Wimbo mpya wa Nay wa Mitego kuhusu bandari views 71,000 ndani ya saa 7

Wimbo mpya wa Nay wa Mitego kuhusu bandari views 71,000 ndani ya saa 7

Wimbo mpya wa Nay wa Mitego unaoitwa amkeni unaozungumzia sakata la Bandari, Ripoti ya CAG na ugumu wa maisha umefikisha watazamaji 71,000 na comments zaidi ya 2,000 ndani ya masaa 7 tu tangu uachiwe hewani

Elimu ya bure haina maana. Nimemwelewa sana
 
Attachments

  • Screenshot_20230906-195302_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20230906-195302_WhatsApp.jpg
    73.3 KB · Views: 1
Unajitahidi kidogo sio mbaya kutosoma sio kosa lako .Soma hapa madaraka huwa yanatoka kwa nani
pia raisi ana mamlaka kikatiba nyie ndio jamii ya mdudu "mavu" mkisha jua kujenga senga tayari mnadhani tayari ni wahitimu na kusahau kuna kujifunza na kutengeneza asali usipende kuchoropoka na aya moja nakudhani umeumaliza msahafu
 
Rais huwa anaapia katiba .kumaanisha iko juu yake .katiba inasema mamlaka zote lengo kuu ni sisi kustawi sio yy kuheshimiwa .kifupi rais ni housegirl wa wananchi
 
Kuna hii kasumba ya kutotaka kukosolewa kqa viongozi wa afrika,sijui ni kwanini wanaogopa kukosolewa???..

Yaani mtu anayekosoa huwa anaonekana kuwa tishio kubwa sana kwa maisha yao na hata usalama wa taifa,ili hali mtu huyo alipaswa kusikilizwa kwa kina kwa sababu ana kitu cha kufundisha.

Ajabu tunawapenda wanaosifia tena hata kwa sifa za kinafiki na uongo(kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa).

Afrika bila unafiki,hatuwezi kutoboa.
 
Back
Top Bottom