Uchaguzi 2020 Wito: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na timu yake yote wajiuzulu

Hadi hapa huu uchaguzi ni invalid, tunarudia, hatukubali matokeo yoyote yale, kura zimekamatwa kibao je ambazo zishapitishwa ni ngapi? na majimbo mangapi?

Huu uchaguzi tushau-cancel tunarudia mwingine tukiwa na tume huru sio hii ya sasa hivi.
 
Hajapiga, haya ni maajabu, mimi sijawahi kusikia kwamba Mgombea Uraisi hajipigii kura halafu anawaambia wengine wajitokeze kumpigia kura? Huyu jamaa tundu kichwani hazimtoshi aisee, ...
Nyie mnaosema lissu hajapiga kura mna uhakika?.... kwahiyo hapo alikuwa anatalii ety??
 
Kila uchaguzi mambo yaleyale yanajirudia kila upande(state na opposition)hawachukui hatua.

Hapa wakulaumiwa ni wote,sio tume ya uchaguzi tu
Opposition hawachukui hatua zipi ?

Sisi opposition tumefanya mengi sana na tumeumizwa sana.

Wananchi mmeshindwa kumalizia tunapoishia uchaguzi huu bila wakala kituoni ni disaster nyinyi mmepiga kura mawakala wetu wanaondolewa vituoni na polisi hamchukui hatua yoyote sisi mnataka tuwafanyie nini kingine ?
 
Hiyo si solution dhidi ya hawa wahuni wa ccm. Hawajali maslahi ya Nchi hawa zaidi ya maslahi yao binafsi.

Maccm yanajua fika hayapendwi na yamechokwa na asilimia kubwa ya Watanzania ndiyo sababu yanahofia chaguzi huru na za haki kwa kujua kwamba ndiyo itakuwa kaburi lao

Baada ya huu uhuni wao mimi naona vikwazo vya kiuchumi labda vinaweza kutusaidia ili kuwatia adabu hawa wahuni wasiwe na jinsi zaidi ya kukubali uwepo wa katiba mpya na tume huru ya Uchaguzi ili kuhakikisha chaguzi zetu ni HURU na za HAKI.

Kama Nchi nyingi za Afrika wapinzani wanashinda na kuingia madarakani bila machafuko yoyote sioni kwanini hilo lishindikane kwenye Nchi yetu. Tanzania bila maccm INAWEZEKANA KABISA.
 
So solution ni kushiriki chaguzi za maigizo?

Haya sawa.

Kila siku mkipigwa kwenye sanduku la kura mtaendelea kulialia kama mnavyolia sasa hivi.

Endeleeni kuwapa uhalali CCM.
 
Weka ushahidi hapa Tundu Lisu akipiga kura kama ilivyo kawaida kwa Wagombea wote Duniani, weka ushahidi tu, its eaaasy , ...

Kwa hiyo hujaona ushahidi niliokuwekea?
Au hujaona kutoka kwa wengine walioku quote?


Haya hizo picha ni za nani, akiwa anafanya nini na wapi!?
Naona ulivyopandwa na hasira, hadi kukukaba kooni!
Umefeli na hako kapropaganda kako uchwara!
Haya anzisha propaganda nyingine kuwa mgombea Urais ataendaje kupiga kura akiwa kavaa jinsi na kofia basi!
 

Zito na Tundu walishazunguka duniani kuomba pia sijui walifanikiwa kwa asilimia ngapi

Ila kama wewe pamoja na wazazi wako, shangazi zako, wajomba zako, bibi zako, babu zako, ndugu zako wote wako nje ya Tanzania kazia hapohapo wawekewe vikwazo maana hutafikwa na msiba
 
Solution kwa sasa baada ya huu uhuni ni kuwepo kwa Serikali ya maridhano au mpito ili kupata Katiba mpya na tume huru ya Uchaguzi ili uchaguzi urudiwe haraka iwezekanavyo ndani ya miezi sita au 12. Haiwezekani basi vikwazo vya kiuchumi vinatuhusu.
So solution ni kushiriki chaguzi za maigizo?

Haya sawa.

Kila siku mkipigwa kwenye sanduku la kura mtaendelea kulialia kama mnavyolia sasa hivi.

Endeleeni kuwapa uhalali CCM.
 
Hebu acha kuwahusisha watu wangu taahira wewe! Hunijui sikujui!
 
Tiba ya hayo yote ni katiba mpya.opposition,wananchi Na serikali hawajafanya vya kutosha kudai/kusaidia upatikanaji wake

Nani mwenye copyright ya katiba?
 
Solution kwa sasa baada ya huu uhuni ni kuwepo kwa Serikali ya maridhano au mpito ili kupata Katiba mpya na tume huru ya Uchaguzi ili uchaguzi urudiwe haraka iwezekanavyo ndani ya miezi sita au 12. Haiwezekani basi vikwazo vya kiuchumi vinatuhusu.
Endelea kuota!

2025 mtashiriki tena uchaguzi mkuu katika mazingira haya haya halafu mkipigwa kwenye sanduku la kura, mtarudia vilio vilevile.
 
Hawa wapinzani wa Tanzania hawaambiliki!

Ni sikio la kufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…