Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye kampeni za mgombea Urais wa CHADEMA, Mh Tundu Lissu Mkoani Mara, Serengeti

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye kampeni za mgombea Urais wa CHADEMA, Mh Tundu Lissu Mkoani Mara, Serengeti

Duh huyu jamaa anakubalika mpaka kero.
Hivi mkurugenzi si alitoabarua kuwa lisu mkutano wake ulikuwa tarehe 27 Leo sio ratiba ya Serengeti kwa hiyo imeshindikana kumzuia kufanya mkutano serengeti
IMG_20200928_170430.jpeg
 
Lissu ni kichaa, hanadi sera hata siku moja ye ananadi mapambano tu kwamba lazima atangazwe kwa sababu watu walikuja kusikiliza mkutano, basi lazima awe mshindi la sivyo damu itamwagika, huyu kichaa ametumwa anatumiwa kama zombie na wazungu
Hivi lisu na magu nani ni kichaa?magu yeye alishasema yeye ni kichaa tena hadharani
 
Hizo kwenye uwanja wa medani huwa zinatumika kuwatoa watu mteru 😅😅😅, hahahah! acheni kulialia CCM inaendelea kusonga mbele.

Ushindi ni kawaida yetu CCM.

JPM ANATOSHA
CCM USHINDI NI JADI
Mkuu unafahamu umeandika madudu gani ?
 
Mkuu unafahamu umeandika madudu gani ?
Huelewi maana ya CCM kushinda tokea lini ukasikia CCM inashindwa?
Watanzania wanataka maendeleo sio porojo.

JPM ANATOSHA
CCM USHINDI NI JADI
 
😂, unajitetea mapemaaa! Unaogopa kupopolewa mawe, kamanda!?
Mkuu waweza tupiwa mawe, na kumwagiwa nyuki humu, wacha mchezo kabisaa, ni hataariii...
Watu nyuma ya keyboard lakini wana medani zote za kivita. 😀 😀

Everyday is Saturday.................................😎
 
Lissu anatia moyo sana, atlist ni mpinzani ambae anaaminika
 
Patachimbika , yako mengi ningekunong'oneza lakini jf ina sheria zake
Mbona tumeengua madiwani wenu karibu 500 Lakini hamjafanya chochote??


Tume ya uchaguzi hebu tuondoleeni huyo mpuuzi naona dharau zimezudi.
 
28 September 2020
Mugumu, Serengeti
Tanzania

Tundu Lissu apokewa kwa kishindo, atoa somo kuhusu kuitwa tarehe 29 /9/2020 Dodoma kufuatia malalamiko ya kutuhumiwa kukiuka maadili ya uchaguzi

First Lady mtarajiwa Alicia Lissu amepanda jukwaani na kuwaambia waTanzania wote kuwa yeye Alicia kama mwanasheria, basi bila shaka waTanzania watambue kuwa Tundu Antipas Lissu akiingia Ikulu yeye Alicia Tundu atakuwa anamsumbua na kumkumbusha kila siku Rais Tundu Antipas Lissu kutetea haki za binadamu ili wananchi wa Tanzania waishi kwa Uhuru, Haki bila kunyanyaswa kama ilivyo sasa kwa miaka mitano ya CCM Mpya 2015 - 2020 inayoishia Oktoba 28 2020

Malalamiko ya wanaokiuka Maadili ya Uchaguzi basi serikali au chama husika kitawakilisha kwa maandishi malalamiko kwa Tume ya Uchaguzi.

Mpaka sasa hakuna taarifa ya mgombea wa chama, chama au Tume wamewakilisha malalamiko kwake Tundu Lissu au kwa chama chake CHADEMA.

Hivyo kukosekana kwa barua ya malalamiko iliyowakilshwa Tume ya Uchaguzi maana yake Tundu Lissu hawezi kwenda Dodoma kesho tarehe 29/09/ 2020.

Ratiba ya mgombea urais 2020 kufanya kampeni eneo la Mugumu Serengeti unaoonesha mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA Mh. Tundu Lissu ulitaka kuvurugwa leo na Mkurugenzi wa Uchaguzi huku nakala ikipelekwa kwa OCD, DSO na DC wote wilaya ya Serengeti.

Baada ya maneno hayo ktk ufunguzi wa kampeni Tundu Lissu anarejea suala la Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu wanaoishi ktk maeneo maalum tengefu .... kama Mugumu Serengeti na maeneo mengine kama hayo Tanzania nzima ....
 
Mbona tumeengua madiwani wenu karibu 500 Lakini hamjafanya chochote??


Time ya uchaguzi hebu tuondoleeni huyo mpuuzi naona dharau zimezudi.
Tunashinda uchaguzi na tutatangazwa chini ya shinikizo , na tutarudia chaguzi kila palipofanyika figisu
 
Back
Top Bottom