Wawiwe kuona haki i kitokewa kila mahala kivitendo.
Mwenyezi Mungu anapendezwa na utolewaji wa haki na sio dhuruma, ghiliba, ufisadi, wizi udhalimu, mauaji, uonevu n.k.
Na Mungu haishii kuchukizwa tu lakini huadhibu pia na adhabu yake huwa ni kubwa kuliko ya mwanadamu kama mwenyewe alivyo mkubwa sana kuliko mwanadamu bila kujali chochote yakiwepo madaraka.
Mfano utakuta adhabu ya laana inaenda kula vizazi vya mtu cha kwanza hadi cha 4 hata cha 7.
Kwani Imeandikwa; “ nawapatiliza wana uovu wa baba zao kizazi cha kwanza hata cha nne”
Bali nawarehemu maelfu kwa maelfu ya wale wanipendao kizazi cha kwanza haya cha nne.
Na maana ya kumpenda Mungu ni kuishi kwa kufuata na kuzingatia alichoagiza.
Mfano alisema acha mabaya uache, Fanya mema na haki ufanye ktk kufanya kazi kwako na kuishi kwako hicho ndicho kipimo cha kumpenda Mungu.
Imeandikwa; “ mkinipenda mtazishika amri zangu nami nitakuwa pamoja nanyi siku zote.