Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kutoka Diamond Jubilee Mkutano Mkuu wa ACT–Wazalendo: Membe apata kura za Ndiyo 410 za Urais Tanzania, Maalim Seif Ndiyo 419 za Zanzibar

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kutoka Diamond Jubilee Mkutano Mkuu wa ACT–Wazalendo: Membe apata kura za Ndiyo 410 za Urais Tanzania, Maalim Seif Ndiyo 419 za Zanzibar

"Ninafuraha kubwa sana kuwa leo tupo tumejumuika hapa kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa Chama chetu hichi chenye miaka 6 tokea kuanzishwa kwake. Ni chama kichanga kuliko vyama vyote vilivyopo Tanzania kwa umri wake."

Zitto Kabwe
 
Kuna wakati najiuliza hivi upinzani ni fikira za kusadikika au ni fikira zinazo ishi

Kama kweli chama cha ACT WAZALENDO

Kilikuwa na nia ya kushirikiana na chadema kilipaswa kuachana na mpango huu kilipaswa kiseme tunaungana na chadema kwenye uraisi

Na kwenye ubunge wangetengeneza majimbo ya kimkakati hii ingeonyesha hapa ndio upinzan unakuja na maono ya kukua sasa na nyinyi mnachagua tena wagombea ili wakashindane na ccm au chadema

Inawezekana walio chagua upande mapema hata kama maamuzi yao yalionekana ya kipuuzi kuliko mnao chagua kugawana kura


Au chama cha Act ndio walitaka wasimamishe mgombea na wakati chadema ila raslimali watu

Kweli adui wa upinzan ni wapinzan wenyewe
Kwanini chadema wasiwaunge mkono ACT?
 
Mkuu tuheshimiane, huyo ni shemeji yako. Watu tumewekeza hapo.
Mkuu, kama umewekeza kwa yule mwanamke, hata tendo utakuwa unapata kwa kufuata vifungu vya sheria! Maana si kwa ujeuri na ujuaji ule!
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Chama cha ACT–Wazalendo leo tarehe 05 Agust 2020 kinafanya Mkutano wake Mkuu Diamond Jubilee–VIP Hall.

#MkutanoMkuuACT2020
#KaziNaBata
#TheFutureIsPurple
=====

UPDATES

======


AJENDA KUU

1. Kupitisha na kutangaza majina ya wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar

2. Kupitisha Ilani ya Chama ya 2020 kwa Uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano na Uchaguzi wa Zanzibar.

Sasa kinachoendelea na utambulisho na Ufunguzi kwa Maombi kutoka Madhehebu mbalimbali.

1153HRS: Maalim Seif anaingia kufungua Mkutano rasmi



Hotuba ya ufunguzi -- Maalim Seif Hamad

Ndugu kiongozi wa chama, ndugu makamo wa mwenyekiti, ndugu katibu mkuu na manaibu wako. ndugu wajumbe wa kamati kuu ndugu wajumbe wa halmashauri ya kamati kuu ya taifa ndugu wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa ndugu, ndugu wajumbe na wananchi na ndugu waalikwa wageni wetu.

Ndugu wananchi mkutano mkuu wa chama chetu leo umekutana, nina furaha kubwa kuwa leo tupo tumejumuika hapa kwenye mkutano mkuu wa chama hiki chenye miaka 6 tokea kuanzishwa kwake ni chama kichanga kuliko vyama vyote na kwakweli pamoja na uchanga wake ndugu Membe aliwahi kusema kuwa ni chama kinachokuwa kwa haraka kabisa.

Ngugu viongozi nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kukutana yena mara ya mwisho tulikutana mwezi Machi tulipokuwa na mkutano mkuu wa kawaida na mwezi huu wa nane tunakutana kwa mkutano mkuu maalum.

msajili tunamsubiri aifute CHADEMA na ACT wabaki na TLPCCM NA Cufccm
 
Mkuu, kama umewekeza kwa yule mwanamke, hata tendo utakuwa unapata kwa kufuata vifungu vya sheria! Maana si kwa ujeuri na ujuaji ule!
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Kipendacho roho shehe.
 
Maalim Seif anasema safari hii CCM wasidhani kuwa Iwapo atashinda uchaguzi Zanzibar halafu CCM wakaleta figisu basi atafunga mikono, Safari hii anasema haki lazima iheshimiwe!
Miaka yote kabla ya uchaguzi huwaga anasema hivyo!
Mwaka juzi alisema atapewa urais wake baada ya miezi 3 mpaka leo miezi 3 haijwahi kufika
 
Zitto is speech tactician..... presentation yake ni level ya juu kabisa
 
"Tunataka Serikali ambayo itajikita katika kufufua na kuimarisha uhusiano wetu na mataifa mengine na haswa nchi jirani. Tumedhamiria kurudisha heshima ya Tanzania kwenye medani ya kimataifa."

Zitto Kabwe
Kiongozi wa Chama
 
Acha siasa za kitoto ww mkuda.

Wewe ndio umepewa kazi ya kunifanyia stalking hapa mtandaoni. Nimekugundua kwa staili yako ya kubadilisha rangi za mavaz katika sura na mwili uleule.
 
“Ni uchaguzi wa kuchagua Uhuru wa kweli kwa kila mtu dhidi ya ukandamizwaji.”

@zittokabwe
IMG-20200805-WA0056.jpg
 
Back
Top Bottom