Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kutoka Diamond Jubilee Mkutano Mkuu wa ACT–Wazalendo: Membe apata kura za Ndiyo 410 za Urais Tanzania, Maalim Seif Ndiyo 419 za Zanzibar

combination ya ACT na CDM ingefaa sana maana ACT inaonekana kidogo ina watu wenye msimamo na wanaojielewa ukiiweka kapu moja na CDM naamini nchi itasimama kuelekea hiyo october..

Siasa za ungangali za CUF enzi zile naona zimeamia ACT ukimuweka na ZZK na vijana wake waKG naamini CCM itatingishika..
 
"Serikali yetu ya #KaziNaBata haitaweza kufikiwa kama wasanii na wanamichezo wataendelea kunyonywa na kufanya kazi katika mazingira magumu. Kwa kushirikiana na wasanii na wanamichezo mbalimbali, serikali yetu itawekeza kwa kiwango kikubwa kuhakikisha vipaji na vipawa vya watanzania vinakuwa vyenye tija kwao, burudani kwetu na tunu ya taifa katika majukwaa ya kimataifa. "

Zitto Kabwe
Kiongozi wa Chama
 
Kwanini chadema wasiwaunge mkono ACT?
Tunaangalia nan mwenye raslimali watu wengi

Pili nan anamvuto kulinganisha na mwingne

Chadema tayar wanae mwenye mvuto kwa watanzania wengi

Tatu tunaangali ni nan ambae amejitahidi kupenya mpka ngazi ya chini chadema hapa tayar wako mpaka ngazi ya chini
 
Kwani mkiiunga mkono ACT hao watu automatically si wanaenda kuipigia kura act?
 
Mtaa wa saba wanakunywa panadol...hali si hali...homa inapanda na kushuka

Lissu & Membe & Maalim ndiyo habari ya mjini kwa sasa!!

Hutaki meza viwembe!!
 
"Ndugu zangu wa @ACTwazalendo, nimeona marafiki zangu wengi sana. Naomba nianze kwa kusema ahsante sana marafiki zangu kwa kunialika nije kushiriki nanyi katika Mkutano wenu Mkuu."

Tundu Lissu

#MkutanoMkuuACT2020
#KaziNaBata
#TheFutureIsPurple
 
Kwenye siasa hakuna kuaminiana. It is a dirty game na kila mtu anaangalia tumbo lake kwanza. Mchezo huu wa kuachiana majimbo unasemekana ndiyo ulikididimiza NCCR mageuzi katika uchaguzi uliopita.

Kwa vyo vyote vile Zitto kacheza pele kwa sababu kule Zanzibar atapata majimbo mengi tu na huku bara atapiga majimbo kadhaa huko Kusini kama Membe atagombea. Na kwao Kigoma. Kazi itakayobakia ni kuhondomola mabilioni ya ruzuku tu. Mwanasiasa umpe nini tena?
 
Safi sana huyu shetani wa kisiasa CCM Mpya mwaka huu 2020 anashambuliwa kwa hoja toka pande zote za upinzani.

Hali hii ya madhaifu ya CCM Mpya kuanikwa peupe itasaidia wapiga kura kufanya maamuzi sahihi ya kumkataa CCM Mpya na kazi zake zote alizofanya kati ya 2015 - 2020.
 
Hivi membe ni mgombea raisi wa Atc? ha ha ha , au tundulissu?
 
Mwaka Huu Lazima Kieleweke
TUNDU LISSU ASIMAMISHA MKUTANO WA ACT WAZALENDO KWA MUDA, ASHANGILIWA
5 Aug 2020
Hivi ndivyo mgombea urais aliyepitishwa na chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Antipas Lissu alivyoingia kwenye mkutano mkuu wa ACT Wazalendo na kusimamisha shughuli za kiitifaki kwa muda

Source : mwananchi digital
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…