Mgombea wa Urais CHADEMA Tundu Lissu leo ataendelea na Kampeni zake katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Arusha na Kilimanjaro ngome Kuu za CHADEMA tangu mfumo wa vyama vingi uanze wanatarajiwa kufanya mapokezi ya kufuru kwa Mgombea huyo ambaye tathmini zote zinaonyesha atapata ushindi wa zaidi ya asilimia 60%.
Jimbo la Hai anakogombea Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ni moja ya sehemu atakazotua Tundu Lissu kumnadi Jemadari wa Siasa za Upinzani Tanzania.Ni wiki iliyopita tu Kamanda wa Polisi Hai bila aibu alimropokea Mbowe hadharani kwamba hatashinda ubunge jimboni humo.Wananchi wa Hai walisema Mungu amemuumbua OCD huyo akaropoka hadharani kilichokuwa kimepangwa nyuma ya Pazia.
Katika mkutano wa Hai CHADEMA inatarajiwa kumkaribisha Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Maalim Seif Sharrif Hamad ambaye atapanda Jukwaani kumnadi Mwenyekiti mwemzake ambao ni marafiki wakubwa katika siasa za Tanzania
Pia baada ya kutoka Hai mgombea huyo wa Urais atatua Moshi mjini Jimbo ambalo limekuwa Upinzani kwa miaka 25 sasa
Picha 2 za Mwanzo ni Lissu na Sheikh Ponda wakiwa Mto wa Mbu Monduli