Within 3 month kilimo kimenipa milioni 40, vijana kilimo kinalipa

Dha! Nilikosa ofa ya nyama choma. Lini tena mkuu utakuwa hapo nyumbani lounge unipe ofa ya kuku choma
 
Mkulima serious hawezi kuandika hivi.
 
mbona unakimbilia kwenye kupata milioni 40? Hizo heka kadhaa ni nini?

sema ulilima heka ngapi?
ulitumia sh. ngapi kulimia?

Palizi sh. ngapi kama ipo

kama mbolea inahusika sema ilitumika gharama kiasi gani?

Umeuza kwa sh. ngapi mpaka umepata hiyo milion 40? na je hiyo Miln 40 ni baada ya gharama zote? usiwaingize wenzio chaka
 
Kuna jamaa aliletaga uzi wake mzuri tu na mchanganuo jinsi alivyolima mahindi na faida aliyoipata, aliweka kwa mtindo wa episode nimeisahau jina la uzi
 
Kuna jamaa aliletaga uzi wake mzuri tu na mchanganuo jinsi alivyolima mahindi na faida aliyoipata, aliweka kwa mtindo wa episode nimeisahau jina la uzi
Hiyo ndio inayotakiwa ili mtu akitaka akitaka kuytimba ayatimbe mwenyewe
 
Hahahaha binafsi nililima heka 30 sehemu inaitwa naungo ipo karibu na nanjilinji, nilikodi kila heka kwa elfu 40, kila heka nilifyeka kwa 30000 na kila heka nilitumia lita 2 za kiua magugu,wasukuma walinitibulia kwa ng'ombe kila heka 45000 na kunipandia ilikuwa 15000 kwa heka,palizi ilikuwa 50000 kwa heka na kiufupi nilitumia wastani wa laki 2 kwakila heka mpaka navuna nikaja kupata mavuno ya tani 5 na nusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…