Wizi wa catalytic converter kwenye magari 'Masega'

Hapo ndio umakini unapokosekana,yaani unawasha gari lako unaondoka nalo,hivyo vitu vyote huwezi kuvugundua hapohapo ili umuulize fundi kuwa kulikoni gari langu limekuwa hivi!nadhani kuna kitu mtoa mada hujaweka vizuri..
 
Hili ni tatizo la ku kopi text za makundi ya What's App na kuzileta hapa,ndo maana utaona mleta mada hana ufafanuzi mzuri wa namna huo unga unavyokuwa 'recycled' sababu naye kakopi na ku pesti.
Wewe ni Thomaso.. Wait and see
 
Mm wamenifanyia huu ujinga nataka kwenda kureport polisi
Kuna mawili
1.cat yako ilikufa,wakatumia short cut na kuitoa. Mafundi wengi wanafanya hivi.
2.Hilo usemalo.

Hayo madude used hayana bei kama hizo ni dili si wangeuza hio platinum badala ya kuuza cat nzima £50-100?!

Fursa hio watu waambieni wasiibe niwaletee hayo madude moja wanipe 100,000 tu.
 
Asante mkuu

Heee[emoji15] [emoji15] ngoja nichungulie sasa
 
Hapo ndio umakini unapokosekana,yaani unawasha gari lako unaondoka nalo,hivyo vitu vyote huwezi kuvugundua hapohapo ili umuulize fundi kuwa kulikoni gari langu limekuwa hivi!nadhani kuna kitu mtoa mada hujaweka vizuri..
Ni kweli kabisa...basi tu hajaeleza vizuri but mafundi wa kibongo ni washenzi hakuna mfano! Yaan anataka atajirikie kwenye kimkoko chako yaan!
 
Upo siriaz
 
Ukifata maneno ya wa bongo unaweza ukachizika
 
Mafundi kibongo siyo...ukigundua tatizo kwenye gari lako nenda msimamie urudi na gari nyumbni...kama huna muda ni bora ulipaki upeleke siku una nafasi..
Kuna uhuni niluona wanafanya siku moja nikasema sitamwachia fundi gari...kuna mzee alileta gari hapo gereji awekewe ball joints mpya akatoa hela ile kajipindua tu, mafundi wakafungua faster na kuzigonga na nyundo zikakaza then wakazirudishia..
 
Kuna biashara imeibuka siku hizi na imekuwa maarufu sana na imeshika kasi sana kwa hapa dar es salaam..

Pindi unapopeleka gari yako gereji au kumpatia fundi huwa wanamtindo wa kuiba catalic converter , masega au alimaarufu kama makinikia.
Mafundi wengi wamekuwa sio waaminifu na kugeuka waharibifu kabisaa..wa magari ya watu..

Najua wengi wenu mtakuwa hamjanielewa ni kwamba kwenye exhaust kuna sehem huwa kuna kuna na kama kibuyu au bomba kubwa zaidi ya sehem nyingine ndani yake huwa kunakuwa na kitu kama masega ya nyuki..huwa yanakuwa kama udongo hivi haya madini yanauzwa bei kubwa sana laki 2 tatu 4 mpaka laki 7 mafundi wanayauza..so wengi wamekuwa wanayabomoa nakuyauza..matokeo yake gari inakuwa na sauti mbaya then ulaji wa mafuta unaongezeka na performance ya gari inapotea kabisaa..hivyo wenye magari kuweni sana makini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…