Wizara ya Elimu huku hali ni mbaya! Watoto mnawatengenezea Ulemavu

Mnaolalamika tafuteni pesa watoto wenu wasome shule mnazozitaka...
Serikal inawasomeshea watoto wenu bure, kazi yenu ni kuhamasisha watoto wapende shule...
Wote mnaolalamika ndio nyie mlifeli shule na mnaelekea kufeli kimaisha
Nina wasiwasi na uelewa wako. Kwa nini michango iwe kipindi hiki cha mama tu wakati wameongeza hata kiasi cha pesa zinazopelekwa mashuleni kwa ajili ya kuendesha dhule hixo na wakati wa JPM michango ya aina hii haikuwepo?
 
Watoto wadogo sana ila wanabeba mabegi makubwa mno yaani unajiuliza Elimu ya wakati huu ambapo tupo kwenye modern world imekumbwa na nini? Miaka ile zamani kabisa shule ya msingi kwanza kulikuwa na ratiba inayoeleweka kabisa yaani Leo masomo matatu au manne na daftari unabeba hizo hizo. Nazungumzia 1993 wakati walimu wa Sasa wengine walikuwa wanasoma na sidhani kama wamesahau umuhimu wa ratiba!

Vipindi kwa siku vilikuwa vinaisha saa nane hivi mnarudi nyumbani mpaka kesho yake ila Sasa mtoto anaingia shule na begi kuuubwa na lazima masomo yote yasomwe kwa siku moja hiyohiyo yaani anaanza vipindi saa moja kamili anamaliza saa kumi na moja na nusu jioni akitoka hapo akapambane na bajaji anakuja kufika nyumbani saa 1 kasoro jioni amechoka hana hali.
Shida ni nini?
Wizara ya Elimu na TAMISEMI wanafahamu hii hali?
Hawaoni kuwa tunatengeneza Taifa la vijana wenye stress?
Natamani Dr Msonde alione hili nankulizungumzia
 
Michango imekuwepo tangu Enzi na Enzi na halijawahi kutoweka aise fuatilia
 
Ni kweli kabisa.

Watoto wanaumia.

Alafu na sisi Wazazi hatuna huruma hasa ktk vyombo vya usafiri

Mtoto kabeba begi kubwaa lkn hata kumsaidia kumpokea kidogo hakuna.

Mtoto anasimama na begi na foleni haiendi.
Na hata siti ikipatikana hana haki ya kukaa
 
Mnaolalamika tafuteni pesa watoto wenu wasome shule mnazozitaka...
Serikal inawasomeshea watoto wenu bure, kazi yenu ni kuhamasisha watoto wapende shule...
Wote mnaolalamika ndio nyie mlifeli shule na mnaelekea kufeli kimaisha
Sawa.
 
Swala la kula ni mzazi unatakiwa ujue jinsi mwanao atavyokula, haiwezekani usomeshewe bure afu na chakula upewe bure
Nini maana ya bure? Mbona pedi wanawapa bure..?
 
Sema wazazi wa Dar mnazingua sana. Hao watoto wenyewe mnaowasema school bus inamchukua getini inamshusha kwenye gate la shuleni. Hilo begi analibeba kutoka kwenye geti la shule mpaka darsani maana huku nyumbani akirudi kuna dada wa kazi anayekuja kumpokea kwenye school bus atambebea begi.

Acheni kuwa maronya ronya
 
Mnaolalamika tafuteni pesa watoto wenu wasome shule mnazozitaka...
Serikal inawasomeshea watoto wenu bure, kazi yenu ni kuhamasisha watoto wapende shule...
Wote mnaolalamika ndio nyie mlifeli shule na mnaelekea kufeli kimaisha
Aisee ficha basi hata kidogo kaujinga ulicho nacho. Tatizo la watoto kubebeshwa madaftari mengi lipo zaidi shule binafsi kuliko hata za umma.
 
Nasikia shule ya sekondari Kantalamba ilikuwa bora usahau ada kuliko usahau jembe.
Watoto wadogo sana ila wanabeba mabegi makubwa mno yaani unajiuliza Elimu ya wakati huu ambapo tupo kwenye modern world imekumbwa na nini? Miaka ile zamani kabisa shule ya msingi kwanza kulikuwa na ratiba inayoeleweka kabisa yaani Leo masomo matatu au manne na daftari unabeba hizo hizo. Nazungumzia 1993 wakati walimu wa Sasa wengine walikuwa wanasoma na sidhani kama wamesahau umuhimu wa ratiba!

Vipindi kwa siku vilikuwa vinaisha saa nane hivi mnarudi nyumbani mpaka kesho yake ila Sasa mtoto anaingia shule na begi kuuubwa na lazima masomo yote yasomwe kwa siku moja hiyohiyo yaani anaanza vipindi saa moja kamili anamaliza saa kumi na moja na nusu jioni akitoka hapo akapambane na bajaji anakuja kufika nyumbani saa 1 kasoro jioni amechoka hana hali.
Shida ni nini?
Wizara ya Elimu na TAMISEMI wanafahamu hii hali?
Hawaoni kuwa tunatengeneza Taifa la vijana wenye stress?
Natamani Dr Msonde alione hili nankulizungumzia
Nazungumza na mwanangu hapa sasa hv, anasoma shule binafsi, anasema walimu hawafuati ratiba, maana unakuta somo ambalo halipo leo mwalimu wake ndio anakuja darasani na anasema usipokuwa na daftari lake unapigwa. Kwa kweli wizara ya elimu iziangalie hizi shule binafsi. Mwanangu mpaka anapinda mgongo. Mtoto wa miaka 9 anabeba counter books 12, vitabu 6 n.k. yaani mpaka begi anapata tabu kulinyanyua
 
Kwakweli ni hatari kwa afya ya mtoto, kuna mtoto amepata tatizo la kuchomoka mkono eneo la bega kwasababu ya mzigo wa bag la vitabu na madaftari. Kitoto chenyewe kidogo.
 
Nazungumza na mwanangu hapa sasa hv, anasoma shule binafsi, anasema walimu hawafuati ratiba, maana unakuta somo ambalo halipo leo mwalimu wake ndio anakuja darasani na anasema usipokuwa na daftari lake unapigwa. Kwa kweli wizara ya elimu iziangalie hizi shule binafsi. Mwanangu mpaka anapinda mgongo. Mtoto wa miaka 9 anabeba counter books 12, vitabu 6 n.k. yaani mpaka begi anapata tabu kulinyanyua
Wewe inaonekana huna akili... Hoja zako za kitoto sana
 
Sweta??????
Punguza chuki!
Watoto siku hizi wamekuwa kama PUNDA kwanini Waalimu wanawabebesha watoto mabegi mazito na makubwa kuliko hata kilo zao??

Je hakuna ratiba maalumu ya masomo?

Hili tatizo lipo kwa ngazi zote Msingi mpaka Sekondari.

Vitu vinavyobebwa ni kama ifuatavyo
1_ Sweta
2_Chupa la maji
3_Vitabu si chini ya nane
4_Madaftari kumi na kuendelea
5_Kompasi/Mkebe
6_Rangi boksi zima + Peni + Penseli
Na vitu vingine

Ukipiga mahesabu hapo si chini ya kilo 8 mtoto anabeba mgongoni na huyo mtoto:
  • Adandie daladala.
  • Huyo huyo atembee umbali mrefu.
  • Huyo huyo ashinde bila kula huko shule.
  • Huyo huyo awahi kuamka asubuhi (Zingatia mzigo anaozunguka nao mgongoni siku nzima)

Niulize swali: Hivi haiwezekani kukajengwa cabinets za kuhifadhi madaftari ya darasani huko huko shule?

Maswala ya Homework vitengenezwe vitabu/Daftari maalumu bila kumlazimu mtoto kutembea na midaftari mingi?

Hivi hakuna sophisticated mechanism itakayowaokoa hawa watoto?

Watoto wanatoka vibiongo wanaumwa migongo na kuchoka mno.

Ila sishangai maana hata waalimu nao wanamapochi makubwa wamejaza Kashata, ubuyu na Kababu hawawezi kuwa na huruma.

punda_ideology
 
Back
Top Bottom