Wito kwa Serikali yetu, Huu ni Udhalilishaji wa Bullying & Intimidation. Mbona Rais Samia Hadhalilishi? Tusiruhusu Udhalilishaji Huu Uendelee!

Mkuu,your appreciation for my politeness is a psychological blow to push me deep down to this issue.... I accept (maybe) and thanks.


You are absolutely right and lets settle this matter as per how we look into it. Thanks once more.
I appreciate your free reasonings 👊

thanks too 🐒
 
Naunga mkono hoja. Makonda anafanya na amekuwa akifanya udhalilishaji kila alipopita..!! Unfortunately, anapata baraka ya wanaomteuwa..!!
 
Makonda ni kiongozi mpuuzi mno. Siungi mkono uteuzi wake. Hata viongozi wengine wengi pia wamekuwa hawajielewi kabisa. Yaani lolote watakalofanya lazima camera iwepo. Kibaya zaidi utasikia "Mama ametutuma"... ina maana mama akisahau kuwatuma hawawezi kutumia madaraka waliyopewa kuamua?
 
Kwa maelezo yako hata Samia alimdhalilisha Bwana Ndugai basi.

Baada ya ile video akiponda ukopaji kusambaa,Ndugai alijitokeza na kuomba radhi hadharani halafu akaibuka muombwa radhi na kumshambulia muombaji publicly.

Hata wazo la kuachia ngazi lilimjia Ndugai baada ya kuchambwa hadharani tu.

Then 2024 Samia anajitokeza na kukubaliana na Ndugai kuwa serikali yake imekopa sana hapa nyuma.

Au hili utalisema siku Samia hayupo madarakani?
 
Kweli. RC kitaaluma ana uwezo mdogo sana.
 
Huu mfumo wa utawala wa vitisho uliletwa na Magufuli kiasi kwamba hata watoto wadogo hawakuupenda, rejea msiba wa kiongozi uliotokea ambapo watoto wa marehemu waligoma kushikwa mikono kutokana na baba yao alivyofanyiwa kwa kutumbuliwa hadharani na kiongozi wa juu kiasi akaugua presha na kufariki.
Hebu tujikumbushe tukio jingine la Morogoro sokoni ambapo kiongozi wa nchi anawauliza wafanyabiashara "nimtumbue nisimtumbue?" Wafanyabiashara wasiomjua mtumbuliwaji wanajibu " mtumbue" naye akamtumbua hapohapo yule mama mkurugenzi wa manispaa.
Huyu unayemtoa kama mfano alikuwa na mungu wake wa Tanzania huku yeye akijiita mungu wa Dar es Salaam!
Ni vigumu kuukomesha mfumo huu ambao umehalalishwa na viongozi wa kitaifa, na kutekelezwa na huyu mungu kama alivyozoezwa, na bahati mbaya haukuliona hilo.
 
Mimi Makonda nimemuelewa,
Jamaa angetoa sifa ya Barabara anazosimamia. Ni zile zenye tabia ipi. Yeye anasema Barabara zake ziko gazzeted, Sasa gazzeted lini hakuna anaejua.

Au ni kama vile yeye kakabidhiwa tu Barabara asizojijua?
 
Ila wabongo kiboko asee dah!

Leo hata wewe NJAA unasimama kwa ukali unamsema Magu?

Kweli mtu ukifa unakufa na yako yote. We si ulikuwa mmoja wa timu chawa pro wa kusifu na kuabudu kila kitu
Paskali huuma na kupuliza. Kamsifia sana jamaa huyu katika mada zake nyingi humu jamvini hata kufikia hatua kwamba anafaa kuwa Mkuu wa Nchi. Fikiria sasa ni Boss wa Mkoa tu. Je akipewa zaidi ya hapo mambo yatakuwaje?
 
Uwasilishaji wa mada yoyote ile kutoka kwa fanani kwenda kwa hadhira huwa ina sehemu muhimu kubwa tatu. za kuzingatia
1. Utangulizi
2. Maudhui makuu au "body"
3. Hitimisho

Ni vyema muwasilishaji angepewa muda wa kutosha ili aweze kumalizia kufanya wasilisho lake lote, kabla ya kuanza kumkatisha katisha na kumkosoa kwa kila sentensi ambayo aliyokuwa akiitoa.

Mwenye kikao ni kama alikuwa amemkamia, ama alikuwa anatuma ujumbe fulani kwa wasaidizi wake. Kikao chenye uwasilishaji wa ajenda mbalimbali ikiwemo ile ya TARURA, naamini kuna baadhi ya ufafanuzi angaliweza kuupata baada ya muwasilishaji kumaliza kuwasilisha kile chote ambacho alikiandaa.
 
Mimi Makonda nimemuelewa,
Jamaa angetoa sifa ya Barabara anazosimamia. Ni zile zenye tabia ipi. Yeye anasema Barabara zake ziko gazzeted, Sasa gazzeted lini hakuna anaejua.

Au ni kama vile yeye kakabidhiwa tu Barabara asizojijua?
Hapa nadhani kinachojadiliwa ni mwenendo wa utendaji kazi, zipo kanuni za utendaji kazi ambao haufanywi kimahakama. Mtindo huu si mtindo rasmi dhidi ya waajiriwa serikalini, ni mtindo wa kisiasa za kutafuta sifa tu.
 
Hapa nadhani kinachojadiliwa ni mwenendo wa utendaji kazi, zipo kanuni za utendaji kazi ambao haufanywi kimahakama. Mtindo huu si mtindo rasmi dhidi ya waajiriwa serikalini, ni mtindo wa kisiasa za kutafuta sifa tu.
Mtu unasema unasimamia Barabara,
Tuelezee Barabara unazosimamia wewe zina sifa zipi. Ili tunapoamua kukuuliza maswali tujue kabisa hizi zinakuhusu na hizi hazikuhusu.

Ukituambia wewe Barabara zako ziko gazzeted sisi hatujaona hilo gazette. Unless utuambie kua hata wewe mwenyewe hujui unasimamia Barabara gani.

Tuambie hata upana labda, au zenye changarawe au hata zinazopita mitaani. La sivyo tunaweza kukuuliza ukawa unatujibu kua haziko chini yako tukakosa majibu tarajiwa.

Na bahati mbaya au nzuri Makonda alimpa muongozo kabisa kwamba aelezee kazi zake katika muktadha upi. Lakini still bado jamaa hakumuelewa.

Watendaji wengi wa Serikali wanafanya kazi "Bora liende" sana.
 
Double standards juzi ukuona video ya ‘Jerry Slaa’ na ‘Alex Msama’ au? Ingekuwa Makonda ndio kafanya vile mngekuwa na kusema.

Sio muda mrefu kulikuwa ya video ya Mtatiro na mfanyakazi wa SHUWASA akimtolea lugha mbofu mbofu, matter of fact karibu kila kiongozi anafanya ivyo pale ambapo maelezo ya watendaji ayajanyooka. Ila Makonda tu ndio anaonekana.
 
Samia ndiyo nani? Kiongozi weak and ignorant ndiyo unaowataka Tanzania hii? Hatuhitaji viongozi waoga waoga wasio na uthubutu! Lazima watu wawajibike
 
Paschal umefanya kazi Serikalini na unajua jinsi watumishi wanavyofanya kazi kimazoea na kufunika uzembe.

Makonda yuko sahihi kwa staili hii ya kukabili uzembe kazini, unachofanya hapa ni kujaribu kulinda legacy ya uzembe wa kitaasisi, kitu ambacho CCM itakifanya muda si mrefu.

Acha Makonda awanyooshe! Ndicho tunachotaka.
 
Ndugai for President

Vote Yes[✓]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…