Wilaya ya Ruangwa wamwambia Rais Samia hakuna changamoto yoyote ya kufanyia kazi

Wilaya ya Ruangwa wamwambia Rais Samia hakuna changamoto yoyote ya kufanyia kazi

Rais Samia Suluhu amesema amekuta Ruangwa hali ni tofauti na maeneo mengine ambapo kote alikopita amepokea changamoto nyingi za kwenda kufanyia kazi, lakini Ruangwa wamemwambia hawana changamoto yoyote, Ruangwa wametaja mazuri waliyofanyiwa na Serikali. Rais Samia amewapongeza mkoa wa Lindi na wilaya ya Ruangwa kwa maendeleo makubwa.

Rais Samia ameahidi kumtunza waziri mkuu kwa kupeleka maendeleo zaidi Ruangwa kutokana wadhfa wake kuwa na kazi nyingi. Rais Samia amesisitiza lazima Serikali ipeleke maendeleo Rungwa.

Rais Samia Suluhu ameanza ziara yake ya kikazi mkoani Lindi na leo Septemba 18, 2023 amehutubia wilayani Ruangwa baada ya kumaliza ziara mkoani Mtwara.

Sasa watu wa Ruangwa si ndo wale waliovaa vinyago na kuweweseka kama matahira?
Unategemea wawe na changamoto wale??
 
Back
Top Bottom