Yaliyojiri kesi ya Wabunge 19 waliovuliwa uanachama Vs CHADEMA. Mahakama yaridhia Ubunge wao uendelee wakati kesi ikiendelea
Haleluyaa aaaahh haleluyaaa haaaa,

Yaani mtanyooka tu, katiba ya Chadema hamuifuati halafu mnataka katiba mpya, mnacheza nyimbo za kichaga, hiyo kesi ichukue hata miaka kumi, sawa tu
Nchi haina mahakama wala Bunge
 
Siasa zetu tamu sana

baada ya karibia mwaka kuwa busy na hashtag za kupigania Mbowe kuachiwa

sasa hivi wametengenezewa agenda ya kuwaweka busy hadi mwishoni mwa 2024

Tunashukuru wabunifu wetu

Hakuna mwenye akili hiyo ya kuwatengenezea watu ajenda. Haya watu wanajadili kwa mapenzi yao, usitake kujifanya kwamba kuna akili hiyo. Wanayoyatengeneza yajadiliwe ni hizo bajeti na miradi yao, ambayo haina mvuto wa hivyo. Haya mengine ni coincidence. Vinginevyo unionyeshe hilo kundi lenu lenye watu waelewa ni kipi mnajadili nje ya haya tunayojadili hapa.
 
Nchi haina mahakama wala Bunge
Nenda kafanye mauaji ndio utajua mahakama ipo ukishadakwa.

Mahakama isafishe uhuni wote wa vikao vya chadema, haiwezekani usajili katiba, halafu usiifuate, mahakama ,piga hao nyamaume
 
Mahakama ya Mchongo!
 
Nenda kafanye mauaji ndio utajua mahakama ipo ukishadakwa.

Mahakama isafishe uhuni wote wa vikao vya chadema, haiwezekani usajili katiba, halafu usiifuate, mahakama ,piga hao nyamaume
Pole Kwa familia yako
 
Bonge moja la mahakama , hii mahakama nimeikubali, inatenda haki bila pressure
 
Kama Kuna Jaji wa hovyo Ni huyu Mgeta, hopeless, Shyster judges!
 
Ninacho jiuliza mawakili wa serikali wanahusika vipi na hii kesi ya michongo
 
Ni kinyaa kitupu ukisikiliza anachosema. Huwa najiuliza imekuwaje tunaongozwa na watu wajinga wa kiwango hiki. Cha ajabu watu wanaofanya haya wanajiita ni wasomi!

Nilichogundua baada ya ccm kupoteza ushawishi kwa umma na kuamua kutumia vyombo vya dola kukaa madarakani kwa shuruti, kumetokea ukiukwaji mkubwa wa sheria, na hali inazidi kuwa mbaya labda CDM ifutwe au wakubali kutawaliwa na ccm kwa mabavu. Na tabia hii ya ukiukwaji mkubwa wa sheria itachukua muda mrefu hadi hali halisi kujirudia.
Kaa Kwa kutulia , huu mchezo hauhitaji hasira chief
 
Haleluyaa aaaahh haleluyaaa haaaa,

Yaani mtanyooka tu, katiba ya Chadema hamuifuati halafu mnataka katiba mpya, mnacheza nyimbo za kichaga, hiyo kesi ichukue hata miaka kumi, sawa tu
Chawa hujielewi, naona mama yako unayemsifia huku kila siku analeta maridhiano leo kajivua nguo unamfichia aibu kwa kujichekelesha tu
 
Sasa Spika aliwaruhusuje kuendelea kubaki Bungeni wakati hakuwa na zuio la Mahakama?

Eti huyu ndio mwanasheria wa kiwango cha Phd na ndio anaongoza Bunge.

Hii nchi imepatwa mchana kweupe

Kwa vituko hivi, ndio mjue hapa hata kesi hamna.
Kupatwa Kwa jua hakuna taarifa ila utabiri utabiri tuu🤔
 
Kesi namba 16 ya mwaka 2022 iliyofunguliwa Mahakama Kuu na Wabunge 19 wa viti maalum wa CHADEMA kupinga uamuzi wa kuwavua uanachama na mwenendo mzima wa maamuzi yaliyofanyika dhidi ya Baraza la Wadhamini CHADEMA, tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kaa nami kujua yatakayojiri Mahakama Kuu, Dar.

==========

Wakili Peter Kibatala na Wakili John Malya tayari wapo ndani ya Chumba Cha Mahakama Mbele ya Jaji Mgeta.

Jopo la mawakili wa Chadema lina mawakili wanne Adv. Kibatala Adv. Mtobesya Adv. J. Mndeme Adv. j. Malya Wengine. Kesi namba 16 ya Mwaka 2022, Mdee na Wenzake 18, ilifunguliwa Mahakama Kuu Mbele ya Jaji Mgeta.

Mdee na wenzake 18 Wanawakilishwa na Mawakili Adv Ikupilika Panya, Adv Edson Kilatu na Adv Aliko Mwamanenge. Baadae likaingia Jopo la Mawakili wa Serikali wapo Wanne Wakiongozwa na Wakili Gabriel Mallata.

Mawakili wa Mdee na wenzake wametoa ombi la Mahakama Iweke zuio "Court Injunction"Wasivuliwe Ubunge na Bunge. Wanaomba Kwanza Mahakama itoe zuio la Mdee na wenzake waendelee Kuwa wabunge mpaka pale ambapo Kesi ya msingi Kesi itakapoisha. Baada Wasilisho lao, Mahakama italazimika Kusikiliza Ombi hilo Kwanza kutoka pande zote.

Amesimama wakili Peter Kibatala anachambua kwanza Viapo vyao ambavyo vimesainiwa na Mawakili wao na Wateja (Wakina Mdee)
  1. Viapo havionyeshi waapaji (Wakina Mdee) Wameapa wapi.
  2. Waapaji hawajataja Dini zao katika Viapo vyote
  3. Ombi lao la kubaki na ubunge halijaelekezwa kwa yoyote kati ya wadaiwa (Mdee na wenzake)
  4. Katika maombi yao hawasemi kama wanataka kuendelea kuwa wanachama wa Chadema ila wanataka kuendelea na ubunge tu.
Mawakili wa CHADEMA wanaendelea Kuchambua Viapo na Kutaja Mahitaji ya Kisheria na sifa zinazohitajika katika Viapo wakiwa na Lengo Kuweka Zuio la awali, preliminary Objection (P.O) Mahakama isikubali Kupokea Maombi yao ya kesi.

Mawakili wa Halima Mdee na wenzake kwa pamoja na Mawakili wa Serikali Wanafanya (Re-joinder) Wanasimama kujibu hoja za Jopo la Mawakili wa Chadema Kuhusu hitilafu katika Viapo na Mapungufu yake katika ufunguaji wa Kesi.

Majibu ya wakili wa Halima Mdee na wenzake 18
  1. Wamesema hawajataja dini lakini kiapo kinajieleza
  2. Wahusika wanaoombewa amri wametajwa kwenye Viapo
  3. Wamekubali baada ya kuelekezwa na Mahakama kwamba inaongeza jambo jipya
  4. Kuhusu kumuunganisha Speaker au Katibu wa Bunge, amri zilizoombwa zimeombwa na wahusika ambao wapo kwenye Maombi yaani Chadema, NEC (tume ya Uchaguzi) na Mwanasheria Mkuu
  5. Kuhusu kwamba NEC ina ulinzi wa Katiba chini ya ibara ya 74(12), hakuna sehemu ambayo wao wameombwa kuchunguza NEC
  6. Kuhusu kwamba hakuna hatari yoyote inayopelekea kutolewa kwa amri iliyoonyeshwa na waleta maombi, wamesema hii ni amri ya upande mmoja na kwenye hayo maombi ya amri hiyo; wameomba kwamba wasitolewe kama wabunge wa viti maalum Kwamba wadaiwa wanajua kwamba watatolewa kuwa Wabunge.
Mawakili wa wabunge 19 na Wanasheria Serikali wanaomba wapewe "status quo" Wakitaka Wakina Mdee na wenzake Waendelee Kuwa Wabunge mpaka Kesi ya Msingi itakapo malizika Kusikilizwa.

Yanasubiriwa maamuzi ya Jaji

Jaji Mgeta ametoa zuio la Muda, "Status quo" Wakina Mdee Waendelee Kuwa Bungeni mpaka tarehe 13 June 2022 ambapo Nyaraka zitalepelekwa Mahakamani ambapo Kesi zote mbili zitaendelea Kusikilizwa

Pia, soma=> Wabunge 19 viti maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama kuu

Tanzania nchi ya ajabu sana kisheria hawa wabunge ambao wamefukuzwa kwa kugushi! wanaruhusiwa kuendelea na ubunge kwa kujichagua wenyewe kama kweli waligushi!. Mahaka inawaruhusu na kesi itachukua mwaka kusikilizwa tena tusiko kuwa makina na wakishashidwa watakata rufaa tena hivyo watabaki bungeni mpaka 2025. Ukiwa na utaratibu wa sheria wa hivi ni tatizo sana hasa kama kweli watagunduliwa wame gushi. Tujue kwamba ushahidi wa kwamba hawajagushi haupo na utaratibu mzima waligoma kutuma hizo documents ambazo ndiyo wanasema Mwanyika amepiga sahihi!
Pascal Mayalla

Kuna kitu nakiona hapa .... mama SSH anataka kuwatoa hawa covid-19 bungeni kwa kutumia mgongo wa mahakama ili isionekane ni shinikizo ... watch this pace
Angeweza kulia ha Bunge litende haki kwamujibu wa sheria na bado ikampa Legacy yake
 
Kesi namba 16 ya mwaka 2022 iliyofunguliwa Mahakama Kuu na Wabunge 19 wa viti maalum wa CHADEMA kupinga uamuzi wa kuwavua uanachama na mwenendo mzima wa maamuzi yaliyofanyika dhidi ya Baraza la Wadhamini CHADEMA, tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali inaendelea Mahakama Kuu.

Kaa nami kujua yatakayojiri Mahakama Kuu, Dar.

==========

Wakili Peter Kibatala na Wakili John Malya tayari wapo ndani ya Chumba Cha Mahakama Mbele ya Jaji Mgeta.

Jopo la mawakili wa Chadema lina mawakili wanne Adv. Kibatala Adv. Mtobesya Adv. J. Mndeme Adv. j. Malya Wengine. Kesi namba 16 ya Mwaka 2022, Mdee na Wenzake 18, ilifunguliwa Mahakama Kuu Mbele ya Jaji Mgeta.

Mdee na wenzake 18 Wanawakilishwa na Mawakili Adv Ikupilika Panya, Adv Edson Kilatu na Adv Aliko Mwamanenge. Baadae likaingia Jopo la Mawakili wa Serikali wapo Wanne Wakiongozwa na Wakili Gabriel Mallata.

Mawakili wa Mdee na wenzake wametoa ombi la Mahakama Iweke zuio "Court Injunction"Wasivuliwe Ubunge na Bunge. Wanaomba Kwanza Mahakama itoe zuio la Mdee na wenzake waendelee Kuwa wabunge mpaka pale ambapo Kesi ya msingi Kesi itakapoisha. Baada Wasilisho lao, Mahakama italazimika Kusikiliza Ombi hilo Kwanza kutoka pande zote.

Amesimama wakili Peter Kibatala anachambua kwanza Viapo vyao ambavyo vimesainiwa na Mawakili wao na Wateja (Wakina Mdee)
  1. Viapo havionyeshi waapaji (Wakina Mdee) Wameapa wapi.
  2. Waapaji hawajataja Dini zao katika Viapo vyote
  3. Ombi lao la kubaki na ubunge halijaelekezwa kwa yoyote kati ya wadaiwa (Mdee na wenzake)
  4. Katika maombi yao hawasemi kama wanataka kuendelea kuwa wanachama wa Chadema ila wanataka kuendelea na ubunge tu.
Mawakili wa CHADEMA wanaendelea Kuchambua Viapo na Kutaja Mahitaji ya Kisheria na sifa zinazohitajika katika Viapo wakiwa na Lengo Kuweka Zuio la awali, preliminary Objection (P.O) Mahakama isikubali Kupokea Maombi yao ya kesi.

Mawakili wa Halima Mdee na wenzake kwa pamoja na Mawakili wa Serikali Wanafanya (Re-joinder) Wanasimama kujibu hoja za Jopo la Mawakili wa Chadema Kuhusu hitilafu katika Viapo na Mapungufu yake katika ufunguaji wa Kesi.

Majibu ya wakili wa Halima Mdee na wenzake 18
  1. Wamesema hawajataja dini lakini kiapo kinajieleza
  2. Wahusika wanaoombewa amri wametajwa kwenye Viapo
  3. Wamekubali baada ya kuelekezwa na Mahakama kwamba inaongeza jambo jipya
  4. Kuhusu kumuunganisha Speaker au Katibu wa Bunge, amri zilizoombwa zimeombwa na wahusika ambao wapo kwenye Maombi yaani Chadema, NEC (tume ya Uchaguzi) na Mwanasheria Mkuu
  5. Kuhusu kwamba NEC ina ulinzi wa Katiba chini ya ibara ya 74(12), hakuna sehemu ambayo wao wameombwa kuchunguza NEC
  6. Kuhusu kwamba hakuna hatari yoyote inayopelekea kutolewa kwa amri iliyoonyeshwa na waleta maombi, wamesema hii ni amri ya upande mmoja na kwenye hayo maombi ya amri hiyo; wameomba kwamba wasitolewe kama wabunge wa viti maalum Kwamba wadaiwa wanajua kwamba watatolewa kuwa Wabunge.
Mawakili wa wabunge 19 na Wanasheria Serikali wanaomba wapewe "status quo" Wakitaka Wakina Mdee na wenzake Waendelee Kuwa Wabunge mpaka Kesi ya Msingi itakapo malizika Kusikilizwa.

Yanasubiriwa maamuzi ya Jaji

Jaji Mgeta ametoa zuio la Muda, "Status quo" Wakina Mdee Waendelee Kuwa Bungeni mpaka tarehe 13 June 2022 ambapo Nyaraka zitalepelekwa Mahakamani ambapo Kesi zote mbili zitaendelea Kusikilizwa

Pia, soma=> Wabunge 19 viti maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama kuu
Mahakama za mchongo
 
Kwa kweli jukwaa la siasa Jf baada ya kuwa jukwaa la malumbano ya hoja limekuwa jukwaa la kutukanana na kuvunjiana heshima...hamaki na mihemko imetamalaki kuliko weledi...........

Wanaohubiri haki na demokrasia ndio wasiopenda au kuvumilia maoni ya wenzao........

JF inashuka thamani sana na hii mihemko.....
 
Back
Top Bottom