Wizara ya Elimu huku hali ni mbaya! Watoto mnawatengenezea Ulemavu

Kwakweli ni hatari kwa afya ya mtoto, kuna mtoto amepata tatizo la kuchomoka mkono eneo la bega kwasababu ya mzigo wa bag la vitabu na madaftari. Kitoto chenyewe kidogo.
Aiseee... hii hali inaumiza watoto wengi sana...
 
Umesahau michango kila siku na cha ajabu zaidi juzi darasa la saba Dar wamefanya Mock mkoa lakini tumechangishwa wazazi kugharimia mock hiyo mfano mzuri shule ya msingi Kizinga Mbagala wilaya ya Temeke. Wamepata mbinu mpya wanawaita wazazi wanawaeleza sababu kibao za kuhalalisha hii michango yao. Tumemjulisha Afisa Elimu mkoa kuhusu kadhia hii hakuna jibu alilotoa. Na lengo lao tumelifahamu kumuharibia mama yetu tu. Maana kiasi cha pesa kinachopelekwa mashuleni ni kilekile tena sasa hivi kuna nyongeza kidogo lakini michango kila siku. Kwanini enzi za JPM kiasi hiki kiliwezekana leo kimeongezeka kishindikane. Prof Mkenda na Waziri wa Tamisemi liangalieni hili.
Unalalama kuchangia elimu ya mwanao
Usifate siasa elimu Ni pana kuna Mambo mengi haiwezi kutolewa bure
Wenzako wanalipia mamilion
We unachangia uji unalalama tu
 
Nazungumza na mwanangu hapa sasa hv, anasoma shule binafsi, anasema walimu hawafuati ratiba, maana unakuta somo ambalo halipo leo mwalimu wake ndio anakuja darasani na anasema usipokuwa na daftari lake unapigwa. Kwa kweli wizara ya elimu iziangalie hizi shule binafsi. Mwanangu mpaka anapinda mgongo. Mtoto wa miaka 9 anabeba counter books 12, vitabu 6 n.k. yaani mpaka begi anapata tabu kulinyanyua
Sio binafsi tu Kuna Ndugu yangu mwanae anasoma shule ya serikali tena ni English medium ipo mkoa mmoja nyanda za juu kusini hali ni hiyo hiyo

Hawafuati ratiba kabisa yaani wanasoma masomo yote kila siku.
Hakuna muda wa kujisomea maana wanakaa shuleni tangu saa moja asbuhi hadi 11:30 jioni mtoto anarudi nyumbani kachoka kama alikuwa vitani
 
Ku
Watoto siku hizi wamekuwa kama PUNDA kwanini Waalimu wanawabebesha watoto mabegi mazito na makubwa kuliko hata kilo zao??

Je hakuna ratiba maalumu ya masomo?

Hili tatizo lipo kwa ngazi zote Msingi mpaka Sekondari.

Vitu vinavyobebwa ni kama ifuatavyo
1_ Sweta
2_Chupa la maji
3_Vitabu si chini ya nane
4_Madaftari kumi na kuendelea
5_Kompasi/Mkebe
6_Rangi boksi zima + Peni + Penseli
Na vitu vingine

Ukipiga mahesabu hapo si chini ya kilo 8 mtoto anabeba mgongoni na huyo mtoto:
  • Adandie daladala.
  • Huyo huyo atembee umbali mrefu.
  • Huyo huyo ashinde bila kula huko shule.
  • Huyo huyo awahi kuamka asubuhi (Zingatia mzigo anaozunguka nao mgongoni siku nzima)

Niulize swali: Hivi haiwezekani kukajengwa cabinets za kuhifadhi madaftari ya darasani huko huko shule?

Maswala ya Homework vitengenezwe vitabu/Daftari maalumu bila kumlazimu mtoto kutembea na midaftari mingi?

Hivi hakuna sophisticated mechanism itakayowaokoa hawa watoto?

Watoto wanatoka vibiongo wanaumwa migongo na kuchoka mno.

Ila sishangai maana hata waalimu nao wanamapochi makubwa wamejaza Kashata, ubuyu na Kababu hawawezi kuwa na huruma.

punda_ideology
Kuwa mpole
 
Sema wazazi wa Dar mnazingua sana. Hao watoto wenyewe mnaowasema school bus inamchukua getini inamshusha kwenye gate la shuleni. Hilo begi analibeba kutoka kwenye geti la shule mpaka darsani maana huku nyumbani akirudi kuna dada wa kazi anayekuja kumpokea kwenye school bus atambebea begi.

Acheni kuwa maronya ronya
Hapo umekaa kwa shemeji yako
 
Watoto siku hizi wamekuwa kama PUNDA kwanini Waalimu wanawabebesha watoto mabegi mazito na makubwa kuliko hata kilo zao??

Je hakuna ratiba maalumu ya masomo?

Hili tatizo lipo kwa ngazi zote Msingi mpaka Sekondari.

Vitu vinavyobebwa ni kama ifuatavyo
1_ Sweta
2_Chupa la maji
3_Vitabu si chini ya nane
4_Madaftari kumi na kuendelea
5_Kompasi/Mkebe
6_Rangi boksi zima + Peni + Penseli
Na vitu vingine

Ukipiga mahesabu hapo si chini ya kilo 8 mtoto anabeba mgongoni na huyo mtoto:
  • Adandie daladala.
  • Huyo huyo atembee umbali mrefu.
  • Huyo huyo ashinde bila kula huko shule.
  • Huyo huyo awahi kuamka asubuhi (Zingatia mzigo anaozunguka nao mgongoni siku nzima)

Niulize swali: Hivi haiwezekani kukajengwa cabinets za kuhifadhi madaftari ya darasani huko huko shule?

Maswala ya Homework vitengenezwe vitabu/Daftari maalumu bila kumlazimu mtoto kutembea na midaftari mingi?

Hivi hakuna sophisticated mechanism itakayowaokoa hawa watoto?

Watoto wanatoka vibiongo wanaumwa migongo na kuchoka mno.

Ila sishangai maana hata waalimu nao wanamapochi makubwa wamejaza Kashata, ubuyu na Kababu hawawezi kuwa na huruma.

punda_ideology
Labda kama unasemea Dar , kwingineko Tz nzima wanafunzi hawapandi Daladala kama wapo hawafiki hata 200 kwa nchi nzima.Watoto wanasoma bweni walioday wanasoma shule zilizokaribu na makwao.Dar shida ni umasikini.
 
Mzazi mpeleke mwanao shule iliyo karibu na makazi yenu.....otherwise lipia school bus
 
hili haliwezi Kuisha Kaka
labda wao Wizara ya Elimu kila Mtoto wao aguswe au labda wanamiliki hizo Shule au wana Maslahi.
Kwa kweli ni hatari ya Kuumwa Back pain,Disc nk!
Wizara wanatakiwa Kutoa Muongozo kwa hili
 
Asilimia kubwa ya wafanya Maamuzi wengi wanasomesha wtt wao shule za Nje ya Nchi
 
Labda kama unasemea Dar , kwingineko Tz nzima wanafunzi hawapandi Daladala kama wapo hawafiki hata 200 kwa nchi nzima.Watoto wanasoma bweni walioday wanasoma shule zilizokaribu na makwao.Dar shida ni umasikini.
Sio wote wanaosoma shule karibu na Makwao hata hao wa Mkoani.

Kutokana na uchache wa Shule inalazimika mtt kutembea umbali mrefu kufata huduma ya shule. Lipo wazi
 
Back
Top Bottom