Wizara husika imchunguze Pastor Dominick (kiboko ya wachawi)

Hujalazimishwa kuamini.

Waache wanaomuamini waendelee kumuamini.

Kila mmoja ana imani yake.
 
ikooo fb
 

Attachments

  • Screenshot_20240704-133819_Lite.jpg
    457 KB · Views: 8
Pastor Dominic Nabii Kiboko ya Wachawi anahudumia Wapiga kura wetu.

Mwache afanye kazi yake.
 
😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Ndugu umepanic
Huo ndiyo ukweli ukienda kwa mwamposa na manabii wengine wengi asilimia kubwa ya waumini ni waisilamu naweza kusema karibu nusu ni waislamu
Umewajuaje kama ni waislamu? na data zako umekusanya vipi? kwa kuangalia tu ama kitu gani?

Naomba unijibu hapo halafu tutaendelea
 
Kodi kubwa ni muhimu ,wanapata pesa sana ,Mbaya zaidi mpaka kina lokole wanampa airtime
Yule jamaa anapiga pesa sana kupitia Hisia na psycholojia ya watu wenye matatizo..

Kiukweli kama huna tatizo uyawadharau wanaoenda kwake.

Jamii imejaa shida nyingi na matatozo kibao ikiwemo
Nuksi, mabalaa, mikosi, ugomvi, wizi, uchawi, ndoa, watoto kudeviate kitabia, magonjwa na umaskini wa kipato.

Sasa jamii hii imekosa tumaini kabisa na hawana kimbilio. Sasa wanapoona kuna mtu madhabahuni ambaye anawasikiliza kwa matumaini ya Kuwapeleka kw Mwenyezi Mungu basi jamii hii haijiulizi mara mbili.

Mkutano mmoja wa Pastor Dominic unakusanya watu zaidi ya elfu tano.

Ana chaji sadaka minimum ni elfu mbili kwa kila kichwa. Achilia mbali kina anayehudhuria Kanisani lazima awe na kitambaa cha elfu moja au maji.

Na ukitazama pale watu walivyo na furaha na matumaini ni ngumu sana kuwaondoa.
 
Yule jamaa ni noma.

Ni mjanja sana. Hata zile shuhuda nilizifatilia kwa muda mrefu nikagundua watu ni wale wale.

Anabadilisha maeneo tu. Anasema huyu wa Songea, kesho anasema Kwao Tanga.

Na muundo wa matukio na mtiririko wake unafanana.

Usipokuwa mjanja hutagundua kama una akili za kimboga mboga.
 
Umewajuaje kama ni waislamu? na data zako umekusanya vipi? kwa kuangalia tu ama kitu gani?

Naomba unijibu hapo halafu tutaendelea
Tumia mwezi mmoja kusikiliza shuhuda za mwamposa utajua nnachoongea

Ex wangu alikuwa muumini wa mwamposa kitu pekee tulichokuwa tunasikiliza nyumbani ni redio ya mahubiri ya mwamposa ilibidi nimnunulie redio ndogo kuepusha mizozo

Majina ya mashuhuda ni ushahidi tosha
Ex alikuwa muislamu na mashoga zake wengi ni waislamu kwa mwamposa kwa wiki mara mbili karibu laki mbili ilikuwa inaisha kila wiki
Mafuta ya gari
Mafuta ya mwamposa
Maji
Na sadaka
 
Hapo ndo nilipopataka ... wajinga ndo waliwao, the fact kwamba ibada zake zinabebwa na ushuhuda wa watu kwenye radio ni dalili tosha ya kuwa hao mashuhuda ni wakupangwa. Tena mnapewa moyo kwa waigizaji kujiita majina ya kiislamu na nyie mnajaa mazima. Mimi nataka nione jamii kweli ya kiislamu tunayoijua huku mtaani iliyobadilika ikawa wafuasi wa nabii yoyote wala sio huyo Mwamposa tu, awe yoyote mnaemuita nyie nabii.

Kuhusu ex wako kuwa alikuwa ni muislamu kama ni kweli usemalo I can guarantee that huyo ex wako hajui hata basics za uislamu, na hajawahi kuuishi huo Uislamu! so sidhani kama ni reference sahihi, otherwise prove me wrong on this.

Si mnasema wafuasi wengi wa mwamposa ni waislamu basi mpelekeni huyo Mwamposa Zanzibar, Tanga au Lindi halafu tuone anavyokubalika.

Muislamu yoyote anaejua tu misingi ya dini yake wala asiwe shekhe basi hawezi kuwa fooled na watu kama hao kina mwamposa.
 
Yani kwa reason yako wewe hata ukiangalia movie utakuwa unaamini ni kweli.

Mufti kaenda kwake au yeye ndo kaenda kwa Mufti? ... Uislamu sio rangi, ikiwa unaweza kumtambua muislamu kanisani mwenu then ni wazi alitaka umtambue hivo, basi haitoshi kukufungua akili kwanini ametaka umtambue kwa uislamu wake?

Eid kachinja na kupeleka ng'ombe bakwata, nguvu yote hiyo ya nini ikiwa anachokihubiri ni kweli?

Hapo mnapigwa nyinyi wakristo na wanawataget wale wanaojiita waislamu lakini hawajui chochote kuhusu dini yao.

Amkeniiiiii
 
Fahamu kwamba asilimia kubwa kabisa ya wafuasi wa manabii wanaenda pale kwa sababu fulani fulani tu lakini kiasili hawajaacha kabisa dini zao za asili wako pale kupata majibu ya changamoto zinazowakabili wakiamini pale ni short cut
Lakini kama ukiweza kuwaambia wajicomit waachane na dini zao kabisa wengi hawatokubali
Fahamu kwamba hata ukristo wa kweli hauungi mkono uwepo wa hizi huduma za kinabii kwa kuwa wengi wao ni matapeli tu
Na mamlaka zimebariki aina hii ya utapeli na wananchi wa dini zote wanatapeliwa kutia ndani waislamu na waislamu wanaamini ule ni ukristo bila kujua kwamba ni ukristo uliokengeuka
Huwezi ukaulaumu ukristo au ukatuhusisha sisi wakristo na mwamposa mmoja au nabii mwingine yeyote ambaye ameangalia kwamba sheria za nchi zinamruhusu na akaamua kufanya anachokifanya hiyo haihusiani kabisa na ukristo
Ukristo ni taasisi na unafanya kazi kama taasisi na siyo huduma ya mtu mmoja

Kwenye uislamu kuna mashekhe wanafuga majini na wengine ni waganga wa kienyeji
Hatuwezi kuulink uislamu na watu wa aina hiyo kwa sababu tunajua hao ni watu tu wamekengeuka wanatumia vitabu vya dini negative lakini uislamu hausupport mambo hayo
Kwa hiyo relax bro wale ni matapeli tu siyo ukristo ule lakini waislamu ni wahanga zaidi ya huo utapeli
 
Tanzania ukitaka kupiga fedha jifanye wewe ni bingwa wa mambo ya uchawi na uganga. Ndicho wanachofanya wachungaji na manabii wa sasa. Ila hawa si ndiyo CCM inawapenda kwa sababu inawatumia?
 
Huwa namsikiliza nabaki nashangaa serikali kwanini haimchukulii hatua
 
Wewe pia umeangalia movie ukaamini waendao ni wakristo tupu?

Hata moh'd ni type hizi tofauti TU zama hizi Kuna mitandao na wapiga spana wengi

Angeibuka zama hizi upinzani ungekua mkubwa sana kwa mahubiri yake na matendo yake na ningekua wakwanza kuleta Uzi kama huu( tafakari na fikiria mafundisho yake mbalimbali na matendo yake kutoka kwenye hadithi sahihi utakubaliana nami )

Narudia Tena huu Uzi ni kwa ajili ya Kiboko ya wachawi na kuwashtua watu dhidi ya utapeli wake sio kuhusu nani anaenda nani haendi,tukitaka mjadala mwengine wa kuhusu kina nani wanapigwa zaidi ,tufungue Uzi mwengine ntakua tayari kwa mjadala.
 
Angeibuka zama hizi upinzani ungekua mkubwa sana kwa mahubiri yake na matendo yake na ningekua wakwanza kuleta Uzi kama huu( tafakari na fikiria mafundisho yake mbalimbali na matendo yake kutoka kwenye hadithi sahihi utakubaliana nami )
Tatizo ni pale mnapotaka kulazimisha ujinga wenu (kumradhi, hapa nimemaanisha ujinga kwa maana ya kutokulielewa jambo unaloliongelea) kuwa ndio ukweli wa mambo ulivyo.

Vipi unaweza kumshutumu Mtume Muhammad (SAW) kwa mafundisho yake ikiwa yeye ndo aliyefikishia watu Quran iliyoyajaa scientifc evidences? tena evidences nyingi tu ndo zinatambuliwa sasa na science yetu (within our century), e.g. Isostasy knowledge, embryology knowledge, ring composition within quran etc. Yote haya yapo kwenye Quran since it was revealed 14 centuries ago and the human is only able to understand and appreciate this knowledge in our century, bado unamuona mtume ndo mwenye shida na sio wewe?

Ukitaka kuongelea upande mwengine kutoka kwako, jielimishe kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…