Hatimaye adhabu aliyopewa Tundu Lissu imemalizika Jana.
Mgombea huyo anayeungwa mkono na mamilioni ya Watanzania leo ataendelea na Kampeni yake katika mikoa ya Dodoma katika maeneo ya Chamwino na Singida katika maeneo ya Ikungi na Manyoni.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa ni kichekesho Cha Dunia kutokana na upendeleo wa waziwazi kuibeba CCM na kuikandamiza Chadema.
Tume hiyo imekataa hata kupokea malalamiko ya Chadema dhidi ya Mgombea wa CCM kwa kukiuka Maadili ya Uchaguzi.
Lissu anatarajiwa kupata mapokezi ya kishindo kutokana na hamu kubwa ya wananchi kutaka kumsikiliza baada ya kudhulumiwa haki yake ya kufanya kampeni kwa siku 7 ili kulinda CCM.
-------- ------- -------
Yanayojiri muda huu saa 5 asubuhi
Wananchi ktk jimbo la Bahi kata ya Bahi mkoa wa Dodoma baada ya kusikia mhe Rais Tundu Lissu atapita maeneo hayo kuelekea Singinda wameamua kumsubiri barabarani tangia saa moja asubuhi ili angalau waone sura yake tu
Jimbo hili tume ya CCM ilimuengua mgombea UBUNGE wetu kwa SABABU za kijinga kabisa!!
View attachment 1595493