyo, alishinda na wenye dhambi.
Imeandikwa wapi kwamba Yesu alikunywa mvinyo(Alcoholic beverage)
Ulafi ni dhambi ila chakula si dhambi, Ulevi ni dhambi ila pombe si dhambi, Uzinzi ni dhambi ila mwanamke au mwanamke si dhambi. Elewa hii mantiki!!
Shirika la Afya(WHO) limeishakuambia pombe ina sumu na sumu hiyo inaharibu ini, ubongo nk Na Biblia imesema tusiliharibu hekalu la Mungu ambalo ndilo sisi, yaani miili yetu. Ukinywa pombe kwakuwa ina sumu, utakuwa unauharibu mwili wako.

Bado tu hujaona kuwa pombe ni dhambi?
 
Pombe NI sumu?


Mbona sukari NI sumu .

Chumvi ni sumu

Hata maji ya kizidi Sana mwili NI sumu .


Soma ili andiko 78:65 Kisha Bwana akaamka Kama mtu aliyelala usingizi Kama shujaa aliyeshindwa na mvinyo"

So Bwana Mungu alikuwa pombe NI sumu ?
 
Hoja yako ya kisayansi kuhusu nyama nyekundu ni sahihi kwa muktadha wa afya, lakini sio sahihi kwa muktadha wa dhambi. Pombe iko kwenye kundi tofauti kabisa: WHO imeiweka kama Group 1 carcinogen, yaani inahusishwa moja kwa moja na saratani kwa binadamu. Zaidi ya hapo, pombe huathiri sio tu mwili, bali akili, maamuzi, tabia, familia, roho na maisha ya kiroho.

Na Biblia haijawahi kukataza kula nyama ya ng'ombe, au pork. Lakini kuhusu pombe, imeandikwa wazi:
‘Wala msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho’ (Waefeso 5:18).
Na tena:
‘Walevi hawataurithi ufalme wa Mungu’ (1 Wakorintho 6:10).

Kwa hiyo, sio kila kitu chenye hatari kiafya ni dhambi kiroho.

Kuhusu miili yetu kuwa hekalu, kumbuka siku ya Pentekoste Roho Mtakatifu aliposhuka. Wanafunzi wa Yesu wote walijazwa Roho Mtakatifu wakaanza kunena kwa lugha. Huo ni udhihirisho kuwa miili yetu hii hii ndiyo hekalu la Roho Mtakatifu. Ndio sababu tunaambiwa tusilewe kwa mvinyo ambamo mna ufisadi bali tujazwe Roho (Waefeso 5:18). Naamini umenipata vizuri Until_The_End
 
Kwanza kabisa, namshukuru Mungu kusikia ushuhuda wako wa kutoka kwenye ulevi. Miaka 28 ya ushindi sio jambo dogo. Hongera sana na Mungu akupe nguvu uendelee kuwa nuru na chumvi kwa wengine.

Kuhusu hoja ya WHO na viwanda vya pombe, ni vizuri kufahamu kwamba kwa sasa baadhi ya nchi duniani, hasa Ulaya na Canada, tayari wameanza kuweka maonyo ya kiafya kwenye chupa za pombe. Mfano: ‘Alcohol causes cancer’ au ‘Drinking harms your health.’ Hii ni kwa sababu WHO ilitoa ripoti hiyo rasmi mwaka juzi tu, 2023 kwamba “There is no safe amount of alcohol that does not affect health.”

Kwa hiyo, hatua zimeanza, lakini mataifa mengi yanasita kuweka labels za onyo kwa sababu pombe ni biashara kubwa sana duniani. Hata kwenye sigara haikuwa rahisi kuweka onyo hilo kabla ya mashinikizo ya kiafya na kisiasa kuongezeka. Nchi zinazotegemea pombe kama kitega uchumi zikiweka onyo ni wazi mapato yataporomoka maana wengi watashtuka kunywa pombe.

Siamini kwamba watu hawaogopi UKIMWI. Wanaogopa, lakini uzinzi ni addictive, ni roho inayomvaa mtu. Mtu anaogopa na anajua ni hatari lakini kwakuwa amefungwa minyororo hawezi kujinasua. Si ulisikia USA waliposema wataondoa msaada wa ARVs, wengi walisikitika. Na hizo ARVs kwa sehemu zimekuwa zikiwafanya watu waone UKIMWI kama vile sio hatari. Sisi tuendelee tu kusema ukweli hata kama kuna watu ambao jambo hili halitaingia akilini mwao.
Mithali 22:3
Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.
 
kawaambie breweries....wapo njia kuelekea njiro karibu na dampo Arusha.
 
Kinondoni pale makaburi ya walokole yapo mengi sana ,kifo ni kifo
Kifo sio kifo ndugu yangu fogoh2
Mlokole akifa anakwenda mbinguni, hivyo kufa kwake ni faida (Wafilipi 1:21-27). Mwenye dhambi akifa anakwenda motoni hivyo kufa kwake ni hasara. Ndio sababu nakazana kuwaonya watu waache kunywa pombe ili wakiondoka duniani wasijikute motoni.
1 Kor 6:9-11
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.
 
Na mkasome 1tim,
Mkasome ,1 tim , 5,23
Hiyo nimeishaijibu kwa undani, soma replies zangu zote. Kwa ufupi hiyo sio contradiction. Timotheo aliambiwa anywe kwa ajili ya magonjwa yake ya tumbo. Wewe unakunywa kwa ajili ya tumbo linalouma? Halafu mvinyo wa nyakati za Biblia sio sawa na mvinyo au pombe zinazotengenezwa siku hizi. Za sasa zinawekwa ethanol ya hatari sana
 
Hii ni hoja ya kifalsafa inayoonekana kama ina mantiki, lakini inapingana moja kwa moja na mafundisho ya Biblia kuhusu hekalu la Mungu na nafasi ya mwili wa mwanadamu katika maisha ya kiroho.
My friend, it’s a misunderstanding to say that the body isn’t part of ‘you’ in God’s eyes. The Bible clearly states in 1 Corinthians 6:19–20:
‘Your bodies are temples of the Holy Spirit... therefore glorify God in your body.’

The body is not just a vessel you own, it’s a sacred part of your whole being. That’s why Scripture warns against defiling it with sin like drunkenness or sexual immorality. To reinforce this, Paul writes: ‘Every sin a person commits is outside the body, but whoever sins sexually sins against their own body’ (1 Corinthians 6:18).

This means your physical body is not spiritually irrelevant, it matters deeply to God. Defiling it through sin, especially sexual immorality or intoxication, is a direct offense to the temple God has made you to be.

1 Corinthians 3:17 also says, ‘If anyone destroys God’s temple, God will destroy that person.’
And that temple, according to Scripture, includes your physical body
 
Hakuna kisicho na sumu kwa sasa. Hata maji ya kwenye chupa yana sumu.
Ni kweli vitu vingi vina kemikali mbaya, lakini hatupaswi kusema ‘hakuna kisicho na sumu’ ili kuhalalisha kunywa sumu inayojulikana wazi kabisa kuwa ni hatari kama pombe.

Tofauti ya maji na pombe ni kwamba:
  • Pombe inaingia mwilini na kumlewesha mtu, anapoteza fahamu, anaendesha gari vibaya anasababisha ajali, ini lake linaharibika. Anagombana na mkewe. Anashindwa kuitunza familia yake
  • Lakini mtu akinywa maji yanatumika kuhuisha mwili, si kuufanya mwili upoteze fahamu au kuharibu ini.
  • Isitoshe WHO haijapiga kelele kuhusu maji ya chupa, lakini imesema wazi: ‘There is no safe amount of alcohol that does not affect health’.
Unaposema "hakuna kisicho na sumu kwa sasa" unahalalisha kunywa sumu yoyote ile. Kama ni hivyo, je uko tayari kunywa acid au sumu ya panya kwa kisingizio hicho? Kama sivyo, basi usihalalishe madhara ya pombe kwa hoja za jumla jumla.
"Mwenye busara huona mabaya, akajificha." (Methali 22:3)
 
Nakubaliana na wewe @Techinoshin kwamba baadhi ya vitu tunavyotumia kila siku vinaweza kuwa na chembechembe hatarishi, lakini mboga mboga safi na uji wa kawaida wa nyumbani havijaorodheshwa na WHO kama visababishi vya kansa (carcinogens). Mboga zinasaidia sana kupunguza hatari ya kansa kwa kuwa zina virutubisho vya asili. Uji nao ni salama, isipokuwa tu kama mahindi yameharibika na kuwa na fangasi aina ya aflatoxin, ambayo inaweza kuwa sumu.

Tofauti yake na pombe ni kubwa: pombe imeainishwa na WHO kama “Group 1 carcinogen”, sawa na sigara na asbestos, yaani imethibitishwa kusababisha saratani kwa binadamu. Kwa hiyo, sio sahihi kusema "kila kitu ni sumu" kama kisingizio cha kupuuza hatari ya pombe, ambayo madhara yake ni ya moja kwa moja kwa mwili na roho.

Biblia imesema tusiwe miongoni mwao wanywao mvinyo/pombe, haijasema tusiwe miongoni mwao wanywao uji au walao mbogamboga. Iko wapi hapo ngoma droo?
 
Maswali yako ni ya msingi kabisa MwananchiOG, na hayapaswi kujibiwa kwa mzaha. Vitabu 66 vinavyopatikana kwenye Biblia ya Kiprotestanti vilipitishwa kwa uangalifu mkubwa na mitume na kanisa la awali, vikijulikana kama Canon, yaani maandiko yaliyoandikwa kwa uongozi wa Mungu, na kuthibitishwa kwa ushahidi wa mitume, manabii, na Roho Mtakatifu mwenyewe.

Hivyo vitabu 66 vilitumika mapema kabisa na Wakristo wa karne ya kwanza, hata kabla ya makanisa kugawanyika madhehebu. Kwa mfano, Yesu na mitume wake walinukuu mara kwa mara kutoka vitabu vya Agano la Kale ambavyo viko kwenye orodha hiyo, lakini hawakunukuu hata mara moja kutoka kwenye vitabu vya Deuterocanon kama Yoshua bin Sira.

Tafakari hii ya maandiko haitegemei tu madhehebu au elimu ya binadamu, bali historia ya ufunuo wa Mungu mwenyewe. Kama una ushahidi wa kihistoria unaoonyesha kuwa Yoshua bin Sira ni sehemu ya ufunuo wa Mungu unaolingana na Kristo na mitume, basi ulete hapa kwa hoja badala ya matusi au hasira.
Mhubiri 7:9
Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu (2 Wakorintho 13:1)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…