Yaliyojiri kesi ya Mbowe leo Novemba 05, 2021: Inspector Mahita Mohamed atoa ushahidi


Kwani Uzi huu unashida Gani? Nyuzi zote ambazo hazina Maana JF huziondoa. Unataka tusijue Yanayo Endelea?
 
.....ina maana Sirro IGP alikuwa hajui yote haya?! Mbona mambo ya aibu haya. Sidhani kama Sirro hii kesi anaipenda hata kuisikia na akiona haya yanayoendelea mahakamani anajutia kauli yake. Na bado akina Kibatala watamtaka mahakamani kama shahidi.
Mkuu huu moto umeanza kupanda juu ya mnazi aliyeko juu anatamani kuruka tatizo urefu wa mnazi....
 
Jamaa watakuwa walioteshwa na roho mtakavitu... ha ha ha
 
Kitendo cha Kuingiza Maandamano yasiyo na Ukomo, kuwa Dhuru Viongozi wa Serikali afu unaambiwa wataje hao viongozi unaishia Kumtaja Sabaya ambaye amehukumiwa kwa Ujambazi. Basi kuna Mahali Kesi inakosa Mashiko, Kusema Nchi isitawalike, Uchaguzi usifanyike, Basi Unajua Kabisa hii Kesi ni ya Kisiasa.

Tujiulize.

Sabaya na wenzake wamehukumiwa kwa Ujambazi.

Afande Jumanne kamuwekea meno ya Tembo mzee wa Watu.

Hawa wengine, Hawana Majina ya Vituo vya mafuta, wala watu waliopanga nao kufanya hivyo Mikoa Mingine.

Je ni kweli Mbowe na Wenzie 3 wanaweza kulipua Vituo vya mafuta kwa mikoa 5, Kuendesha maandamano yasiyo na Ukomo wakati huo kuwadhuru viongozi?

Hii kesi, Nataka nione Hukumu Ya Jaji Itakuwaje.

Ila kitendo cha kutumia Polisi kama Shahidi wamejichanganya pakubwa maana polisi ni watu wa kukiuka Sheria katika kutekeleza majukumu yao.
 
Kwani Uzi huu unashida Gani? Nyuzi zote ambazo hazina Maana JF huziondoa. Unataka tusijue Yanayo Endelea?

Nazungumzia mada za hovyo zote kutia ndani na uzi huu. Hebu angalia alichoandika mtoa hoja.
 
Hi kesi mashahidi wameshashtuka inaweza kubaki mikononi mwao kutokana na matukio ya bosy wao Sabaya. Naona hi kesi ikibaki mikononi mwa Siro akiwa Kama kamanda wa usalama taifa.

Kila Shahid anamkwepa mwenzake katika maelezo yaliyopelekwa mahakamani.
 
Sheria ni fact na ushahidi sasa kama hakuna ushahidi kuwa kulikuwa na kikao cha kupanga, majina ya watu waliotakiwa kudhuriwa, hakuna maandamano yaliyofanyika na hakuna vituo vya mafuta vilivyolupuliwa sasa nini zaidi ya hapo.
 
Hawa Mawakili wa upande wa UTETEZI ukiwasiliza/kuwasoma hadi raha wallahi.

 
Maswli hayo mh. Hayana uzito stahili
 
Shahidi hapo awali akidodoswa na wakili wa serikali...

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama ukiwa Kama Afisa wa Polisi Majukumu Yako yalikuwa ni yapi

Shahidi: Ukamataji wa wahalifu, Upekuzi wa tuhumiwa na Maeneo, Kusafirisha Watuhumiwa



Halafu punde kidogo wakati akidodoswa na upande wa utetezi...anakana moja ya jukumu alilolitaja kama sehemu ya JD yake...

Kibatala: Pale Rau Madukani, nani alikuwa Arresting Officer

Shahidi: Mimi hapa

Kibatala: Unafahamu au hufahamu kwamba ukisoma pamoja kifungu cha 23 cha CPA pamoja na PGO, arresting person ndiyo anapaswa kufanya search, Je unafahamu hilo?

Shahidi: Siyo lazima
 
Nchi imetekwa na upotofu hii.

Wananchi wote tuko ndani ya basi bovu, viti vichafu, kuna joto ndani, dereva mlevi halafu anaendesha kwa kasi sana huku akinena maneno machafu dhidi ya abiria.....The Beautiful Ones Are Not Yet Born
 
Kama kwa upande wako huna cha kujifunza kwenye hii kesi, basi wewe utakuwa ni mwanadamu outdated kabisa! Na huenda wewe ndiyo anaye ota! Maana kama huamini hivi namna mashahidi wenzako wanavyo jichanganya pale mahakamani.

Na hayo mawazo yako ya kufa kwa JF yasahau! Maana utatangulia wewe, na JF itabaki milele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…