Imekopiwa kutoka Twitter kwa account ya Martin Malanja
www.twitter.com/IAMartin_
Saa 09:23 | 20/09/2021 East Africa Time.
Polisi wametuzuia mimi na Boniface Jacob tusiingie mahakamani. Wanasema wanayo majina mawili. Boniface Jacob na Martin Maranja Masese. Tumewashauri kama kuna kosa la jinai tumefanya basi watukamate, wanasema hapana, maelekezo ni kutoingia ndani ya mahakama.
Kimsingi tumewashauri, kama wanataka kesi iendelee, basi waruache tuingie ndani ya mahakama kwa sababu hakuna kosa la jinai ambalo tumelifanya. Lakini wameendelea kushikilia msimamo wao, hadi a sasa hakuna kiongozi Wala mtu wa CHADEMA aliyefanikiwa kuingia ndani ya mahakama.
Mageti yote mawili wameweka askari ambao wametuzuia. Hakuna kuingia ndani. Wakili Peter Kibatala anaenda na Wakili Fred Kihwelo wamekwenda kuongea na wahusika wa mahakama, lakini wakati huo sisi wakulungwa tusioruhusiwa bado tupo nje ya geti.. The guilty are afraid.
Nimekuwa the mhalifu? Nazuiwa vipi kuingia mahakamani kwa maelekezo maalum?? For what purpose? What a wasted country... Tuliambiwa tumepata uhuru kutoka kwa mkoloni ili tuweze kuwa huru.. Lakini bado kuna tabaka limeshikilia uhuru wetu hata wa kuhabarisha umma. Hii siyo sawa...
JAJI MKUU, tafadhali linda hadhi ya mahakama. EXECUTIVE inatakiwa kuheshimu JUDICIARY na sio kupanga utaratibu wa nani anatakiwa kuingia na nani asiingie mahakamani. Huu ni mhimili muhimu, unaojitegemea, mahakama inapaswa kuwa huru. Tuilinde ibara ya 107B ya katiba ya JMT
View attachment 1945855View attachment 1945856
Fellas, It's on!
Tupo ndani tayari. Hakuna kosa la jinai kuhabarisha umma kuhusu mwenendo wa kesi. Labda kama Jaji atakaa na kusema tumevunja sheria. Kama tumetenda jinai, tushtakiwe, lakini hadi sasa sisi ni raia wema kwenye Taifa letu la wababe wenye dola..
View attachment 1945860View attachment 1945861
Mawakili wetu wasomi wamefika na kuketi katika sehemu yao...
View attachment 1945865
Freeman Mbowe na wenzake watatu wameletwa tayari na gari la magereza.. Wamefika mahakamani saa 3:45 saa za Afrika ya mashariki...
Freeman Mbowe na washtakiwa wengine watatu wameidhinisha msimamo wetu kuwa kwa sababu yoyote ile kama wakizuiwa watu wa familia zao, mawakili au viongozi wa chama, basi mawakili wasiendelee na kesi hadi watu wote waruhusiwe kuingia ndani na mahakama.
Polisi wameweka na daftari la kusaini kuingia mahakamani. Tumewauliza kwanini mnatuzuia? kuna jinai tumetenda? Wanasema hapana. Shida ni nini sasa? Wanasema maelekezo kutoka juu. Tukawaeleza hii kesi mtafanya ihairishwe bure bila kujua. Kesi haipo hadi wote tuwe ndani, full stop!
Kimsingi, mahakama sasa imejaa pomoni, watu wote waliokuwepo nje, wameingia ndani, siti zote na mawakili wa utetezi wapo tayari, na wanasubiri mawakili wa serikali na Judge waingie ndani ya chumba cha mahakama.
Mawakili wa Utetezi waliofika mahakamani hadi sasa ni
Peter Kibatala
Jeremiah Mtobesya
Fred Kiwhelo
John Malya
Gaston Garubindi
Seleman Mtauka
Michael Mwangasa
Evaresta Kisanga
Khadija Aron
Maria Mushi
Adv. Maria Mushi,
Adv.Hadija Aron,
Adv. Evarista Kisanga.
Mawakili wetu wanawake, wanaunda pia Jopo la mawakili wa utetezi, tayari wapo katika nafasi zao katika dawati la mawakili wa utetezi.
Wakili Jebra Kambole (@Advocate_Jebra) pia yupo mahakamani leo. Ametoka Njombe alipokwenda kuwatetea wanachama wetu wa CHADEMA ambao wapo gerezani tangu August 2020.. Zile porojo za MaCCM kuwa amekataa kufika mahakamani, nadhani tuzipuuze, ni upuuzi mwingine.
View attachment 1945878
Kushoto ni Adv. Fred Kihwelo (@FrederickWakili).. Kulia ni Adv. John Mallya (
johnmallya) na Leo wapi wote mahakamani, katika jopo la mawakili wa utetezi.. Leo ni siku ya kuzaliwa ya Adv. Fred Kihwelo.. Tumtakie heri ya siku ya kuzaliwa na tuifuate akaunti yake.
View attachment 1945881
Kushoto, @FrederickWakili
Mbele,
johnmallya
Aliyesimama, @Advocate_Jebra
View attachment 1945892View attachment 1945893
Wakili Fred Kiwhelo ndiye wakili Mratibu, Adv. Fred pamoja na kazi kubwa wanayoifanya mahakamani na wenzake lakini ndiye wakili anayekwenda gereza la UKONGA kumpatia Freeman Mbowe briefing ya kesi kila mara.
Huyu ana LL.B ya UDSM na M.A UDSM.
View attachment 1945895
-----------------------
Jaji ameingia mahakamani..
Kesi Na. 16 ya mwaka 2021 inatajwa..
Kesi namba 16 ya 2021, jamhuri dhidi ya Khalfan Bwire, Adam Hassana Kasekwa (Adamoo), Mohammed Abdalah Ling'wenya na Freeman Aikael Mbowe
Jaji anamuita Wakili wa Serikali...
Wakili wa Serikali anatambulisha Jopo lake..
1. Robert Kidando
2. Nassoro Katuga
3. Ignas Mwanuka
4. Esther Martin
5. Tulumanywa Majigo
Pia anawatambulisha mawakili na mawakili wengine watatu.
Jaji anaita wakili upande wa utetezi.
Wakili Kibatala anatambulisha Jopo la utetezi
Peter Kibatala
Jeremiah Mtobesya
Fred Kihwelo
John Malya
Gaston Garubindi
Seleman Mtauka
Michael Mwangasa
Evaresta Kisanga
Khadija Aron
Maria Mushi
Deogratius Mahinyila
Nashon Nkungu
Jebra Kambole
anasema anamtambulisha Wakili Fredrick Kihwelo kwa sababu maalum
Kibatala anatambulisha Mawakili wa mshtakiwa wa kwanza kuwa ni Jeremiah Mtobesya na Nashon Nkungu..
Mshtakiwa wa tatu atawakilishwa na Dickson Matata na Fredrick Kihwelo
Mshtakiwa wa pili atawakilishwa na John Mallya
Mawakili wengine wote watamwakilisha mshtakiwa wa nne
Jaji anauliza kama mawakili wa serikali wanalolote Juu ya ingizo Jipya la wakili Fredrick Kihwelo kama kuna mgongano wa maslahi..
Wakili wa Serikali anasema hakuna tatizo kwa sababu tangu kesi ianze hajaonekana kwenye Column yoyote.
Jaji: hiyo wakili Fredrick Kihwelo anamshikia mikoba wakili Dickson Matata au atakuwa moja kwa moja kwa mshtakiwa watatu?
Kibatala: kuanzia leo mshtakiwa watatu atawakilishwa na wakili Fredrick Kihwelo na kusaidiana na Dickson Matata ambaye leo hayupo mahakamani
Wakili wa serikali anahoji mshtakiwa mwenyewe anasemaje baada ya kumsikiliz Kibatala
Jaji: hilo tayari nimeshaliongelea kuwa baada ya utambulisho wa Kibatala nitamuhoji Mshtakiwa
Jaji: Ling' wenya bila shaka umesikia?
Ling'wenya; Nimesikia Mh. nakubaliana na Wakili Kibatala
Jaji: hiyo wakili Fredrick Kihwelo anamshikia mikoba wakili Dickson Matata au atakuwa moja kwa moja kwa mshtakiwa watatu?
Kibatala: kuanzia leo mshtakiwa watatu atawakilishwa na wakili Fredrick Kihwelo na kusaidiana na Dickson Matata ambaye leo hayupo mahakamani