Wizara ya Elimu huku hali ni mbaya! Watoto mnawatengenezea Ulemavu

Sio kila mwanaume aendaye dukani hununua wengine hukopa ili mradi kutimize majukumu.
Hata kama ni wakukodi.
Tuombe yatimie maana ni jambo jema.
Nawaza pia Maabara za hizo kazi au fani stadi.. je tumewaza kuhusu hilo?
 
Nimekuelewa.

Kuhusu hela iwe miambili au mia moja. Au miatano sio tatizo. Tatizo ni kwamba wanashindwa nini kujumuisha hizo hela ktk Ada? Kama ni shule ya serikali kwanini Isiingizwe ktk bajeti huko Tamisemi walimu wapewe posho za muda wa ziada?

Ok turudi kwenye hoja nyingine, nimeona unapenda elimu ya kukariri ili mtu afaulu mitihani. Na sio uelewa.

Kama mwanafunzi ameelewa vzr haina haja ya kumchapa mitihani ya mara kwa mara!

Je mtaalaa wa Cambridge wanahuo utaratibu?
 
Sahiv kuna kipindupindu mtt asipobeba maji ni hatari sana. Ingawa naskia walimu wanadoea maji na juice za wanafunzi
 
Shule ya sekondari St Francis Girls' Mbeya tuna huduma za cabinet za kuhifadhia kila kitu cha mwanafunzi ..lakini pia ni hostel..karibu sana..
Safi sana... nimekaribia
 
Mkuu kumbuka hii ni Tanzania sio Uingereza.
Ni kweli tunahitaji mabadiliko lakini kwa hali yetu ilivyo kwa sasa hatuna budi kuendana nayo.

Mtoto wa darasa la saba umfundishe hesabu leo aelewe, utegemee aje kufanya mtihani mwezi wa 9 bila kumfanyisha mazoezi ya hicho ulichomfundisha???
Nimeshangaa sana uliposema ati akielewa inatosha!! Ndgu wewe ulivyokua shule ulikua hujisomei au ulikua unasoma mambo mapya tu na ukishaelewa imeisha hiyo hupitii tena hadi siku ya pepa???

Kwani mkuu wewe uelewa wa mwanafunzi unaupimaje??
 
Shule ya sekondari St Francis Girls' Mbeya tuna huduma za cabinet za kuhifadhia kila kitu cha mwanafunzi ..lakini pia ni hostel..karibu sana..
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tanzania hii hakuna hatakaijali mkuu.
 
Nimeuliza swali jepesi hapo juu kuhusu mtaala wa Cambridge je wana huo utaratibu wa pepa za mara kwa mara?

Pia imeshindikana nini kutengeneza cabinets maalumu za wanafunzi watunzie vitu vyao huko shuleni na warudi na daftari la assignments/homeworks tu? Kwanini umbebeshe mtoto mdg mzigo wa kilo 20 bila sababu za msingi..?
 
Nimwalimu peke yake analaumiwa au namzazi?
Anayepewa lawama si MWALIMU bali ni WIZARA ya ELIMU. maana wao wameshindwa kutengeneza Policy or Guidelines za kuwaongoza WAKUU Wa SHULE kuhusu hii shida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…